Mnunuzi wa nyumba/ kiwanja usilazimishwe kulipa 10% Serikali za mitaa, haipo kisheria

I

IJUE SHERIA

Member
Dec 11, 2017
11
75

NA MWANASHERIA WETU

Mara nyingi nimekuwa nikiandika kuhusu masuala muhimu kuhusu ardhi hasa namna ya kuandika mikataba mtu anapokuwa ananunua nyumba/kiwanja, hadhi ya mikataba hiyo kisheria, na ubora wake.

Pia nimeandika mambo mbalmbali kuhusu namna ya kununua nyumba au kiwanja kwa usalama ili watu wasitapeliwe. Nikasema suala si tu kununua kile unachokipenda na kuondoka isipokuwa ni kununua na kuwa salama na ulichonunua bila hatari ya kukumbana na mgogoro mbeleni.

Lengo la haya yote ni katika kuhakikisha watu hawatapeliwi na hivyo kupoteza fedha walizochuma kwa jasho.Lengo lingine ni kuwaepusha wanunuzi na hatari ya kuingia mahakamani ambako kuna usumbufu mkubwa na panapoteza fedha na muda sana tena sana, naongea hili kwa uzoefu.

Leo pia nasisitiza tena kuwa ili ununue kiwanja au nyumba na uepuke kabisa kupata mgogoro hakikisha unafuata taratibu zote za msingi na za kisheria ikiwemo kuhakikisha unaandaa mkataba wenye hadhi ambao hata likitokea tatizo basi mkataba uwe ndio mlinzi wako.

Aidha leo naongelea tatizo lingine tena katika masuala hayahaya ya manunuzi ya viwanja na nyumba. Naongelea fedha ambayo serikali za mitaa wamekuwa wakiichukua kutoka kwa watu wanaouziana ardhi.

1 . SERIKALI ZA MITAA KUCHUKUA ASILIMIA KUMI WAKATI WA MANUNUZI YA KIWANJA/NYUMBA
Hatua hii ya serikali za mitaa kuchukua fedha kutoka kwa wanaouziana viwanja au nyumba limekuwa la kawaida sana.

Watu wanauziana kiwanja au nyumba serikali za mitaa wanawaambia kuwa mnatakiwa kulipa asilimia kumi kama ada ya mauziano .

Asilimia kumi ni hela nyingi sana kwakuwa kama nyumba imeuzwa milioni mianne asilimia kumi ni sawa na milioni arobaini.

Zipo serikali za mitaa nyingine ambazo wakati mwingine hudai chini ya hizo lakini mara kwa mara asilimia kumi ndio huwa inaombwa. Kinachouma zaidi hawa jamaa wa serikali za mitaa huwa wanalazimisha kutolewa kwa fedha hizo.

Hufikia hadi hatua ya kutoa vitisho na ikitokea kuwa mtu ameuza bila kuwa taarifu ili wachukue hela basi wanamjengea uadui na hata yule aliyenunua naye anajengewa uadui.

2 .ASILIMIA KUMI YA SERIKALI ZA MITAA HAIPO KISHERIA
Hakuna sheria yoyote katika nchi hii ambayo inatambua hiyo asilimia kumi. Hili ni jambo la kuzuka tu na limeanzishwa kwa matamanio(tamaa) ya watu.

Narudia tena hakuna katika sheria yoyote ya nchi hii inayosema kuwa watu wanapouziana kiwanja au nymba inatakiwa muuzaji au mnunuzi alipe asilimia kumi serikali za mitaa.Asilimia kumi ni mradi wa watu tu ambao wameamua kujipatia kipato kwa njia hiyo.

Natoa changamoto( challenge) ukimuona kiongozi yoyote wa serikali za mitaa kwa nia njema tu muulize asilimia kumi wanayotoza au gharama yoyote ile wanayotoza wakati wa mauzo ya viwanja na nyumba inapatikana katika sheria ipi.

Niseme tu kuwa Sura ya 113, sheria namba 4 ya ardhi pamoja na sura ya 334 sheria ya usajili wa ardhi zinachosisitiza ni kuwa mkataba wa ununuzi wa ardhi ni lazima uwe katika maandishi.

Sambamba na sheria hizo, kifungu cha 10 cha Sheria ya Mikataba kimesema mkataba unaokubalika kisheria ni ule uliofanywa kwa hiari huru,wahusika wenye sifa, malipo halali na mali halali.
Sheria hizi ndizo zinazosimamia mauzo ya ardhi.

Hakuna asilimia 10 humu pote. Pia humu pote hamna mahali kuwa usipolipa asilimia 10 ununuzi wako sio halali. Hakuna kabisa .

Kadhalika hakuna sheria nyingine yoyote nje ya nilizotaja hapa juu imeruhusu jambo hilo.

3 . JE IPI HADHI YA ASILIMIA KUMI?
Jibu ni rahisi kuwa asilimia kumi au malipo yoyote unayoyatoa serikali za mitaa wakati wa ununuzi wa nyumba/kiwanja ni rushwa. Ni rushwa na ni ufisadi.

Ifahamike wazi kuwa viongozi wa serikali za mitaa ni watumishi wa serikali. Fedha yoyote ambayo hulipwa serikalini ni lazima iwe imeainishwa katika sheria fulani.

Hakuna malipo yoyote kwa serikali ambayo hutolewa bila ya kuwa yameainishwa pahala fulani.

Pili fedha yoyote halali inayolipwa kihalali katika mamlaka yoyote ya serikali ni lazima itolewe risiti ya serikali. Inatolewa risiti ya serikali ikiwa na maana kuwa inatambuliwa na serikali , itakwenda serikalini na matumizi yake yatakaguliwa na serikali.

Fedha yoyote inayotolewa kwa serikali bila aliyetoa kupewa risiti ni fedha ambayo ina ufisadi ndani yake.

Na katika maana hiyo ni kuwa unapolipa fedha serikali za mitaa kwasababu yoyote ile kuhusu kufanyika kwa mkataba wa manunuzi ya kiwanja/nyumba unakuwa umetoa rushwa ndugu na kama utachukuliwa hatua utatakiwa kujibu mashtaka ya kutoa rushwa.

Kiongozi wa serikali za mitaa anayeomba na kupokea fedha hizo anakuwa ameomba na kupokea rushwa. Na ndio maana fedha hizi hazitolewi risiti.

Na ukipata bahati ukapewa risiti haitakuwa EFD bali zile za vitabu vyao vya kutengeza ambavyo kimsingi ni zuga tu.

4 . UWEPO WA SERIKALI ZA MITAA UNAPONUNUA ARDHI
Kisheria unaponunua kiwanja au nyumba pahala fulani suala la kuwashirikisha serikali za mitaa ni hiari yako.

Katu mkataba wa ununuzi haubatiliki kwakuwa hakukuwa na serikali za mitaa. Serikali za mitaa tunawahitaji kwa ajili ya kuainisha mipaka na kuepuka kuuziwa kiwanja mara mbili japo hizi dili nazo wamekuwa wakizicheza wao zaidi.

Kwahiyo wewe utaamua uwashirikishe au usiwashirikishe.

Narudia tena mkataba wa ununuzi wa ardhi kisheria haubatiliki ati kwasababu serikali za mitaa hawakushirishwa.

KWA MAPENDEKO YA MADA AMBAYO UNGEPENDA IJADILIWE 0784482959.
 
tindo

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
28,560
2,000
Wiki ijayo nafanya biashara ya shamba. Hao serekali ya kijiji wakija nitawataka kwanza wanionyeshe sheria inayotaka wao wapate 10%, kisha nitawasisitiza hata kama hiyo sheria ipo waje na EFD receipt na sio hivyo vitabu vya kitapeli.
 
lup

lup

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
2,291
2,000
Kuna zile sheria nasikia zinaitwa bylaw ambazo huwa zinatugwa na kijiji.. nahisi hizo ndio zinafanya mtu kulipa asilimia kumi.. au nimeelewa vibaya
 
serio

serio

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
6,840
2,000
Thread subscribed..
Watu wamepigwa sana
 
Cathode Rays

Cathode Rays

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
1,738
1,250
Nimenunua viwanja Mradi wa viwanja Mvomero na agizo juu la kulipa hiyo 10% tena kwa akaunti rasmi ya Halmashauri inayojulikana kama "DED Mvomero Miscellaneous"

Ninaposoma hii thread unajikuta niko confused maana hiyo 10% niliyolipa kwa Jan ni hatari
 
Ulipewa receipt ya EFD?
 
mgusi mukulu

mgusi mukulu

JF-Expert Member
Oct 24, 2013
719
1,000
Hivi mwanasheria akisimamia mauziano naye huwa ana asilimia yake pale.. na ipo kwa sheria gani na kwa efd gani anakupa...??? Tuanzie hapo mtoa mada .
 
casanova69

casanova69

JF-Expert Member
Sep 14, 2015
1,940
2,000
mi nadhani iyo asilimia kumi ni capital gain unayotakiwa kulipa kama kodi
 
shungurui

shungurui

JF-Expert Member
Sep 1, 2008
3,512
2,000
Sasa kama mishahara hamuwalipi mnafikiri watakula wapi, vinginevyo mtaishia kusumbuliwa tu kila nenda rudi.
 
M

Muntu

Member
Dec 22, 2011
32
95
Nimenunua Kiwanja, naomba kujua utaratibu wa kufanya transfers, Maana kuna jamaa angu amefanya transfers lakini jamaa anamzungusha kumpa risiti zake za hayo malipo.
 
wiseboy

wiseboy

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
2,952
2,000
Viwanja bongo kuuziana ni mtihani sna, pili serikali za mitaa ni miungu watu linapokuja hili swala la kupata ushuhuda wao kama serikali
 
likandambwasada

likandambwasada

JF-Expert Member
May 27, 2015
5,425
2,000
mgusi mukulu MWANASHERIA NI MTU BINAFSI, HUDUMA YAKE NI PRIVATE NA SYO HUDUMA YA SERIKALI HVYO KUMLIPA AU KUTOMLIPA NA KUMLIPA KIAS GAN HUTEGEMEA MAKUBALIANO YENU
 
Titicomb

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,091
2,000
Shida inakuja pale unapokuwa una mgogoro wa ardhi husika kama kuuziwa mara mbili au uliuziwa eneo la watu au eneo la wazi kwa ajili ya huduma za jamii.

Utakapohojiwa uliwashirikisha serikali za mtaa ili kupata uthibitisho wa uhalali wa umiliki wa ardhi wa aliekuuzia, hapo utatamani ukawaombe radhi siku zirudi nyuma uwahusishe kisha uwape 10% yao.

Ubishi mwingine ni kwa hasara yako tu. Unapogoma kuwalipa posho napo huwezi kuwalazimisha watoe nyaraka zao kama mashahidi.

Hawalipwi mshahara unategemea waishi vipi na muda wao wa kujitafutia riziki wanaupoteza kwa kazi yako.

Serikali za mitaa zinaweza kupitisha by laws za kutoza ushuru biashara fulani zinazofanyika maeneo yao kama vile ushuru wa masokoni, kutoza gharama za uzoaji taka taka au usafi wa mtaani au barabara za mtaa, n.k. kwa kadiri watakavyoona yafaa.

Ukigoma kutoa hizo tozo wanaweza kukuburuza mahakamani ingawa hakuna sheria ya nchi iliyotaja hiyo tozo explicitly ktk sheria za nchi.

NB: Mimi si mwanasheria lakini natumia common sense tu.
Remember "common sense is not common".
You will appriciate this common sense from a bush lawyer when the shit is starting to get out of control and you are about to lose your valuable piece of land because you didn't consult local government authorities when buying that land.

Don't lose your life savings for just a fvcking local government official's stipend of 10% of sale.

Use your common sense. Akili za kuambiwa changanya na zako.
 
Erick Kalemela

Erick Kalemela

JF-Expert Member
Nov 19, 2017
714
1,000
Mada ni nzuri ila Serikali za mitaa ni mhimu sana linapokuja suala la kumtambua mmiliki wa Ardhi ni mhimu sana kuwashirikisha ila mimi hua nawapa aslimia isiyozidi Tano
Vinginevyo wapigaji watawaliza wengi
Kama serikali ya mtaa hawatashirikishwa
 
M

Maasai 2676

Member
Jan 19, 2018
27
45
MNUNUZI WA NYUMBA/KIWANJA USILAZIMISHWE KULIPA ASILIMIA 10 SERIKALI ZA MITAA HAIPO KISHERIA.NA MWANASHERIA WETU.

Mara nyingi nimekuwa nikiandika kuhusu masuala muhimu kuhusu ardhi hasa namna ya kuandika mikataba mtu anapokuwa ananunua nyumba/kiwanja , hadhi ya mikataba hiyo kisheria, na ubora wake.

Pia nimeandika mambo mbalmbali kuhusu namna ya kununua nyumba au kiwanja kwa usalama ili watu wasitapeliwe. Nikasema suala si tu kununua kile unachokipenda na kuondoka isipokuwa ni kununua na kuwa salama na ulichonunua bila hatari ya kukumbana na mgogoro mbeleni.

Lengo la haya yote ni katika kuhakikisha watu hawatapeliwi na hivyo kupoteza fedha walizochuma kwa jasho.Lengo lingine ni kuwaepusha wanunuzi na hatari ya kuingia mahakamani ambako kuna usumbufu mkubwa na panapoteza fedha na muda sana tena sana, naongea hili kwa uzoefu.

Leo pia nasisitiza tena kuwa ili ununue kiwanja au nyumba na uepuke kabisa kupata mgogoro hakikisha unafuata taratibu zote za msingi na za kisheria ikiwemo kuhakikisha unaandaa mkataba wenye hadhi ambao hata likitokea tatizo basi mkataba uwe ndio mlinzi wako.

Aidha leo naongelea tatizo lingine tena katika masuala hayahaya ya manunuzi ya viwanja na nyumba. Naongelea fedha ambayo serikali za mitaa wamekuwa wakiichukua kutoka kwa watu wanaouziana ardhi.

1 . SERIKALI ZA MITAA KUCHUKUA ASILIMIA KUMI WAKATI WA MANUNUZI YA KIWANJA/NYUMBA

Hatua hii ya serikali za mitaa kuchukua fedha kutoka kwa wanaouziana viwanja au nyumba limekuwa la kawaida sana.

Watu wanauziana kiwanja au nyumba serikali za mitaa wanawaambia kuwa mnatakiwa kulipa asilimia kumi kama ada ya mauziano .

Asilimia kumi ni hela nyingi sana kwakuwa kama nyumba imeuzwa milioni mianne asilimia kumi ni sawa na milioni arobaini.

Zipo serikali za mitaa nyingine ambazo wakati mwingine hudai chini ya hizo lakini mara kwa mara asilimia kumi ndio huwa inaombwa. Kinachouma zaidi hawa jamaa wa serikali za mitaa huwa wanalazimisha kutolewa kwa fedha hizo.

Hufikia hadi hatua ya kutoa vitisho na ikitokea kuwa mtu ameuza bila kuwa taarifu ili wachukue hela basi wanamjengea uadui na hata yule aliyenunua naye anajengewa uadui.

2 .ASILIMIA KUMI YA SERIKALI ZA MITAA HAIPO KISHERIA.

Hakuna sheria yoyote katika nchi hii ambayo inatambua hiyo asilimia kumi. Hili ni jambo la kuzuka tu na limeanzishwa kwa matamanio(tamaa) ya watu.

Narudia tena hakuna katika sheria yoyote ya nchi hii inayosema kuwa watu wanapouziana kiwanja au nymba inatakiwa muuzaji au mnunuzi alipe asilimia kumi serikali za mitaa.Asilimia kumi ni mradi wa watu tu ambao wameamua kujipatia kipato kwa njia hiyo.

Natoa changamoto( challenge) ukimuona kiongozi yoyote wa serikali za mitaa kwa nia njema tu muulize asilimia kumi wanayotoza au gharama yoyote ile wanayotoza wakati wa mauzo ya viwanja na nyumba inapatikana katika sheria ipi.

Niseme tu kuwa Sura ya 113, sheria namba 4 ya ardhi pamoja na sura ya 334 sheria ya usajili wa ardhi zinachosisitiza ni kuwa mkataba wa ununuzi wa ardhi ni lazima uwe katika maandishi.

Sambamba na sheria hizo, kifungu cha 10 cha Sheria ya Mikataba kimesema mkataba unaokubalika kisheria ni ule uliofanywa kwa hiari huru,wahusika wenye sifa, malipo halali na mali halali.
Sheria hizi ndizo zinazosimamia mauzo ya ardhi.

Hakuna asilimia 10 humu pote. Pia humu pote hamna mahali kuwa usipolipa asilimia 10 ununuzi wako sio halali. Hakuna kabisa .

Kadhalika hakuna sheria nyingine yoyote nje ya nilizotaja hapa juu imeruhusu jambo hilo.

3 . JE IPI HADHI YA ASILIMIA KUM ?.

Jibu ni rahisi kuwa asilimia kumi au malipo yoyote unayoyatoa serikali za mitaa wakati wa ununuzi wa nyumba/kiwanja ni rushwa. Ni rushwa na ni ufisadi.

Ifahamike wazi kuwa viongozi wa serikali za mitaa ni watumishi wa serikali. Fedha yoyote ambayo hulipwa serikalini ni lazima iwe imeainishwa katika sheria fulani.

Hakuna malipo yoyote kwa serikali ambayo hutolewa bila ya kuwa yameainishwa pahala fulani.

Pili fedha yoyote halali inayolipwa kihalali katika mamlaka yoyote ya serikali ni lazima itolewe risiti ya serikali. Inatolewa risiti ya serikali ikiwa na maana kuwa inatambuliwa na serikali , itakwenda serikalini na matumizi yake yatakaguliwa na serikali.

Fedha yoyote inayotolewa kwa serikali bila aliyetoa kupewa risiti ni fedha ambayo ina ufisadi ndani yake.

Na katika maana hiyo ni kuwa unapolipa fedha serikali za mitaa kwasababu yoyote ile kuhusu kufanyika kwa mkataba wa manunuzi ya kiwanja/nyumba unakuwa umetoa rushwa ndugu na kama utachukuliwa hatua utatakiwa kujibu mashtaka ya kutoa rushwa.

Kiongozi wa serikali za mitaa anayeomba na kupokea fedha hizo anakuwa ameomba na kupokea rushwa. Na ndio maana fedha hizi hazitolewi risiti.

Na ukipata bahati ukapewa risiti haitakuwa EFD bali zile za vitabu vyao vya kutengeza ambavyo kimsingi ni zuga tu.

4 . UWEPO WA SERIKALI ZA MITAA UNAPONUNUA ARDHI.

Kisheria unaponunua kiwanja au nyumba pahala fulani suala la kuwashirikisha serikali za mitaa ni hiari yako.

Katu mkataba wa ununuzi haubatiliki kwakuwa hakukuwa na serikali za mitaa. Serikali za mitaa tunawahitaji kwa ajili ya kuainisha mipaka na kuepuka kuuziwa kiwanja mara mbili japo hizi dili nazo wamekuwa wakizicheza wao zaidi.

Kwahiyo wewe utaamua uwashirikishe au usiwashirikishe.

Narudia tena mkataba wa ununuzi wa ardhi kisheria haubatiliki ati kwasababu serikali za mitaa hawakushirishwa.

KWA MAPENDEKO YA MADA AMBAYO UNGEPENDA IJADILIWE 0784482959.
Duh! Kweli usilolijua ni kama usiku wa giza,kunbe hawa jamaa wa serikali za mitaa ni wezi namna hii,asilimia kumi ni pesa nyingi sana aki.manunuzi ya milioni kumi ni milioni,yani umefanyia watu kazi kwa ajili ya kalamu ya sh mia tena si wasomi...wakati wingine mwandishi ni wewe nunuzi au muuzaji.....viongozi wengi ni zero,hawajui kitu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom