Mnunuzi wa Nyumba au Kiwanja jihadhari, Serikali za Mitaa hawaruhusiwi kusimamia mikataba kisheria

IJUE SHERIA

Member
Dec 11, 2017
11
146
MNUNUZI WA NYUMBA/KIWANJA JIHADHARI SERIKALI ZA MITAA HAWARUHUSIWI KUSIMAMIA MIKATABA KISHERIA

Na Mwanasheria Wetu

Wiki chache zilizopita niliandika kuhusu Asilimia kumi ambayo serikali za mitaa huwa wanaidai hasa maeneo ya mijini baada ya wahusika kuwa wameuziana nyumba au kiwanja. Nikasema wazi kabisa bila kung'ata meno kuwa hiyo pesa iitwayo asilimia kumi au pesa nyingine yoyote mtu atakayolipa serikali za mitaa eti kwakuwa amenunua au ameuza eneo lake na hakuna risiti yoyote ya EFD inayotolewa ni rushwa.

Na leo nakumbusha na kusisitiza tena kuwa Watanzana wajue ukitoa pesa ile umetoa rushwa na huyo kiongozi wa serikali za mitaa uliyempa amepokea rushwa kwakuwa malipo hayo hayatambuliwi na hayajaainishwi na sheria yoyote.

Lazima ifike hatua haya mambo yaeleweke. Pia nimetahadharisha mara nyingi kuhusu umakini unaponunua kiwanja/nyumba na kueleza baadhi ya mambo ambayo ukiyafanya utakuwa umefanya manunuzi salama na utakuwa umeepuka migogoro na hata mgogoro ukitokea wewe hautapoteza.

Anayetaka kusoma haya yaliyopita aandike neno MAKALA SHERIA kwenye google ataona makala hizo. Leo tena naeleza uhalali kisheria wa serikali za mitaa kusimamia mikataba.

(a) KISHERIA HAIRUHUSIWI SERIKALI ZA MITAA KUSIMAMIA MAUZO YA NYUMBA/KIWANJA.
Kwanza nataka nieleweke wazi kuwa nazungumzia sana ununuzi wa nyumba /viwanja kutokana na jinsi watu wanavyopoteza umiliki wa maeneo yao waliyonunua kwa kuamini wameyanunua kihalali kumbe kuna nukta walizokosea katika taratibu za kimanunuzi na sasa zinawagharimu.

Ninayosema hapo yanatokea karibia kila siku mahakamani. Watu wanalia lakini mda huo huna wa kumlilia.Nianze hivi kisheria

Wakili ndio mtu ambaye anaruhusiwa kusimamia mkataba . Wakili ana vyeo vitatu, kwanza ni wakili, pili mthibitishaji wa umma ( notary public) tatu ni afisa wa viapo. Uwakili nao ni cheo katika vyeo alivyonavyo wakili. Vyeo viwili yaani uwakili na uthibitishaji wa umma ndivyo humpa mamlaka ya kusimamia mikataba. Namaanisha mikataba yote japo hapa naongelea zaidi nyumba/viwanja.

Hakuna katka nchi hii sheria yoyote ambayo imemruhusu kiongozi wa serikali za mitaa kusimamia mkataba, uwe wa nyumba, mkopo au wowote ule hata wa mauzo ya baiskeli. Kama hakuna sheria hiyo maana yake ni kuwa kusimamia mikataba si kazi yao.

Kwa maana hii hii narudia kusema na kusistiza kuwa hairuhusiwi serikali za mitaa kusimamia mauzo ya nyumba/kiwanja.

(b) MKATABA WANGU WA MANUNUZI YA NYUMBA/KIWANJA UMESIMAMIWA NA SERIKALI ZA MITAA JE UNA HADHI GANI?
Kama ndani kwako una mkataba wa manunuzi ya nyumba/kiwanja ambao ulisimamiwa na serikali za mitaa basi ujue kuwa mkataba huo hadhi yake ni sawa na umesimamiwa na jirani yako , ndugu yako au mtu mwingine yeyote unayemuamini ambaye amekusaidia kukamilisha mkataba. Tuache kuishi kwa mazoea hii ndiyo hali halisi kisheria.

Mkataba wa mauzo ya nyumba/viwanja au mkataba mwingine wowote uliofanyika serikali za mitaa ni sawa na mkataba uliofanyika nyumbani kwako. Hiyo ndio hadhi au nafasi ya mkataba wa aina hiyo kisheria.

(c) SHAHIDI WAKO WAKATI WA UNUNUZI
Kumbuka kisheria Wakili anaposimamia mkataba pia anakuwa shahidi wako. Unaweza kuongeza shahidi mwingine ukitaka lakini Wakili kwa hadhi yake kisheria anatosha kabisa.

Pia kiongozi yeyote wa serikali za mitaa anaweza kuwa shahidi yako ukiamua kumuita lakini lazima ujue kuwa ushahidi wake katika mkataba wako kisheria ni sawa na ushahidi wa mtu mwingine yeyote. Hakuna eti kwakuwa huyu au hawa ni serikali za mitaa kwahiyo wakionekana katika mkataba wangu ndio utakuwa na uzito na wenye kuaminika zaidi, hapana.

Hawa kama utaamua kuwashirikisha maana hata kuwashirikisha nayo ni hiari yako wanaweza kuwa mashahidi sawa na shahidi ndugu yako au jamaa yako mwingine yeyote.

Anayeufanya mkataba kuwa na uzito mbele ya macho ya sheria ni wakili na huyu ndiye aliyepewa kazi hii. Kwa hiyo wanunuzi wa viwanja/nyumba jihadharini kwakuwa serikali za mitaa kisheria hilo si jukumu lao. Wanayo majukumu yao lakini hili si miongoni mwa hayo. Watu wasifanyiwe utapeli serikali haisimamii mikataba ya watu binafsi.

Kama serikali kuu haiwezi kusimamia mkataba kati Bakhresa na Mohammed enterprise hata serikali za mitaa haiwezi kusimamia mkataba kati yangu na wewe. Nawatahadharisha zaidi wanunuzi kwakuwa upande wa ununuzi ndio upande wa kupoteza linapotokea tatizo.

(d) HUWEZI KUFANYA TRANSFER UKIWA NA MKATABA WA SERIKALI ZA MTAA.
Mnajua ukinunua nyumba/kiwanja unatakiwa kubadili jina kwenda jina lako hasa kukiwa na hati. Katika hatua hii huwezi kupeleka mkataba wa serikali za mtaa ukakubaliwa. Waliowahi kufanya hivo wanajua.

Narudia tena hautaweza kufanya transfer kabisa kabisa ukiwa na mkataba wa serikali za mitaa. Hii inadhihirisha ni kwa kiasi gani jambo hilo halikubaliki. Nenda ardhi uulize utaambiwa.

(e) USHAURI KWA WANUNUZI WA NYUMBA/VIWANJA
Kama unataka kununua nyumba/kiwanja na unataka mkataba wako wa manunuzi uwe na nguvu na hadhi ya usimamizi wa kisheria basi epuka kuwatumia serikali za mitaa kufanya jambo hili.

Kazi ya serikali za mitaa katika hili yaweza kuwa kumtambulisha na kumtambua muuzaji kuwa wanamfaham na ni mmiliki wa eneo husika. Nyingine ni kueleza ikiwa wanatambua eneo hilo kuwa na mgogoro ama laah. Si kusimamia mkataba.

Yumkini serikali za mitaa hujua vyema kuwa kusimamia mikataba ya kuuza na kununua si katika majukumu yao isipokuwa kwakuwa hapa ndipo penye hela kuliko hata hizo posho zao wanazopewa na serikali kuu basi hawako tayari kulisema hili kwa mtu yeyote. Hili utakuja kulijua vyema ukishapata mgogoro wakati wao hawapo tena wameshaondoka na chao.

Mikataba ya serikali za mitaa haina hadhi na wanasheria wanaichallenge sana mahakamani wakati wa migogoro kiasi cha kuonekana kama vile pengine hukufanya mkataba kabisa.

Migogoro ya nyumba na viwanja ni mingi mno lakini wewe unaweza kuiepuka migogoro hiyo ikiwa utazingatia ushauri wa kitaalam na utaepuka kukurupuka unapotaka kununua kiwanja/nyumba.

Leo nilitaka nikuhadharishe na hilo ndugu mpendwa.

KWA MAONI/ KUPENDEKEZA MADA 0784482959.
 
Mwanasheria Hiyo pesa ukitoa 10℅ Sema anakua ametapeliwa siyo Rushwa nimesikitishwa na Uanasheria wako wa kushindwa kutofautisha kati ya neno Utapeli na Rushwa na Nina wasiwasi hujui maana ya neno Rushwa mtu akiuza Mali yake akatakiwa kutoa 10℅ ni wazi kuwa ametapeliwa.

All in all article ni rekebisha hapo nilipokwambia.
 
Mwanasheria Hiyo pesa ukitoa 10℅ Sema anakua ametapeliwa siyo Rushwa nimesikitishwa na Uanasheria wako wa kushindwa kutofautisha kati ya neno Utapeli na Rushwa na Nina wasiwasi hujui maana ya neno Rushwa mtu akiuza Mali yake akatakiwa kutoa 10℅ ni wazi kuwa ametapeliwa.

All in all article ni rekebisha hapo nilipokwambia
Ww ndio umechemka, kiongozi wa serekali zikiwepo serekali za mitaa anayetoza malipo yyte ambayo hayatambuliki kisheria kwa ajili ya kutoa huduma flani ni rushwa tafuta sheria ya rushwa kwenye defining sections utakutana na hayo mambo
 
Kila kona vurugu tu. Wananchi wana changanyana. Viongozi wana changanyana. Mwisho wa siku wana wachanganya walaji na kuanza kuwalaumu.

SIASA ni Adui wa haki na maendeleo.
 
Wakili wa nini kwenye manunuzi ayse, 90 ya Watanzania wamenunua viwanja au Nyumba kupitia hao viongozi wa mtaa.

Mawakili wengi hatuwajui, Lakini pia mpaka umutoe ofisi atataka hela zaidi ya thamani ya kiwanja, wakati m/kiti ukimpa elfu 20 anapokea, sasa Niambie ni Wakili gani atatoka ofisini kwenda mahari kwa sh elfu 20?

Mambo mengine tunanunua kwa imani au kwa kujitoa muhanga.

NB: Sina uhakika na % nilizo toa, msije nikasema nimetoa takwim fake, huo ni mtazamo tu wangu.
 
Nyongeza nyingine kuna watu wanakopeshana kwa riba na wanaandikishana kwa mwenyekiti. Hapo pia hakuna mkataba
 
Mwanasheria Hiyo pesa ukitoa 10℅ Sema anakua ametapeliwa siyo Rushwa nimesikitishwa na Uanasheria wako wa kushindwa kutofautisha kati ya neno Utapeli na Rushwa na Nina wasiwasi hujui maana ya neno Rushwa mtu akiuza Mali yake akatakiwa kutoa 10℅ ni wazi kuwa ametapeliwa.

All in all article ni rekebisha hapo nilipokwambia
Leo umechemka mkuu rudi form 2 kasome upya maana ya rushwa
 
Viongozi wa mitaa hawana mshahara hayo ndiyo Malipo Yao ya halali na siyo rushwa.
 
Mkuu nashukuru na Elimu yako uliyotoa. Mimi si Mwanasheria lakini nina imani maoni yangu hapa chini unaweza kuyatolea ufafanuzi

1. Kama ni kweli serikali za mitaa zimekuwa zikiwaibia wauzaji na Wanunuzi kupitia kufungisha mikataba 'hewa' pande hizo mbili, kwanini serikali hai-intervene kudhibiti hali hiyo kwani inajua kinachoendelea? Hii haitakuwa mara ya kwanza serikali ku-intervene kwenye mambo ya Wananchi hasa pale wanapoibiwa ama kupotoshwa. Mfano kwenye michezo ya upatu.

2. Katika maeneo mengine ninaona hii dhana ikikubalika na ikitumika. Dhana ya BEST PRACTICE. Kwanini sheria isiutambue huu mfumo ambao umezoeleka na unakidhi malengo na inaendana na mazingira ya nchi yetu kwani sio kila mtanzania mwenye access ya Mawakili?
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom