Mnunuzi wa nyumba/kiwanja jihadhari Serikali za mitaa hawaruhusiwi kusimamia mikataba kisheria

moyafricatz

JF-Expert Member
Nov 27, 2015
2,900
4,864
Wiki iliyopita niliandika kuhusu Asilimia kumi ambayo serikali za mitaa huwa wanaidai hasa maeneo ya mijini baada ya wahusika kuwa wameuziana nyumba au kiwanja. Nikasema wazi kabisa bila kungata meno kuwa hiyo pesa iitwayo asilimia kumi au pesa nyingine yoyote mtu atakayolipa serikali za mitaa eti kwakuwa amenunua au ameuza eneo lake ni rushwa. Na leo nakumbusha na kusisitiza tena kuwa Watanzana wajue ukitoa pesa ile umetoa rushwa na huyo kiongozi wa serikali za mitaa uliyempa amepokea rushwa kwakuwa malipo hayo hayatambuliwi na hayaainishwi na sheria yoyote. Lazima ifike hatua haya mambo yaeleweke. Pia nimetahadharisha mara nyingi kuhusu umakini unaponunua kiwanja/nyumba na kueleza baadhi ya mambo ambayo ukiyafanya utakuwa umefanya manunuzi salama na utakuwa umeepuka migogoro na hata mgogoro ukitokea wewe hautapoteza.

Uhalali kisheria wa serikali za mitaa kusimamia mikataba.

( a ) KISHERIA HAIRUHUSIWI SERIKALI ZA MITAA KUSIMAMIA MAUZO YA NYUMBA/KIWANJA.

Kwanza nataka nieleweke wazi kuwa nazungumzia sana ununuzi wa nyumba /viwanja kwa kuona huruma jinsi watu wanavyopoteza umiliki wa maeneo yao waliyonunua kwa kuamini wameyanunua kihalali kumbe kuna nukta walizokosea katika taratibu za kimanunuzi na sasa zinawagharimu. Ninayosema hapo yanatokea karibia kila siku mahakamani. Watu wanalia lakini mda huo huna wa kumlilia.Nianze hivi kisheria Wakili ndio mtu ambaye anaruhusiwa kusimamia mkataba . Wakili ana vyeo vitatu, kwanza ni wakili, pili mthibitishaji wa umma ( notary public) tatu ni afisa wa viapo. Uwakili nao ni cheo katika vyeo alivyonavyo wakili. Vyeo viwili yaani uwakili na uthibitishaji wa umma ndivyo humpa mamlaka ya kusimamia mikataba. Hapa naongelea nyumba/viwanja lakini kimsingi vyeo hivi si tu humpa mamlaka ya kusimamia mikataba ya viwanja/nyumba lakini pia mikataba yote. Hakuna katka nchi hii sheria yoyote ambayo imemruhusu kiongozi wa serikali za mitaa kusimamia mkataba, uwe wa nyumba, mkopo au wowote ule hata wa mauzo ya baiskeli. Kama hakuna sheria hiyo maana yake ni kuwa kusimamia mikataba si kazi yao. Kwa maana hii hii narudia kusema na kusistiza kuwa hairuhusiwi serikali za mitaa kusimamia mauzo ya nyumba/kiwanja.

( b ) MKATABA WANGU WA MANUNUZI YA NYUMBA/KIWANJA UMESIMAMIWA NA SERIKALI ZA MITAA JE UNA HADHI GANI?.

Kama ndani kwako una mkataba wa manunuzi ya nyumba/kiwanja ambao ulisimamiwa na serikali za mitaa basi ujue kuwa mkataba huo hadhi yake ni sawa na umesimamiwa na jirani yako , ndugu yako au mtu mwingine yeyote unayemuamini ambaye amekusaidia kukamilisha mkataba. Tuache kuishi kwa mazoea hii ndiyo hali halisi kisheria. Mkataba wa mauzo ya nyumba/viwanja au mkataba mwingine wowote uliofanyika serikali za mitaa ni sawa na mkataba uliofanyika nyumbani kwako. Hiyo ndio hadhi au nafasi ya mkataba wa aina hiyo kisheria. Kiongozi yeyote wa serikali za mitaa anaweza kuwa shahidi yako ukiamua kumuita lakini lazima ujue kuwa ushahidi wake katika mkataba wako kisheria ni sawa na ushahidi wa mtu mwingine yeyote. Hakuna eti kwakuwa huyu au hawa ni serikali za mitaa kwahiyo wakionekana katika mkataba wangu ndio utakuwa na uzito na wenye kuaminika zaidi, hapana. Hawa kama utaamua kuwashirikisha maana hata kuwashirikisha nayo ni hiari yako wanaweza kuwa mashahidi sawa na shahidi ndugu yako au jamaa yako mwingine yeyote . Anayeufanya mkataba kuwa na uzito mbele ya macho ya sheria ni wakili na huyu ndiye aliyepewa kazi hii. Kwa hiyo wanunuzi wa viwanja/nyumba jihadharini kwakuwa serikali za mitaa kisheria hilo si jukumu lao. Wanayo majukumu yao lakini hili si miongoni mwa hayo. Watu wasifanyiwe utapeli serikali haisimamii mikataba ya watu binafsi. Kama serikali kuu haiwezi kusimamia mkataba kati Bakhresa na Mohammed enterprise hata serikali za mitaa hawezi kusimamia mkataba kati yangu na wewe. Nawatahadharisha zaidi wanunuzi kwakuwa upande wa ununuzi ndio upande wa kupoteza linapotokea tatizo.

( c ) USHAURI KWA WANUNUZI WA NYUMBA/VIWANJA.

Kama unataka kununua nyumba/kiwanja na unataka mkataba wako wa manunuzi uwe na nguvu na hadhi ya usimamizi wa kisheria basi epuka kuwatumia serikali za mitaa kufanya jambo hili. Serikali za mitaa wanajua vyema kuwa kusimamia mikataba ya kuuza na kunuua si katika majukumu yao isipokuwa kwakuwa hapa ndipo penye hela kuliko hata hizo posho zao wanazopewa na serikali kuu basi hawako tayari kulisema hili kwa mtu yeyote. Hili utakuja kulijua vyema ukishapata mgogoro wakati wao hawapo tena wameshaondoka na chao. Mikataba ya serikali za mitaa haina hadhi na wanasheria wanaichallenge sana mahakamani wakati wa migogoro kiasi cha kuonekana kama vile pengine hukufanya mkataba kabisa. Migogoro ya nyumba na viwanja ni mingi mno lakini wewe unaweza kuiepuka migogoro hiyo ikiwa utazingatia ushauri wa kitaalam na utaepuka kukurupuka unapotaka kununua kiwanja/nyumba. Leo nilitaka nikuhadharishe na hilo ndugu mpendwa.

MWANDISHI WA MAKALA HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA SERIKALI LA HABARI LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA JUMATANO.
 
Shukran kwa ushauri mkuu, nina swali "kama ushanunua kiwanja kwa kupitia hizo serikali za mitaa, je nawezaje kubadili hiyo hati ili iwe na uzito zaidi, kiwanja ni squatter, yaani hakijapimwa
 
Ooooh umenikumbusha sehemu nilinunua sasa muhusika niliye nunua kwake kafariki na tuliandikishana kwa mwenyekiti wa mtaa sasa mashamba serkali imeyachukua mkewe yupo hivi haki yangu imekaaje???
 
Ooooh umenikumbusha sehemu nilinunua sasa muhusika niliye nunua kwake kafariki na tuliandikishana kwa mwenyekiti wa mtaa sasa mashamba serkali imeyachukua mkewe yupo hivi haki yangu imekaaje???
Kamata mkewe tu..ndio halali yako iliyobakia
 
Inaitwa serikali ya mtaa halafu unasema haina mamlaka uko sawa kweli Mkuu? Ukitaka usajili wowote unaambiwa nenda kapate barua ya serikali ya mtaa na inatambulika ni halali halafu kwenye mauziano useme haitambuliki labda unatania

Hoja yako labda ungezungumzia hiyo asilimia 10 unayodai inalipwa kuwa siyo lakini kusimamia mauziano hilo hapana

Viwanja vingi huku tunauziana kupitia mamlaka hiyo na mambo yako safi kabisa na sasa hivi tunapimiwa kwa ajili ya urasimishaji makazi kwa mauziano yaliyothibitishwa na serikali ya mtaa sasa wakili unajitafutia wateja kwa maelezo hayo ya kuikataa serikali ya mtaa tafuta namna nyingine
 
Naona huyu mwandishi wa hii makala anasahau kitu kimoja. Lengo la kushirikisha serikali ya mtaa si kuipa uzito wa kisheria, kama alivyosema, mkataba inabidi ukawe certified na wakili ili upate uzito wa kisheria, ila serikali za mtaa zinashirikishwa ili kuepusha watu kuuziwa na wauzaji wasiohusika (matapeli), ni rahisi kwa ofisa wa serikali kukueleza kwamba shamba hili ni la nani na anakaa wapi na utampata vipi; lakini wakili yeye anakaa mjini, atakuja kishuhudia mauziano baina yako na matapeli na ata certify bila shida yoyote, unapata uzito wa kisheria ndio lakini umeuziwa na watu wasio wamiliki, sasa ni umetapeliwa tu maana hata ukiwatafuta hao walikuuzia wanakua wameshahama hadi mkoa. Serikali za mtaa hazishirikishwi tu for no reason.
 
Inaitwa serikali ya mtaa halafu unasema haina mamlaka uko sawa kweli Mkuu? Ukitaka usajili wowote unaambiwa nenda kapate barua ya serikali ya mtaa na inatambulika ni halali halafu kwenye mauziano useme haitambuliki labda unatania

Hoja yako labda ungezungumzia hiyo asilimia 10 unayodai inalipwa kuwa siyo lakini kusimamia mauziano hilo hapana

Viwanja vingi huku tunauziana kupitia mamlaka hiyo na mambo yako safi kabisa na sasa hivi tunapimiwa kwa ajili ya urasimishaji makazi kwa mauziano yaliyothibitishwa na serikali ya mtaa sasa wakili unajitafutia wateja kwa maelezo hayo ya kuikataa serikali ya mtaa tafuta namna nyingine
Niliwahi kupoteza vitambulisho vyote na line zote (niliibiwa), nikaambiwa niende serikali ya mtaa ili waandike barua ya kunitambua kwamba mimi ni nani na nakaa wapi, kila nilipoipeleka hiyo barua waliitambua na kuikibali, nikapata laini zangu na vitambulisho vyangu, hivyo wana umuhimu wao.
 
Unaongea kama mwanasheria au kwa experience tu mkuu ???
 
The only thing kama nakumbuka vyema ni kwamba agreement ni lazima iwe in writing hilo la wakili is not even necessarily, the law of contract and the land law does not put the requirement of an advocate.

Kuhusu ardhi, kuna ardhi za aina tatu, reserved, village and survey land. Whereby the village land act inaiweka village land under the village council. Sasa nashindwa elewa hapa kwanini kwenye village land serikali za mitaa wasiwepo wakati land hiyo ipo chini ya authority yao. "Selling land is not like selling oranges"

Kama ingekuwa land ambayo imefanyiwasurvey then unaweza check kwa rigistrer kuona kama kuna incumbarance lakini kwa village land it is those serikali za mitaa
 
Niliwahi kupoteza vitambulisho vyote na line zote (niliibiwa), nikaambiwa niende serikali ya mtaa ili waandike barua ya kunitambua kwamba mimi ni nani na nakaa wapi, kila nilipoipeleka hiyo barua waliitambua na kuikibali, nikapata laini zangu na vitambulisho vyangu, hivyo wana umuhimu wao.
Umuhimu tena mkubwa, asante kwa kuwa shuhuda mkuu asilimia kubwa sana ya viwanja watu wameuziana kupitia serikali za mitaa mpk kupata hati za nyumba zao hawa mawakili naona wanatafuta mbinu tu za kupata deal ingawa ni kwa kupotosha
 
Nenda kanunue Nyumba au kiwanja bila ya kumshilikisha Mwenyekiti wa mtaa uone siku utakavyokuja kulia hawa jama ndio wanajua maeneo yao
Inatakiwa waboreshewe kama mnaona haipo sawa sio kuwatanyia majungu
 
The only thing kama nakumbuka vyema ni kwamba agreement ni lazima iwe in writing hilo la wakili is not even necessarily, the law of contract and the land law does not put the requirement of an advocate.

Kuhusu ardhi, kuna ardhi za aina tatu, reserved, village and survey land. Whereby the village land act inaiweka village land under the village council. Sasa nashindwa elewa hapa kwanini kwenye village land serikali za mitaa wasiwepo wakati land hiyo ipo chini ya authority yao. "Selling land is not like selling oranges"

Kama ingekuwa land ambayo imefanyiwasurvey then unaweza check kwa rigistrer kuona kama kuna incumbarance lakini kwa village land it is those serikali za mitaa
Na hata ardhi ambayo sio surveyed, baadae inaweza ikaja kuwa surveyed na ikarasimishwa bila shida
 
Sheria za INCHI zinasema ardhi yote iliyoko kijijini/mjini au kwenye mtaa ni mali ya kijiji/halmashauri/manispaa kwa niaba ya Serikali .
Pia kisheria ardhi yote ni mali ya umma chini ya Raisi wa Inchi na watu wengine wote ni wakodishaji tu.
Ni kweli malipo yanayofanywa kwa serikali za mitaa wakati watu wanauziana ardhi/nyumba ni batili kama hayana stakabadhi halali ya Serikali ( kwa sasa EFD RISITI) . Ni lazima ulipe kitu kidogo serikalini wakati wa mauziano na pia wakati mwasasheria anaadika mkataba wa mauziano lazima alipwe na TRA lazima walipwe na waweke stamp, vinginevyo mkataba huo pia si halali.
Haiwezekani kisheria ukaenda kijijini na kununua eneo kubwa au dogo bila ridhaa ya uongozi wa kijiji/mtaa.
Viongozi hawa hawasaini kama wanasheria ila wanaisini kama mashahidi na wenye mali kwa niaba ya serikali.
Ili makubaliano yao yawe ya kisheria na yaitwe mkataba ni lazima yaandikwe kwa lugha ya kisheria na Mwanasheria aliyesajiliwa ili wahusika wasaini tena.
 
The only thing kama nakumbuka vyema ni kwamba agreement ni lazima iwe in writing hilo la wakili is not even necessarily, the law of contract and the land law does not put the requirement of an advocate.
Point yako iko hapa. An advocate is not necessary, Any land transactions should be in writing! ..land law, 1999.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom