Mnyika acha visingizio

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Hebu acha kujitembeza. Njoo hapa ujibu maswali yako na ya mwenyekiti wako, usijifiche miongoni mwa wamachinga

Chadema kutetea wamachinga

Na Muhibu Said

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeipa serikali mwezi mmoja kueleza hatua ilizokwishachukua kuhusu ahadi ilizozitoa kwa wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga, vinginevyo kitachukua hatua mbalimbali, ikiwamo kushawishi nguvu ya umma kutekeleza watakayoona yanafaa.

Ahadi hizo ni pamoja na kuwawezesha kwa kuwapatia mitaji ya biashara, mafunzo na ujuzi.

Kauli hiyo ya Chadema, ilitolewa na Mwenyekiti wa Vijana Taifa , John Mnyika, wakati wa uzinduzi wa ripoti ya uchunguzi wa mwenendo wa biashara ya wafanyabiashara ndogondogo katika Jiji la Dar es Salaam, uliofanyika katika Soko la Kigogo Sambusa jana.

Uzinduzi huo uliongozwa na Mbunge wa Viti Maalum wa chama hicho, Mhonga Ruhwanya, ambaye alikuwa mgeni rasmi.

"Serikali inapita inasema mabilioni ya JK, ukiuliza ni wamachinga wangapi wamepata hayo mabilioni ya JK? Hakuna hata mmoja aliyepata, " alisema Mnyika.

Alisema hadi sasa serikali imeshindwa kumaliza mvutano uliojitokeza kwa kueleza bayana nani mmiliki hasa wa kiwanja liliko Soko la Kigogo Sambusa kati yake (serikali) na Kampuni ya Konoike, ambayo miezi michache baada ya serikali kuwahamishia wamachinga katika eneo hilo, iliibuka na kudai kuwa ni milki yake.

Alisema hali hiyo imesababisha baadhi ya wafanyabiashara kupata hasara kwa kuvunjiwa vibanda vyao kwa madai ya kuvamia eneo la Konoike na wengine kuendelea na biashara katika eneo hilo kwa hofu.

Hata hivyo, alisema licha ya serikali kuahidi kuifutia Konoike hatimilki ya kiwanja hicho ili kuwapa fursa wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa amani, ukuta wa kampuni hiyo unaendelea kujengwa, kitendo ambacho alisema kinaonyesha kuhalalishwa kwa kampuni hiyo kuwapo katika eneo hilo.

"Ni aibu kwa taifa. Wafanyabiashara waliovunjiwa Kariakoo wakaletwa hapa. Baada ya miezi michache, akajitokeza mmiliki Konoike, wakavunjiwa tena," alisema Mnyika na kuongeza:

"Serikali isipotoa taarifa ndani ya mwezi mmoja kuhusu mambo hayo, tutaeleza hatua tutakazochukua, kama za Kibunge au za nguvu ya umma. Sisi vijana wa Chadema tutaongoza mapambano hayo".

Akizungumzia ripoti hiyo, Mhonga, alisema uchunguzi ulifanywa na Kurugenzi ya Vijana ya Chadema kwa kuwahoji watu 500 na kupata taarifa mbalimbali na kwamba, ulifanyika katika kipindi cha miezi minne, kuanzia Aprili hadi Julai, mwaka jana katika masoko mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, ikiwa ni sampuli ya wafanyabiashara ndogondogo nchini.

Aliyataja masoko hayo kuwa ni, Makumbusho, Nyuki, Tegeta, Kawe, Mkwamani, Kinondoni, Chai Bora, Urafiki, Shekilango, Mwenge, Sinza, Posta Barabarani, Tegeta Barabarani, Tazara, Tandika, Temeke Mwisho, Kigogo Sambusa, Mbagala Sabasaba, Zakhiem, Rangi Tatu, Mtoni Mtongani, Mtoni Kwa Azizi Ally, Mwembe-Yanga, Kituo cha Polisi Chang'ombe na Yombo.
 
kuna kitu nilimuagiza Mnyika afanye ili asipotezewe muda wake na MBOWE nafikiri kaamua kwa njia moja ama nyingine kufuata ushauri na kaona bora kukimbilia kwa wamachinga !

ENDELEA KUFUATA USHAURI TOKA KWA KADAMPINZANI !
 
Safi sana

Wakati Lowassa anawahamisha wamachinga kwa bakora, wananchi walipolalamika msanii Kikwete akalihutubia taifa akasema wanawapeleka sehemu yenye anuani ili wakawape mikopo. Nani anakumbuka hayo maneno ya JK

Asha
 
Hapa ndipo Chadema wanathibitisha kuwajali wananchi wakati ambao sisiemu na viongozi wao wezi wakihamisha watanzania toka kwenye makazi yao na babu zao ili kuwapaatia wazungu na wakoloni wachukue madini na hazina zote za nchi kwa bei ya karanga.

Good job Mnyika, Job well done!
 
Na kubaliana na wewe kabisa dada Asha
huu usanii ni wa hali ya juu, na kama mnakumbuka, Kikwete aliahidi kujenga Machinga House kwenye wilaya hizo tatu hapo DSM, ambazo kwa maneno yake zitakuwa za kisasa na kuwa kila machinga atapata mahali pa kuuzia bidhaa zake
Usanii uliendelea pale ambapo wilaya ya Ilala, walionyesha mpaka kijiramani cha jengo la Machinga House
Je ziko wapi hizo Machinga house sasa hivi, kama nyie CCm sio wasanii wa kutupa kabisa!!!!!!!!!!

Unajua ccm wamesahau kuwa zama hizi kuna watu wanatunza kumbukumbu ya kila kinachofanyika Tanzania. Wao wanauza nchi na watanzania wenye uchungu na nchi hawatawaruhusu kuendelea kufanya hivi hata kidogo!

Hongera Mnyika kwa kuona hili!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom