Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 80
Hebu acha kujitembeza. Njoo hapa ujibu maswali yako na ya mwenyekiti wako, usijifiche miongoni mwa wamachinga
Chadema kutetea wamachinga
Na Muhibu Said
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeipa serikali mwezi mmoja kueleza hatua ilizokwishachukua kuhusu ahadi ilizozitoa kwa wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga, vinginevyo kitachukua hatua mbalimbali, ikiwamo kushawishi nguvu ya umma kutekeleza watakayoona yanafaa.
Ahadi hizo ni pamoja na kuwawezesha kwa kuwapatia mitaji ya biashara, mafunzo na ujuzi.
Kauli hiyo ya Chadema, ilitolewa na Mwenyekiti wa Vijana Taifa , John Mnyika, wakati wa uzinduzi wa ripoti ya uchunguzi wa mwenendo wa biashara ya wafanyabiashara ndogondogo katika Jiji la Dar es Salaam, uliofanyika katika Soko la Kigogo Sambusa jana.
Uzinduzi huo uliongozwa na Mbunge wa Viti Maalum wa chama hicho, Mhonga Ruhwanya, ambaye alikuwa mgeni rasmi.
"Serikali inapita inasema mabilioni ya JK, ukiuliza ni wamachinga wangapi wamepata hayo mabilioni ya JK? Hakuna hata mmoja aliyepata, " alisema Mnyika.
Alisema hadi sasa serikali imeshindwa kumaliza mvutano uliojitokeza kwa kueleza bayana nani mmiliki hasa wa kiwanja liliko Soko la Kigogo Sambusa kati yake (serikali) na Kampuni ya Konoike, ambayo miezi michache baada ya serikali kuwahamishia wamachinga katika eneo hilo, iliibuka na kudai kuwa ni milki yake.
Alisema hali hiyo imesababisha baadhi ya wafanyabiashara kupata hasara kwa kuvunjiwa vibanda vyao kwa madai ya kuvamia eneo la Konoike na wengine kuendelea na biashara katika eneo hilo kwa hofu.
Hata hivyo, alisema licha ya serikali kuahidi kuifutia Konoike hatimilki ya kiwanja hicho ili kuwapa fursa wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa amani, ukuta wa kampuni hiyo unaendelea kujengwa, kitendo ambacho alisema kinaonyesha kuhalalishwa kwa kampuni hiyo kuwapo katika eneo hilo.
"Ni aibu kwa taifa. Wafanyabiashara waliovunjiwa Kariakoo wakaletwa hapa. Baada ya miezi michache, akajitokeza mmiliki Konoike, wakavunjiwa tena," alisema Mnyika na kuongeza:
"Serikali isipotoa taarifa ndani ya mwezi mmoja kuhusu mambo hayo, tutaeleza hatua tutakazochukua, kama za Kibunge au za nguvu ya umma. Sisi vijana wa Chadema tutaongoza mapambano hayo".
Akizungumzia ripoti hiyo, Mhonga, alisema uchunguzi ulifanywa na Kurugenzi ya Vijana ya Chadema kwa kuwahoji watu 500 na kupata taarifa mbalimbali na kwamba, ulifanyika katika kipindi cha miezi minne, kuanzia Aprili hadi Julai, mwaka jana katika masoko mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, ikiwa ni sampuli ya wafanyabiashara ndogondogo nchini.
Aliyataja masoko hayo kuwa ni, Makumbusho, Nyuki, Tegeta, Kawe, Mkwamani, Kinondoni, Chai Bora, Urafiki, Shekilango, Mwenge, Sinza, Posta Barabarani, Tegeta Barabarani, Tazara, Tandika, Temeke Mwisho, Kigogo Sambusa, Mbagala Sabasaba, Zakhiem, Rangi Tatu, Mtoni Mtongani, Mtoni Kwa Azizi Ally, Mwembe-Yanga, Kituo cha Polisi Chang'ombe na Yombo.