Mnunuzi wa nyumba/ kiwanja usilazimishwe kulipa 10% Serikali za mitaa, haipo kisheria

Joseph lebai

JF-Expert Member
Jul 19, 2017
3,757
2,000
Pamoja na kuwa haipo kisheria , pesa inatumika kuimarisha miradi ya kitongoji na kukarabati ofisi . Ila kwa wengine ni dili kwani viongozi wa kitongoji wanatanua na hizo pesa . Nilihitaji maji nikaambiwa niende na barua kutoka serikali za mitaa , nikaambiwa mpaka nilipe ile asilimia 10 ili nipewe barua !! Ni haki ??
 

nosspass

JF-Expert Member
Mar 7, 2013
4,734
2,000
hii kitu iko kimtego sana....... anyway wale jamaa wa serikali za mitaa unaweza bargain nao....na isitoshe wanakuwa majirani......mimi hata ya dalali huwa sitoi......namzunguka shaaaa.....akitokea tunabargain kiaina......mjini shule...watu washapigwa sana......
 

MESHACK WARIOBA

JF-Expert Member
Mar 29, 2017
620
1,000
Titicomb,
Mkuu ni wazo Zuri sana, ila naomba tu nikwambie kuwa Asilimia Kubwa ya wanunuzi/wauzaji wa maeneo mbalimbali nchini mwetu mengi hayajapimwa, Lakini pia Kumekuwa na Shida nyingi sana, Unakuta Eneo limeuzwa mara mbili, na Mwenyekiti amesaini vilevile, maana Kwake hakuna Hasar kubwa, Kama ikitokea Mgogoro yeye atakuja kama Shahidi, si kama Mtuhumiwa;
 

MESHACK WARIOBA

JF-Expert Member
Mar 29, 2017
620
1,000
Erick Kalemela,
Hawana Umuhimu Saana kama wanavyopaishwa, Ukutaka kununu zingatia haya:

1. Mchukue Mtu wa Halmashauri, atakuchekia Eneo lako kama linafaa kwa matumizi yapi? Hata kama halijapimwa wao huwa wanajua, ili ikifika kipindi cha upimaji usionekane umejenga pasipo, Maana Wenyeviti wengi sana hawajui Master Plan ya maeneo wanayoishi, hivyo hata kama ni eneo ambalo la wazi anaweza asifahamu kama hapajapimwa, pakiwa pamepimwa ni rahisi, maana Halmashauri husika huwa wanatenga kabisa kwa maandishi/Alama etc.

2. Kwenye Mkataba hakikisha Unatafuta mwanasheria wakati wa Mauziano, kama unataka Kumweka Mwenyekiti muweke kama Shahidi, sio kama Mwenyekiti, hivyo hatahitaji kuweka Muhuri wake pale, Muhuri wa Mwanasheria utatosha.
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,102
2,000
Mkuu ni wazo Zuri sana, ila naomba tu nikwambie kuwa Asilimia Kubwa ya wanunuzi/wauzaji wa maeneo mbalimbali nchini mwetu mengi hayajapimwa, Lakini pia Kumekuwa na Shida nyingi sana, Unakuta Eneo limeuzwa mara mbili, na Mwenyekiti amesaini vilevile, maana Kwake hakuna Hasar kubwa, Kama ikitokea Mgogoro yeye atakuja kama Shahidi, si kama Mtuhumiwa;
Baba sio serikali hii.
Sasa wanaogopa kujihusisha na migogoro ya ardhi.
Siku hizi hata kukujazia na kutia saini fomu yako ya kibali cha ujenzi wakisikia kuna mgogoro hata wa mpaka tu hawakubali kuweka saini yao hata uwape kitu kidogo taslimu.
 

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,159
2,000
Mkuu mbona mimi nilikatiwa lisiti kabisa. Miaka ya Nyuma kabla ya mambo ya EFD hayajaja.
Asante kwa maarifa lkn binafsi yamenielea.
 

The indigenous

Senior Member
May 14, 2018
177
225
Nimenunua viwanja Mradi wa viwanja Mvomero na agizo juu la kulipa hiyo 10% tena kwa akaunti rasmi ya Halmashauri inayojulikana kama "DED Mvomero Miscellaneous"

Ninaposoma hii thread unajikuta niko confused maana hiyo 10% niliyolipa kwa Jan ni hatari
akaunti haithibitishi kama 10% ni sahihi,kinachothibitisha ni listi ya serikali ambayo unaweza kuwarahisi hata kushitaki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jan 1, 2019
17
45
Wiki ijayo nafanya biashara ya shamba. Hao serekali ya kijiji wakija nitawataka kwanza wanionyeshe sheria inayotaka wao wapate 10%, kisha nitawasisitiza hata kama hiyo sheria ipo waje na EFD receipt na sio hivyo vitabu vya kitapeli.
Na weye risiti ya EFD waainishe ni aina gani ya mauzo yamefanyika
 

The Alchemist

Senior Member
Jun 15, 2016
180
250
Whoever wrote this clearly hajui source ya income ya local governments inatokana na vyanzo vya ndani vya serikali husika.

Na hii huwekwa na bylaws za vijiji husika. Amd yes, haipo kwenye sheria za ardhi lakini ipo kwenye by laws.

IJUE SHERIA,
 

permanides

JF-Expert Member
May 18, 2013
3,847
2,000
IJUE SHERIA, Kuna kitu hukukiangalia vizuri, Sheria ulizotaja yaani Sheria ya Ardhi na Sheria ya usajili wa Ardhi hutumika katika maeneo ambayo ardhi imepimwa. Kuna maeneo ya vijijini ambayo hayajapimwa ni wazi Sheria hizi hazitumiki bali Sheria ya Ardhi ya Vijiji. Sambamba na hilo Sheria nyingi Ndogo zimefanya ardhi kuwa ni chanzo cha mapato, ndio maana mtu anapaswa kupewa risiti, risiti za EFD ni za wafanyabiashara hakuna sharti la malipo ya Serikali kupitia EFD.

Kinachotokea ni kuwa kuna wakati viongozi wa Serikali za Mitaa hawatoi risiti, hawatumii carbon copy au wanachomoa ile copy ili watafune pesa na wakaguzi wasijue. Hivyo ili kujua kama malipo hayo ni halali au hapana lazima uangalie Sheria za fedha /mapato ya eneo husika. Kwa mantiki hiyo Sheria ulizotaja hazina usaidizi wa kutosha wa kujibu hoja uliyoileta hapa.

Wasalaam

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom