Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,401
- 31,364
Mkuu Pascal Mayalla
Rejea bandiko#214. Maelezo na majibu ni mepesi kuliko hoja zilivyo
Kuna manung'uniko kutoka kwa vijana wa leo, kizazi tofauti na kile kilichounda muungano
Kauli za viongozi ikiwemo ya Waziri mchengerwa zinapalilia ufa ndani ya muungano.
Karibuni kuna kauli inayowatambua Watu wa bara kama Wageni katika suala la ardhi znz
Malalamiko ya muungano ni ya pande zote yaliyopelekea rasimu ya Warioba kuliangalia kwa upana na wa kina. Hakuna kitu kinachoitwa kero za Wazanzibar bali matatizo ya muungano. Jibu la rasimu ya Warioba ni serikali 3, ya Tanganyika ikirejeshwa
Kuna sababu kwanini rasimu ilisema hivyo. Moja ya sababu ni kuchelea kwamba siku Watanganyika watakapoidai Tanganyika litakuwa tatizo.
Waziri Mchengerwa alisema ajira za Wazanzibar ni 21% na kwamba usaili ufanyike Zanzibar. Kauli yake ilikuwa ya 'ushabiki' badala ya uhalisia na imechangiza sana hasira kwa vijana
1. Waziri anaposema 21% ya ajira, je ni za mambo ya muungano tu au mambo yote?
Kuna wizara zisizo za muungano, ina maana ya 21% ya takribani ajira 300,000 za muungano!
Hii ina maana moja, muungano unaajiri Wznz wengi kuliko SMZ tena katika maeneo yasiyo ya muungano. Hapo ndipo vijana wanapohoji ni kwa mantiki gani?
Swali, hivi kuna sababu gani za Wazanzibar kuajiriwa katika maeneo yasiyo ya muungano?
Kwanini Waziri hakufafanua hilo?
Na kwanini Wznz wagombee nafasi zisizo katika mambo ya muugano na Watanganyika?
Kwanini Watanganyika wanyimwe kugombea nafasi ndani ya SMZ?
Ikiwa nafasi ni za muungano kwanini zitolewe kwa sifa ya ''uzanzibar' na si sifa za kitaaluma?
Mbona hatuna nafasi za Wakigoma au Waruvuma au Wamtwara? Kwanini asilimia 21 itolewe kwa sifa ya eneo?
2. Waziri kasema 21% lakini hakuzungumzia katika ajira hizo za muungano nani anawalipia 21% kutoka Zanzibar!
3. Waziri ''haki' ya 21%. Je wajibu wa kuchangia muungano upo wapi?
Je, nini mchango wa Znz katika muungano? Inajulikana Znz ilisimama kuchangia muungano miaka mingi iliyopita. Je, nani anayewalipa 21% ya Wznz walioajiriwa na muungano kwa sifa ya Uzanzibar tu!
4. Katika mikopo znz iliruhusiwa kukopa kama nchi.
Hivi ni kwanini bado znz inapewa mikopo inayotokana na muungano?
Je, ZNZ inawajibika kulipa kwa kiasi gani mikopo hiyo?
Haiwezekani kudai mikopo bila kujua nani analipa.
5. Kuna kauli ya Wabara kuwa wageni hasa katika ardhi ya Zanzibar
Je, Wazanzibar takribani nusu yao wanaoishi bara haki ya umiliki wa ardhi ipoje kwao?
Orodha ya hoja ni ndefu na hawa vijana wanaohoji wanasababu za msingi kabisa.
Znz ina watu 1.5M na nusu yao wanaishi bara .
Mchango wa Znz katika muungano hauonekani!
Lakini Znz inapata 'upendeleo' kuliko mkoa wowote mdogo sana wa Tanganyika.
Ni kwa mantiki hiyo ZNZ imejificha katika koti la muungano ! kwamba katika masilahi znz ni Tanzania. Katika kuwajibika znz haipo si kuchangia au kulipa madeni
Suluhu ni uwepo wa Tanganyika itakayosimamia mambo yake na taratibu zake bila kuibeba znz. Kwanini znz na si Ilala katika mchango wa nchi?
Kwa hali ilivyo hali ya muungano ni mbaya sana. Watanganyika wanaponung'unika wakiwa na zigo la muungano 100% kwa hali na mali, kuna tatizo kubwa.
Viongozi waelewe kizazi cha leo kinaangalia masilahi ya leo, wenye historia na usalama wameshaondoka.
Kauli za kupendeza wznz hazijengi badala yake zinachochoe hisia tunazoziona
Alinda JokaKuu jmushi1