Mnielimishe: Ni kitu gani haswa Nyerere alikitaka kwenye Muungano, maana nachoona tunapigwa wazi wazi

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,014
1638361542179.png

Naombeni wenye jicho la ziada mnitoe ujinga maana huu ujinga nilionao ndio unanifanya niwe napatwa na hasira kwa maono mafupi yanayonifanga nione Zanzibar inatunyonya

Kwa upeo wangu mfupi najionea mambo haya, Naombeni mnipe maarifa, huenda mtazamo wangu haupo sawa.

Mambo ya huku bara lazima yawe na mchanganyiko wa mtanganyika na mzanzibari kuanzia ajira, uongozi, jeshini, mahakama, n.k kwenye uongozi kukiwa na msaidizi wa bara basi mkuu inabidi awe wa Zanzibar, kwenye ajira nako katika kila ajira 100 basi 21 za wazanzibar, jeshini huko wapo wengi pia sana sana polisi na jwtz, ila sasa huko kwao mambo yao ni ya wao hawataki mchanganyiko, hapa Tanganyika tunanufaika kivipi????

Ukija kwenye ardhi, wazanzibari kibao wanamiliki mashamba makubwa na viwanja huku bara lakini mtanganyika harusiwi kufanya hivyo, Je tunanufaika kivipi??

Ukija kwenye Power, hakuna kabila wala kundi linalowafikia wala kuwasogelea wazanzibar, yani si mchaga wala msukuma wala kabila lolote unaloweza kulifikiria, hawa wenzetu wapo wachache lakini wamesambazwa si mchezo kwenye vyeo vizito. kuna mawaziri, wakuu wamikoa, wakuu wa wilaya, ma rpc, vyeo vikubwa jwtz, mabalozi wa nchi za nje, majaji wa mahakama, maprofesa vyuoni, waajiriwa kwenye mashirika yenye mishahara minono kama bandarini, Bot, Tanapa, Tra, Nssf, n.k hii ni kwasababu muungano unahitaji mchanganyiko wa pande mbili.

Mtanganyika hana nafasi kwenye serikali ya zanzibar kuanzia kwenye uongozi, ajira, mahakama, n.k Wana serikali yao kwajili yao kuanzia uraisi, makamu wa raisi, spika wa bunge, n.k hawa inabidi wawe wa zanzibar. pia wana taasisi zao kama Zff ambayo ni kama tff ya huku, Zrb ambayo ni kama Tra ya huku, Zssf ambayo ni kama Nssf ya huku, Jku ambayo ni kama jkt ya huku, yani taasisi zipo kibao kwakweli, hizo taasisi zinatoa ajira kwa wazanzibar tu, mtu wa Tanganyika huna sifa, lakini cha ajabu mzanzibar anaweza kupata ajira pande mbili za bara na huko kwao, vya bara ni vya wote ila vya zanzibar ni vya wao pekee, Patamu happ aisee 🤔🤔

Tukubali kwamba wazanzibar "WALITUZIDI AKILI" na wanafaidi mno muungano bila kujijua.

Kwa upeo wangu nimegundua Karume alimzidi akili Nyerere, Alipoona kwamba Nyerere anambembeleza sana kuwe na muungano, Karume akatumia nafasi hii kumbana Nyerere aipe Zanzibar upendeleo kama huu tunaouona ama sivyo hakuna muungano, Pia akaongezea kipengere kwamba endapo kukiwa na muungano basi Zanzibar iwe kwajili ya Zanzibar lakini Tanganyika ibanwe iwe kwajili ya wote, Kwa lugha nyepesi "changu ni changu ila chako tutagawana" matokeo yake leo Tanganyika tunashuhudia inapigwa nje ndani na wazanzibar, haya malalamiko kutoka Zanzibar kwamba wananyonywa yaliwekwa kimkakati ili iwe silaha kwa wazanzibar kuridhika na kujitapa kwamba wametuzidi akili, ingekuwa hivi muungano ungekufa mapema. lakini pia haya malalamiko yapo kimkakti kuizubaza Tanganyika idhani kwamba Zanzibar ni kama mkoa wake kumbe kiukweli wazanziba ndio wanaonufaika.
 
Tatizo nyie vijan hamuelewi, Nyerere aliona mbali sana for security reasons kwasababu hata leo hii zanzbar wakijitenga hawata survive coz watakua week kijeshi kitendo cha nyerere kuleta muungano ni kutaka ku access eneo kubwa la bahari ya hind
 
Tatizo nyie vijan hamuelewi...........nyerere aliona mbari sana for security reasons kwasababu hata leo hii zanzbar wakijitenga hawata survive coz watakua week kijeshi................kitendo cha nyerere kuleta muungano ni kutaka ku access eneo kubwa la bahari ya hind
Watakuwa weak kijeshi na huku wanajeshi na Sasa wana uwezo wa kununua Silaha bila muungano
 
Naombeni wenye jicho la ziada mnitoe ujinga maana huu ujinga nilionao ndio unanifanya niwe napatwa na hasira kwa maono mafupi yanayonifanga nione Zanzibar inatunyonya...
Hadi leo sijajua, kwamba wazanzibar wanamiliki ardhi ya bara kwa uhuru wote, ila sisi tukienda kule tunafanywa wawekezaji hakuna kumiliki kwa haki sawa kama wao wakija huku. wazanzibar wameajiriwa kwenye serikali huku bara lakini marufuku kuajiri mbara kule kwao. si ujinga huu?
 
Kuna mawazo yanaweza kuwa sawa leo lakini miaka ya mbele ukitafakari kwa kina unaona kabisa hayakuwa sawa Nyakati zinabadilika na fikra za binadamu zinabadilika pia Mtazamo wa leo unaweza kua bora lakini kesho ukawa tofauti kulingana na ukuwaji na upanukaji wa fikra za binadamu.

Mwalimu Nyerere na karume waliweza kuonekana mawazo yao yalikuwa bora kipindi kile lakini leo yanaonekana kuwa na kasoro kubwa kutokana na kukua kwa fikra na mtazamo wa wananchi wa leo.
 
kiukweli sioni umuhmu wa muungano,Kama nchi ni moja ,why wawe na ubalos nje .si tuwaache waendelee na maisha yao,wakiuzwa ughaibuni na watt wao ,Basi!!
Rejea history ya TipTip.
Himaya ya oman east africa,
Helgrod treat(spelling?)
 
hadi leo sijajua, kwamba wazanzibar wanamiliki ardhi ya bara kwa uhuru wote, ila sisi tukienda kule tunafanywa wawekezaji hakuna kumiliki kwa haki sawa kama wao wakija huku. wazanzibar wameajiriwa kwenye serikali huku bara lakini marufuku kuajiri mbara kule kwao. si ujinga huu?
Mbaya zaidi likitoka tangazo la ajira huku bara, basi waombaji wa huku bara watachujwa kwa vigezo kama ufaulu, experience, hadhi ya chuo, n.k. na kiukweli wahitimu wapo wengi sana na ushindani ni mkubwa sana.

Ila kwa upande wa wenzetu huko kwanza wapo wachache, kigezo kikubwa kinakua uraia ili ajira nao wapate ionekane kuwa zimetolewa kimuungano zaidi.
 
Pan africanism ilikuwa ktk process ya kuunganisha Afrika kuwa nchi moja. Sasa hayo hayakufanikiwa na hivyo hata huu muungano umekuwa batili siyo tija tena.
 
53 Reactions
Reply
Back
Top Bottom