Mnigeria akamatwa na dawa za kulevya JNIA

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,477
15,320
Mnigeria Bede Eke (45) amekamatwa jana katika Uwanja wa Ndege Dar na kilo tano za dawa za kulevya. Raia huyo wa Nigeria alikamatwa uwanjani hapo wakati akitaka kuondoka kwenda Lagos, Nigeria kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia. Dawa hizo zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu kwa uchunguzi na kujua dhamani yake.

Polisi wanamhoji mtuhumiwa huyo kujua alikozipata dawa hizo na pia kuwajua Watanzania wanaoshirikiana nae katika biashara ya dawa za kulevya. Kwa mujibu wa polisi, Nigeria huyo alikamatwa baada ya mashine ya kisasa kufungwa uwanjani hapo kuimarisha usalama.

Mnamo Januari mwaka huu Mnigeria mwingine alikamatwa na dawa za kulevya uwanjani hapo.
 
Hawa wauza madawa nao ni janga kubwa sana katika taifaletu nashauri wakidhibitika wa hukumiwe harakaharaka.
 
Back
Top Bottom