Mnyalu na Mzungu

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
6,829
1,296
Mzungu mmoja alipita katika kijiji cha Igangidung'u na bahati mbaya alishikwa na haja kubwa alipokuwa akikatiza mashambani kwa wenyeji. Baada ya kuhakikisha kwamba hapakuwa na mtu jirani alijitoma kwenye shamba mojawapo ili ajisetiri. Baada ya kumaliza shughuli zake mzungua alijiandaa kuondoka na ndipo kwa bahti mbaya mwenye shamba (Mzee wa Kihehe) akatokea ; kumbe muda wote alikuwa ndani ya shamba akilikagua. Na yafuatayo ni majibizano yao.

Mzee: (kwa mshituko mkubwa) Heee heee
Mzungu: SORRY!

mzee: (kwa mshangao mkubwa kuliko mwanzo) HEEE HEEEEEE!
Mzungu: (akiwa kachanganyikiwa sasa;) AM VERY SORRY I was just'

Mzee: (akimkatisha mzungu) Wina uhulo veve (huna adabu kabisa!) Kunnya unnye veve!! Kusola ; nzole nene! (kunya unye wewe na kuzoa nizoe mimi; kwani wakati wote akiiitafsiri ile SORRY as SOOLE yaani zoa kwa kihehe)!

Asubuhi njema!
 
ahaaaa.... ni kama ile ya msukuma na mthungu pale alipotaka kujua umbali gani atatakiwa kuendesha ili kufika wanapokwenda, Msukuma kila akiulizwa kama wamefika anasema "TWENTE TU"...Mthungu anajua ni 22 Km akaendesha mpaka kupitiliza kituo...
 
Back
Top Bottom