Mnyama okwi apigwa pingu-rage yumo

Bwana Mapesa

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,551
1,777
[h=3]OKWI AJITIA KINANZI HADI 2014 SIMBA SC, RAGE NA HANS POPPE WAMALIZA KAZI KAMPALA USIKU WA JANA[/h]

Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage (kushoto) baada ya kutilia saini mkataba na Okwi hoteli ya Sheraton, Kampala

Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Simba SC ya Dar es Salaam, baada ya kusaini jana usiku katika hoteli ya Sheraton mjini hapa.
Okwi alisaini mbele ya Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage ambaye ameongozana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe.
Baada ya kusaini, Okwi alisema; “Nimefurahi kuongeza mkataba na klabu yangu na ninaahidi kuendelea kuitumikia kwa nguvu zangu zote,”alisema Okwi.
Kwa upande wake, Hans Poppe alisema kwamba anaamini kusaini na Okwi sasa kutawakata vilimilimi wapinzani wao, ambao walikuwa wanamuwania mchezaji huyo.
“Sisi tunajua yote yaliyokuwa yakiendelea kwenye Challenge, tunajua wapinzani wetu walimfuata Okwi huku, lakini huyu mchezaji ana mapenzi yeye mwenyewe na Simba SC,”alisema Hans Poppe.
Okwi aliyezaliwa Desemba 25, mwaka 1992 mjini hapa, alisajiliwa na Simba SC mwaka 2009 akitokea SC Villa ya hapa, baada ya klabu hiyo kumkosa mshambuliaji mwingine Mganda, Brian Umony aliyewahiwa na SuperSport United ya Afrika Kusini.
Tangu msimu uliopita, Okwi amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia Yanga au Azam na akiwa kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge iliyoanza Novemba 24 na inafikia tamati kesho, ziliibuka habari za klabu hizo kumfuata kumsainisha mjini hapa.
Okwi jana alifunga bao moja kati ya matatu ya Uganda kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini hapa, yaliyozima ndoto za Tanzania Bara kurejea nyumbani na Kombe la Challenge.
Kwa matokeo hayo, Uganda itamenyana na majirani zao na wapinzani wao wakubwa, Kenya katika fainali Jumamosi, ambao katika mchezo wa kwanza waliitoa kwa mikwaju ya penalti 4-2 Zanzibar, kufuatia sare ya jumla ya 2-2 ndani ya dakika 120.
Zanzibar na Bara zitamenyana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu siku hiyo hiyo ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Namboole.
Hadi mapumziko, Uganda walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na Emmanuel Okwi dakika ya 11, baada ta kuuwahi mpira mrefu uliopigwa na kipa wake, Hamza Muwonge na kufumua shuti kali la umbali wa mita 19, ambalo lilimshinda kipa Juma Kaseja.
Baada ya bao hilo, Okwi aliumia na kutoka nje dakika ya 36 nafasi yake ikichukuliwa na Hamisi Kiiza.
Uganda ndio waliouanza mchezo huo kwa kasi na kulitia misukosuko lango la Stars kwa takriban dakika 10 mfululizo, lakini baada ya hapo timu hizo zikaanza kushambuliana kwa zamu.
Timu zote zilikuwa zikishambulia kutokea pembeni, lakini Uganda ndio walioonekana kuzalisha mashambulizi ya hatari zaidi.
Kipa na Nahodha wa Stars, Juma Kaseja alitoka uwanjani baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza akilaumiana na mabeki wake kwa kufungwa bao la kutanguliwa.
Kipindi cha pili, Waganda walirudi na moto wao tena na kufanikiwa na kupata bao la pili dakika ya 51, safari hii Robert Ssentongo akimtungua Kaseja, baada ya mabeki wa Stars kudhani ameotea.
Pamoja na kufungwa bao la pili, Stars waliendelea kucheza kwa juhudi, ingawa Waganda waliendelea kutawala mchezo.
Mpira uliotemwa na Juma Kaseja kufuatia shuti la Moses Oloya, ulimkuta Ssentongo dakika ya 71 akaukwamisha nyavuni na kuipatia The Cranes bao la tatu. Kutoka hapo, hali ilikuwa mbaya kwa Stars.
Zikiwa zimesalia dakika tano mchezo kumalizika, taa za Uwanja wa Mandela zilizimika, lakini baada ya jitihada za pamoja za FUFA, CECAFA na uongozi wa Uwanja, ziliwaka baada ya dakika saba na mchezo kuendelea hadi filimbi ya mwisho.

Anasaini

Anasaini

Anaweka dole gumba

Kazi imekwisha, naona hasira ya Azam wameamua kuifanyia simba mtima nyongo kwa kumuuza Ngasa kinyume na mkataba wao wa mkopo wa mwaka mmoja.
 
Natafuta lile gazeti la kijani kijani kama matembele waliosema Kanjibai kamwaga mamilioni. Hahahahahahaha masikini Yanga Watakuwa wameanza kukonda tena!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Jamani msishau ya Twite! Rage alienda Kigali, akapigwa picha akiwa na Twite baada ya mkataba kusainiwa. Si mnakumbuka kilichotokea? Sinema isije ikarudiwa!
 
Nimeipenda sana picha hii baada ya kuona Dollar zipo hapo pembeni, hongera sana Okwi hawa wajinga ungewachekea ungecheza Simba kwa kukopwa tu. naomba na Wachezaji wengine ambao bado mko juu igeni msimamo wa Okwi.

20121206_235243.jpg
 
[h=2]Thursday, August 2, 2012[/h] [h=3]HIVI NDIVYO ADEN RAGE ALIVYOWAPIGA BAO YANGA NA KUMSAINI MBUYI TWITE[/h]
Wakati makamu mwenyekiti wa Simba Geodfrey Nyange Kaburu na mwenyekiti wa kamati ya usajili Zakaria Hans Pope wakiwa wanamalizana na kiungo mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa na mabingwa wa Tanzania bara, upande mwingine mwenyekiti wa klabu hiyo Mheshimiwa Aden Rage nae alisafiri umbali wa kilomita zipatazo 1,459.7, kutoka Dar kwenda Kigali kukamilisha usajili wa beki wa kati wa APR Mbuyi Twite.

Wakati Rage akiwa anamsainisha Twite ambaye pia alikuwa akiwindwa na mabingwa wa Africa mashariki na kati Yanga - upande mwingine Ngassa alikuwa anatia saini kuitumikia Simba kwa miaka 2.

Kwa maana hiyo Simba wakawa wameipiga bao wapinzani wao Yanga ambao wao pia walikuwa wakiwahitaji wachezaji hao wote wawili Twite na Ngassa.

Na haya ndio matambo ya Simba kupitia msemaji wao Ezekiel Kamwaga kuhusu kuwapiga bao wapinzani wao.

[h=6] Ezekiel Kamwaga
drP8vlvSl_8.gif
Ligi Kuu Tanzania
[/h] [h=6]Kigali, saa nne kasoro asubuhi ya leo....Mbuyi Twite anasaini mkataba wa kuitumikia Simba mbele ya Mhe; Ismail Aden Rage...Wakati akipata kahawa, jamaa mmoja anaitwa Bin Kleb akapiga simu, "Twite, siye Yanga tunakutaka sana tuambie tu tuje lini ili tumalizane....Akawekewa loud speaker; akaambiwa Mzee, hapa napata cappuccino nikiwa na Mwenyekiti wa Simba...Kleb akakata simu....2-0....1-0 ilikuwa Ngassa.......Jamani Simba ina watu kibao....Jamani Simba...Mi Casa Es Su Casa[/h] [h=6]By Aidan Charlie[/h]
 
Thursday, August 2, 2012

HIVI NDIVYO ADEN RAGE ALIVYOWAPIGA BAO YANGA NA KUMSAINI MBUYI TWITE

Wakati makamu mwenyekiti wa Simba Geodfrey Nyange Kaburu na mwenyekiti wa kamati ya usajili Zakaria Hans Pope wakiwa wanamalizana na kiungo mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa na mabingwa wa Tanzania bara, upande mwingine mwenyekiti wa klabu hiyo Mheshimiwa Aden Rage nae alisafiri umbali wa kilomita zipatazo 1,459.7, kutoka Dar kwenda Kigali kukamilisha usajili wa beki wa kati wa APR Mbuyi Twite.

Wakati Rage akiwa anamsainisha Twite ambaye pia alikuwa akiwindwa na mabingwa wa Africa mashariki na kati Yanga - upande mwingine Ngassa alikuwa anatia saini kuitumikia Simba kwa miaka 2.

Kwa maana hiyo Simba wakawa wameipiga bao wapinzani wao Yanga ambao wao pia walikuwa wakiwahitaji wachezaji hao wote wawili Twite na Ngassa.

Na haya ndio matambo ya Simba kupitia msemaji wao Ezekiel Kamwaga kuhusu kuwapiga bao wapinzani wao.

Ezekiel Kamwaga
drP8vlvSl_8.gif
Ligi Kuu Tanzania

Kigali, saa nne kasoro asubuhi ya leo....Mbuyi Twite anasaini mkataba wa kuitumikia Simba mbele ya Mhe; Ismail Aden Rage...Wakati akipata kahawa, jamaa mmoja anaitwa Bin Kleb akapiga simu, "Twite, siye Yanga tunakutaka sana tuambie tu tuje lini ili tumalizane....Akawekewa loud speaker; akaambiwa Mzee, hapa napata cappuccino nikiwa na Mwenyekiti wa Simba...Kleb akakata simu....2-0....1-0 ilikuwa Ngassa.......Jamani Simba ina watu kibao....Jamani Simba...Mi Casa Es Su Casa

By Aidan Charlie

Matola.... huu sasa ni uchokozi!!
 
Yangga kuna kitu kibaya mtakua mmekiachia huku kwa kukalia, thanx rage na captain hans poppe, kweli mnaweza na hongereni sana kwa hilo.
 
Hiiii,ina maana okwi ana miaka 20,kazaliwa 1992,duu,uongo wa mchana kabisa,kukomaa sura kote kule
 
Okwi ana future nzuri maana bado mdogo sana hapo muhimu ni kujituma ataweza enda mbele na kuendelea pata mapesa kama kawa
 
Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage (kushoto) baada ya kutilia saini mkataba na Okwi hoteli ya Sheraton, Kampala

Na Mahmoud Zubeiry, Kampala

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Simba SC ya Dar es Salaam, baada ya kusaini jana usiku katika hoteli ya Sheraton mjini hapa.

Okwi alisaini mbele ya Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage ambaye ameongozana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe.

Baada ya kusaini, Okwi alisema; "Nimefurahi kuongeza mkataba na klabu yangu na ninaahidi kuendelea kuitumikia kwa nguvu zangu zote,"alisema Okwi.

Kwa upande wake, Hans Poppe alisema kwamba anaamini kusaini na Okwi sasa kutawakata vilimilimi wapinzani wao, ambao walikuwa wanamuwania mchezaji huyo.

"Sisi tunajua yote yaliyokuwa yakiendelea kwenye Challenge, tunajua wapinzani wetu walimfuata Okwi huku, lakini huyu mchezaji ana mapenzi yeye mwenyewe na Simba SC,"alisema Hans Poppe.

Okwi aliyezaliwa Desemba 25, mwaka 1992 mjini hapa, alisajiliwa na Simba SC mwaka 2009 akitokea SC Villa ya hapa, baada ya klabu hiyo kumkosa mshambuliaji mwingine Mganda, Brian Umony aliyewahiwa na SuperSport United ya Afrika Kusini.

Tangu msimu uliopita, Okwi amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia Yanga au Azam na akiwa kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge iliyoanza Novemba 24 na inafikia tamati kesho, ziliibuka habari za klabu hizo kumfuata kumsainisha mjini hapa.

Okwi jana alifunga bao moja kati ya matatu ya Uganda kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini hapa, yaliyozima ndoto za Tanzania Bara kurejea nyumbani na Kombe la Challenge.

Kwa matokeo hayo, Uganda itamenyana na majirani zao na wapinzani wao wakubwa, Kenya katika fainali Jumamosi, ambao katika mchezo wa kwanza waliitoa kwa mikwaju ya penalti 4-2 Zanzibar, kufuatia sare ya jumla ya 2-2 ndani ya dakika 120.

Zanzibar na Bara zitamenyana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu siku hiyo hiyo ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Namboole.

Hadi mapumziko, Uganda walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na Emmanuel Okwi dakika ya 11, baada ta kuuwahi mpira mrefu uliopigwa na kipa wake, Hamza Muwonge na kufumua shuti kali la umbali wa mita 19, ambalo lilimshinda kipa Juma Kaseja.

Baada ya bao hilo, Okwi aliumia na kutoka nje dakika ya 36 nafasi yake ikichukuliwa na Hamisi Kiiza.

Uganda ndio waliouanza mchezo huo kwa kasi na kulitia misukosuko lango la Stars kwa takriban dakika 10 mfululizo, lakini baada ya hapo timu hizo zikaanza kushambuliana kwa zamu.

Timu zote zilikuwa zikishambulia kutokea pembeni, lakini Uganda ndio walioonekana kuzalisha mashambulizi ya hatari zaidi.

Kipa na Nahodha wa Stars, Juma Kaseja alitoka uwanjani baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza akilaumiana na mabeki wake kwa kufungwa bao la kutanguliwa.

Kipindi cha pili, Waganda walirudi na moto wao tena na kufanikiwa na kupata bao la pili dakika ya 51, safari hii Robert Ssentongo akimtungua Kaseja, baada ya mabeki wa Stars kudhani ameotea.

Pamoja na kufungwa bao la pili, Stars waliendelea kucheza kwa juhudi, ingawa Waganda waliendelea kutawala mchezo.

Mpira uliotemwa na Juma Kaseja kufuatia shuti la Moses Oloya, ulimkuta Ssentongo dakika ya 71 akaukwamisha nyavuni na kuipatia The Cranes bao la tatu. Kutoka hapo, hali ilikuwa mbaya kwa Stars.

Zikiwa zimesalia dakika tano mchezo kumalizika, taa za Uwanja wa Mandela zilizimika, lakini baada ya jitihada za pamoja za FUFA, CECAFA na uongozi wa Uwanja, ziliwaka baada ya dakika saba na mchezo kuendelea hadi filimbi ya mwisho.

Anasaini

Anasaini

Anaweka dole gumba
 
Anaonekana HANA RAHA; AMEKULA PESA za AZAM as well???

WOW PICHA ya CHINI ina BANDLE la $100.00 US
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom