Mnisaidie elimu ya kuishi na watu maofisini, changamoto ni nyingi

Watalamu Naomba mnisaidie kunipa elimu ya jinsi ya kuishi na watu maofisini.

Changamoto kwenye maofisi ni nyingi, naombeni muongozo.
Kuwa mnafiki na upende upigaji/udokozi, kama hutaki kupiga wakipiga kausha na jichanganye hata kama hupendi maana unaweza zushiwa kuwa unawachoma in case of any scandal na wakawa Wana ku skip kwenye fursa kumbe hujui..

Na ukizushiwa unaweza kuja kuumizwa kumbe uko innocent na kamwe hutokuja mjua aliyekuzushia maana wote watakuwa wanakuona hivyo..

Kiufupi Watz wengi ni wezi,wapenda shortcut na wabinafsi.

Nazungumza from experience,fuata huu ushauri utakuja kunishukuru.
 
Fanya kazi yako kwa ufanisi wako pasi kuathiri afya wala utu wako. Usiwe mbea, yasiyokuhusu achana nayo.

Kumbuka Bosi sio rafiki yako. Anaweza kukubadilikia sekunde moja tu na kukuachisha kazi.

La mwisho na la muhimu zaidi epuka mahusiano ya mapenzi kazini.
 
Watalamu Naomba mnisaidie kunipa elimu ya jinsi ya kuishi na watu maofisini.

Changamoto kwenye maofisi ni nyingi, naombeni muongozo.

1. Epuka mahusiano ya kimapenzi kazini
2. Wafanyakazi wenzako siyo lazima wawe marafiki zako. Hukuenda kutafuta marafiki bali kufanya kazi. Ikitokea umepata marafiki kazini, jenga mipaka yako.

3. Wafanyakazi wenzio sio wanaukoo wako, usiwashirikishe mambo yako binafsi.

4. Heshimu kila mtu bila kujali umri, uchumi, cheo na madaraka

5. Toa ushirikiano kwa wenzio kazini

6. Usikubali kuingia kwenye makundi kazini

7. Usifanye umbea na kuwasemea wenzako kwa wakubwa

8. Hata kama unafahamu jambo zaidi ya wengine, usijivune na kujiona Wewe ni bora kuliko wengine.
 
Hapo kwenye wafanyakazi kuwa marafiki ndo pa muhimu...yaan wao kukuharibia ni dk moja

Kiufupi hakuna kujenga urafiki na mtu ofisini
 
Back
Top Bottom