Mnielimishe: Ni kitu gani haswa Nyerere alikitaka kwenye Muungano, maana nachoona tunapigwa wazi wazi

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,683
2,000
Mkuu Pascal Mayalla

Rejea bandiko#214. Maelezo na majibu ni mepesi kuliko hoja zilivyo
Kuna manung'uniko kutoka kwa vijana wa leo, kizazi tofauti na kile kilichounda muungano

Kauli za viongozi ikiwemo ya Waziri mchengerwa zinapalilia ufa ndani ya muungano.
Karibuni kuna kauli inayowatambua Watu wa bara kama Wageni katika suala la ardhi znz

Malalamiko ya muungano ni ya pande zote yaliyopelekea rasimu ya Warioba kuliangalia kwa upana na wa kina. Hakuna kitu kinachoitwa kero za Wazanzibar bali matatizo ya muungano. Jibu la rasimu ya Warioba ni serikali 3, ya Tanganyika ikirejeshwa

Kuna sababu kwanini rasimu ilisema hivyo. Moja ya sababu ni kuchelea kwamba siku Watanganyika watakapoidai Tanganyika litakuwa tatizo.

Waziri Mchengerwa alisema ajira za Wazanzibar ni 21% na kwamba usaili ufanyike Zanzibar. Kauli yake ilikuwa ya 'ushabiki' badala ya uhalisia na imechangiza sana hasira kwa vijana

1. Waziri anaposema 21% ya ajira, je ni za mambo ya muungano tu au mambo yote?
Kuna wizara zisizo za muungano, ina maana ya 21% ya takribani ajira 300,000 za muungano!

Hii ina maana moja, muungano unaajiri Wznz wengi kuliko SMZ tena katika maeneo yasiyo ya muungano. Hapo ndipo vijana wanapohoji ni kwa mantiki gani?

Swali, hivi kuna sababu gani za Wazanzibar kuajiriwa katika maeneo yasiyo ya muungano?
Kwanini Waziri hakufafanua hilo?

Na kwanini Wznz wagombee nafasi zisizo katika mambo ya muugano na Watanganyika?
Kwanini Watanganyika wanyimwe kugombea nafasi ndani ya SMZ?

Ikiwa nafasi ni za muungano kwanini zitolewe kwa sifa ya ''uzanzibar' na si sifa za kitaaluma?
Mbona hatuna nafasi za Wakigoma au Waruvuma au Wamtwara? Kwanini asilimia 21 itolewe kwa sifa ya eneo?

2. Waziri kasema 21% lakini hakuzungumzia katika ajira hizo za muungano nani anawalipia 21% kutoka Zanzibar!

3. Waziri ''haki' ya 21%. Je wajibu wa kuchangia muungano upo wapi?

Je, nini mchango wa Znz katika muungano? Inajulikana Znz ilisimama kuchangia muungano miaka mingi iliyopita. Je, nani anayewalipa 21% ya Wznz walioajiriwa na muungano kwa sifa ya Uzanzibar tu!

4. Katika mikopo znz iliruhusiwa kukopa kama nchi.
Hivi ni kwanini bado znz inapewa mikopo inayotokana na muungano?

Je, ZNZ inawajibika kulipa kwa kiasi gani mikopo hiyo?
Haiwezekani kudai mikopo bila kujua nani analipa.

5. Kuna kauli ya Wabara kuwa wageni hasa katika ardhi ya Zanzibar

Je, Wazanzibar takribani nusu yao wanaoishi bara haki ya umiliki wa ardhi ipoje kwao?

Orodha ya hoja ni ndefu na hawa vijana wanaohoji wanasababu za msingi kabisa.

Znz ina watu 1.5M na nusu yao wanaishi bara .
Mchango wa Znz katika muungano hauonekani!
Lakini Znz inapata 'upendeleo' kuliko mkoa wowote mdogo sana wa Tanganyika.

Ni kwa mantiki hiyo ZNZ imejificha katika koti la muungano ! kwamba katika masilahi znz ni Tanzania. Katika kuwajibika znz haipo si kuchangia au kulipa madeni

Suluhu ni uwepo wa Tanganyika itakayosimamia mambo yake na taratibu zake bila kuibeba znz. Kwanini znz na si Ilala katika mchango wa nchi?

Kwa hali ilivyo hali ya muungano ni mbaya sana. Watanganyika wanaponung'unika wakiwa na zigo la muungano 100% kwa hali na mali, kuna tatizo kubwa.

Viongozi waelewe kizazi cha leo kinaangalia masilahi ya leo, wenye historia na usalama wameshaondoka.

Kauli za kupendeza wznz hazijengi badala yake zinachochoe hisia tunazoziona

Alinda JokaKuu jmushi1
 
chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,870
2,000
Hio siku ikifika utakuwa ushakufa zamani sana, ni miaka 2000 ijayo, ila kama kweli upo serious unataka kuishuhudia basi anza ule ubaguzi wa kiafrika Kusini dhidi ya wapemba na waunguja , anza Harakati za kuwatimua.
mzee wewe utatangulia kufa kuliko mimi, mimi sifi leo wala kesho kwa JIna la Yesu Kristo wa Nazareth.
 
chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,870
2,000
Nyuma misaada ikitolewa kwa Tanzania, hawapati ,,,
hawapati kivipi wakati wapo hapahapa bongo au wanataka wale mara mbili. wanzanzibari rundo wapo hapa bara wanakula hiyo misaada pamoja nasisi na wanataka wale mara mbili, wale bara na wakale visiwani si uroho huo?
 
MpendaTz

JF-Expert Member
May 15, 2009
1,999
2,000
Umewahi kudadisi kabla Karume hajatangulia mbele za haki huo mwaka alikuwa na mawazo gani kuhusu Muungano? Nimesikia aliwahi kusema haya "Muungano ni kama koti likikubana unalivua"...
Naam, hata mimi niliwahi kuyasikia haya maneno ya koti likikubana.
 
Aug 28, 2020
51
150

Naombeni wenye jicho la ziada mnitoe ujinga maana huu ujinga nilionao ndio unanifanya niwe napatwa na hasira kwa maono mafupi yanayonifanga nione Zanzibar inatunyonya

Kwa upeo wangu mfupi najionea mambo haya, Naombeni mnipe maarifa, huenda mtazamo wangu haupo sawa.

Mambo ya huku bara lazima yawe na mchanganyiko wa mtanganyika na mzanzibari kuanzia ajira, uongozi, jeshini, mahakama, n.k kwenye uongozi kukiwa na msaidizi wa bara basi mkuu inabidi awe wa Zanzibar, kwenye ajira nako katika kila ajira 100 basi 21 za wazanzibar, jeshini huko wapo wengi pia sana sana polisi na jwtz, ila sasa huko kwao mambo yao ni ya wao hawataki mchanganyiko, hapa Tanganyika tunanufaika kivipi????

Ukija kwenye ardhi, wazanzibari kibao wanamiliki mashamba makubwa na viwanja huku bara lakini mtanganyika harusiwi kufanya hivyo, Je tunanufaika kivipi??

Ukija kwenye Power, hakuna kabila wala kundi linalowafikia wala kuwasogelea wazanzibar, yani si mchaga wala msukuma wala kabila lolote unaloweza kulifikiria, hawa wenzetu wapo wachache lakini wamesambazwa si mchezo kwenye vyeo vizito. kuna mawaziri, wakuu wamikoa, wakuu wa wilaya, ma rpc, vyeo vikubwa jwtz, mabalozi wa nchi za nje, majaji wa mahakama, maprofesa vyuoni, waajiriwa kwenye mashirika yenye mishahara minono kama bandarini, Bot, Tanapa, Tra, Nssf, n.k hii ni kwasababu muungano unahitaji mchanganyiko wa pande mbili.

Mtanganyika hana nafasi kwenye serikali ya zanzibar kuanzia kwenye uongozi, ajira, mahakama, n.k Wana serikali yao kwajili yao kuanzia uraisi, makamu wa raisi, spika wa bunge, n.k hawa inabidi wawe wa zanzibar. pia wana taasisi zao kama Zff ambayo ni kama tff ya huku, Zrb ambayo ni kama Tra ya huku, Zssf ambayo ni kama Nssf ya huku, Jku ambayo ni kama jkt ya huku, yani taasisi zipo kibao kwakweli, hizo taasisi zinatoa ajira kwa wazanzibar tu, mtu wa Tanganyika huna sifa, lakini cha ajabu mzanzibar anaweza kupata ajira pande mbili za bara na huko kwao, vya bara ni vya wote ila vya zanzibar ni vya wao pekee, Patamu happ aisee

Tukubali kwamba wazanzibar "WALITUZIDI AKILI" na wanafaidi mno muungano bila kujijua.

Kwa upeo wangu nimegundua Karume alimzidi akili Nyerere, Alipoona kwamba Nyerere anambembeleza sana kuwe na muungano, Karume akatumia nafasi hii kumbana Nyerere aipe Zanzibar upendeleo kama huu tunaouona ama sivyo hakuna muungano, Pia akaongezea kipengere kwamba endapo kukiwa na muungano basi Zanzibar iwe kwajili ya Zanzibar lakini Tanganyika ibanwe iwe kwajili ya wote, Kwa lugha nyepesi "changu ni changu ila chako tutagawana" matokeo yake leo Tanganyika tunashuhudia inapigwa nje ndani na wazanzibar, haya malalamiko kutoka Zanzibar kwamba wananyonywa yaliwekwa kimkakati ili iwe silaha kwa wazanzibar kuridhika na kujitapa kwamba wametuzidi akili, ingekuwa hivi muungano ungekufa mapema. lakini pia haya malalamiko yapo kimkakti kuizubaza Tanganyika idhani kwamba Zanzibar ni kama mkoa wake kumbe kiukweli wazanziba ndio wanaonufaika.
Muungano wetu ulilazimishwa na Marekani na Uingereza, someni historia kwa kuchimba mtajua.
 
Bugsy

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
228
500
Nami nimefaidi .binafsi sijawahi kumsikia mzanzibar akijitambulisha kama mtanzania sijui hii imekaaje. Pili unadhani muungano ukifa mwarabu anaweza kurudi? Una habari huyo mwarabu alokimbilia uingereza kwamba bado anajipa hadhi ya kuwa mtawala wa Zanzibar ?

Mwisho juzi nimemsikiliza jusa anadai mwingereza alimsaidia kambarage kuitawala Zanzibar nawe unasema sultani angesaidiwa na mwingereza .tuelewe lipi Mzee Baba
Sultani alisaidiwa na Muingereza kwa sababu hii
Screenshot_20211207-151005_1.jpg

Inshort Tanganyika hawana benefit kwenye huu muungano, wanao benefit ni Zanzibari

Zanzibar ni mfano wa mke alie bembeleza kuolewa na Tanganyika kwa kigezo cha maslahi yake binafsi na sio upendo, mke wa aina hii inabidi apewe talaka.

Na kuhusu security reason ni kwa upande wa Zanzibar na sio bara hakuna issue ya terrorism, kwasababu Sultan Jamshid alikua tayari utawala wake alijiunga kwenye Commonwealth ya Muingereza na alikua recognized nchi huru, hivo mapinduzi yali kua Kama act of terrorism kwa waingereza, ndio maana mameli yakivita yalitumwa, Karume kuliona Hilo ilibidi amkimbilie Nyerere kudai muungano waonekane wapo pamoja na Commonwealth countries, kilicho mponza Nyerere misifa na sera ya ujamaa, alitaka kua mfano wa kuiunganisha Africa
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
24,078
2,000
Mkuu Pascal Mayalla

Rejea bandiko#214. Maelezo na majibu ni mepesi kuliko hoja zilivyo
Kuna manung'uniko kutoka kwa vijana wa leo, kizazi tofauti na kile kilichounda muungano

Kauli za viongozi ikiwemo ya Waziri mchengerwa zinapalilia ufa ndani ya muungano.
Karibuni kuna kauli inayowatambua Watu wa bara kama Wageni katika suala la ardhi znz

Malalamiko ya muungano ni ya pande zote yaliyopelekea rasimu ya Warioba kuliangalia kwa upana na wa kina. Hakuna kitu kinachoitwa kero za Wazanzibar bali matatizo ya muungano. Jibu la rasimu ya Warioba ni serikali 3, ya Tanganyika ikirejeshwa

Kuna sababu kwanini rasimu ilisema hivyo. Moja ya sababu ni kuchelea kwamba siku Watanganyika watakapoidai Tanganyika litakuwa tatizo.

Waziri Mchengerwa alisema ajira za Wazanzibar ni 21% na kwamba usaili ufanyike Zanzibar. Kauli yake ilikuwa ya 'ushabiki' badala ya uhalisia na imechangiza sana hasira kwa vijana

1. Waziri anaposema 21% ya ajira, je ni za mambo ya muungano tu au mambo yote?
Kuna wizara zisizo za muungano, ina maana ya 21% ya takribani ajira 300,000 za muungano!

Hii ina maana moja, muungano unaajiri Wznz wengi kuliko SMZ tena katika maeneo yasiyo ya muungano. Hapo ndipo vijana wanapohoji ni kwa mantiki gani?

Swali, hivi kuna sababu gani za Wazanzibar kuajiriwa katika maeneo yasiyo ya muungano?
Kwanini Waziri hakufafanua hilo?

Na kwanini Wznz wagombee nafasi zisizo katika mambo ya muugano na Watanganyika?
Kwanini Watanganyika wanyimwe kugombea nafasi ndani ya SMZ?

Ikiwa nafasi ni za muungano kwanini zitolewe kwa sifa ya ''uzanzibar' na si sifa za kitaaluma?
Mbona hatuna nafasi za Wakigoma au Waruvuma au Wamtwara? Kwanini asilimia 21 itolewe kwa sifa ya eneo?

2. Waziri kasema 21% lakini hakuzungumzia katika ajira hizo za muungano nani anawalipia 21% kutoka Zanzibar!

3. Waziri ''haki' ya 21%. Je wajibu wa kuchangia muungano upo wapi?

Je, nini mchango wa Znz katika muungano? Inajulikana Znz ilisimama kuchangia muungano miaka mingi iliyopita. Je, nani anayewalipa 21% ya Wznz walioajiriwa na muungano kwa sifa ya Uzanzibar tu!

4. Katika mikopo znz iliruhusiwa kukopa kama nchi.
Hivi ni kwanini bado znz inapewa mikopo inayotokana na muungano?

Je, ZNZ inawajibika kulipa kwa kiasi gani mikopo hiyo?
Haiwezekani kudai mikopo bila kujua nani analipa.

5. Kuna kauli ya Wabara kuwa wageni hasa katika ardhi ya Zanzibar

Je, Wazanzibar takribani nusu yao wanaoishi bara haki ya umiliki wa ardhi ipoje kwao?

Orodha ya hoja ni ndefu na hawa vijana wanaohoji wanasababu za msingi kabisa.

Znz ina watu 1.5M na nusu yao wanaishi bara .
Mchango wa Znz katika muungano hauonekani!
Lakini Znz inapata 'upendeleo' kuliko mkoa wowote mdogo sana wa Tanganyika.

Ni kwa mantiki hiyo ZNZ imejificha katika koti la muungano ! kwamba katika masilahi znz ni Tanzania. Katika kuwajibika znz haipo si kuchangia au kulipa madeni

Suluhu ni uwepo wa Tanganyika itakayosimamia mambo yake na taratibu zake bila kuibeba znz. Kwanini znz na si Ilala katika mchango wa nchi?

Kwa hali ilivyo hali ya muungano ni mbaya sana. Watanganyika wanaponung'unika wakiwa na zigo la muungano 100% kwa hali na mali, kuna tatizo kubwa.

Viongozi waelewe kizazi cha leo kinaangalia masilahi ya leo, wenye historia na usalama wameshaondoka.

Kauli za kupendeza wznz hazijengi badala yake zinachochoe hisia tunazoziona

Alinda JokaKuu jmushi1
Hoja zako ni nzito mno kiongozi. Kiukweli hazijibiki, zaidi ya kuuona uhitaji wa katiba mpya na uwepo wa serikali tatu Kama ambavyo tume ya Warioba ilipendekeza.

Karibu sana mkuu ulipotea mno. Umuhimu wa michango yako upo wazi kabisa.
 
Bugsy

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
228
500
Hoja zako ni nzito mno kiongozi. Kiukweli hazikibiki zaidi ya kuuona uhitaji wa katiba mpya na uwepo wa serikali tatu tume ya Warioba ilivyopendekeza.

Karibu sana mkuu ulipotea mno. Umuhimu wa michango yako upo wazi kabisa.
Kabisaa mkuu either kuwe na katiba mpya ya muungano wa serikali 3 au uvunjwe huu muungano, nyakati zimebadilika zamani sio sawa na sasa
 
Clemence Baraka

JF-Expert Member
Sep 4, 2012
1,692
2,000
Kwa wakati ule wake hofu kubwa ilikua Tanzania kuvamiwa kutokana na kuwa mstari wa mbele wa ukombozi wa nchi za Afrika. Muungano ulifanikisha JWTZ kuwepo Zanzibar.
 
rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
11,179
2,000
wakati wanaungana Karume alitaka tuwe nchi moja lakini Nyerere alikataa makusudi kwa kufikiri mbeleni wazanzibar baada ya kuona faida za muungano wangeomba wenyewe tuwe nchi moja.
Lakini tofauti ya maono ya Mwalimu Nyerere wazanzibar wameendelea kuwa wabinafsi, wao chakwenu cha wote chakwetu ni chetu. Kwa hali tuliyofikia sasa muungano ni mzigo mkubwa kwa Tanganyika ila unafiki wa ccm ndio unafanya muungano uendelee kuwepo kwani hata taratibu zilizowekwa kuhusu maswala ya muungano iwapo yanataka kuongezwa au kuondolewa yamekiukwa na badala yake watu wanajifungia na kuja kutueleza wametatua kero za muungano ambazo hazina jina.
Kero kubwa ya muungano ni usiri uliopo.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,683
2,000
Hoja zako ni nzito mno kiongozi. Kiukweli hazijibiki, zaidi ya kuuona uhitaji wa katiba mpya na uwepo wa serikali tatu Kama ambavyo tume ya Warioba ilipendekeza.
Mkuu, Waziri Mchengerwa alitoa maagizo nikajiuliza kama alifanya tahmini kabla ya kusema.
Amri anafasi 21% ziwe za Zanzibar na interview ifanyike huko hataki kusikia imefanyika bara!!

Waziri hakueleza 21% ya ajira zinahusisha Wizara gani. Ikiwa zinahusisha Wizara zisizo za muungano, hiyo ni kugombea nafasi za Tanganyika kwa kuzitoa Znz zifanyiwe iterview huko.
Je, hii ni haki kwa Tanganyika?

Kuna hesabu, 21% ya watu 1.5 inapatikanaje dhidi ya 79% ya watu milioni 50 wa Tanganyika?
Ndani ya ajira 21% Wznz wanaingia wizara zisizo za muungano, si 21% ni zaidi ya hapo
Ni kwanini na je ni haki kwa Watanganyika?

21% ajira gharama za mishahara zinatoka hazina Dar, kodi za Watanganyika.
Ikiwa Zanzibar wanachangia hazina , ni kiasi gani na kuanzia lini?

Waziri kushabikia 21% ya Wzn ni kuwasumanga Watangayika waliobeba gharama 21% kwa 100%

Hli ipo hivyo kwa Mikopo. Ikiwa Znz ilitaka na kuruhusiwa kukopa kama nchi, kwanini mikopo inayokuja Bara wanapewa?

Ikiwa wanapewa, ni kiasi gani wanachangia katika kurudisha hiyo mikopo?
Na ni kwanini wapitie Tanganyika wasiende kukopa wenyewe?
Kuna nini kinachowavuta kwenye mikopo ya muungano ikiwa walitaka kuwa huru kukopa?

Ile 4.5% ya BoT nayo inategemea uchumi wa Tanganyika. Uchumi ukipanda kama tulivyoambiwa nayo inapanda automatic. Swali lisilojibiwa, ni kiasi gani Zanzibar inachangia uchumi wa nchi?

Kauli ya Waziri ilikuwa kama kusema '' sasa ni wakati wetu' bila kuangalia madhara yake

'Reactions ' inayoonekana dhidi ya muungano ni kutokana na kauli kama za Waziri.
Nina wasi wasi hawa Watanganyika walioubeba muungano 100% wanahisia gani! sijui

Miaka ya 80 kulikuwa na kundi la G55 la akina Jenerali Ulimwengu na Njelu Kasaka.

Kundi hili lilitokana na kutoridhishwa na mambo kama ya Paasport kwenda znz na kipaumbele kwa Zanzibar na kuiacha Tanganyika. Rais alikuwa A.H.Mwinyi

Ilipotokea nafasi ya 'OIC' G55 likaingiza hoja ya Tanganyika likitaka Tanganyika irudi ili iamue masuala yake. G55 waliona kwa dhati muungano haukuwa na haki kwa Tanganyika.

Kurudi kwa Tanganyika na kuwa na serikali tatu ya muungano ikiwa na mambo 7 ni jibu sahihi ili kuondoa hizi figisu na kuulinda muungano. Rasimu ya Warioba irudi mezani.

Tukiendekeza 'viraka' na kujidanganya kwa kero za Wznz na kupuuza madai mazito ya Watanganyika ipo siku walioubeba muungano wataidai Tanganyika yao , sijui kama kutakuwa na muda wa maongezi. Nyerere aliweza kuzuia sioni anayeweza tena katika kizazi hiki.

Kizazi cha leo kinaangalia masilahi na si historia tena wala usalama. Kizazi kimeona kuna matundu mengi katika muungano kinadai Tanganyika ili kama znz iweze kuamua hatma yake.
Kuna hoja nzito sana za Watanganyika kuliko kero za wnz.
 
Sixmoth

Senior Member
Sep 11, 2021
122
225

Naombeni wenye jicho la ziada mnitoe ujinga maana huu ujinga nilionao ndio unanifanya niwe napatwa na hasira kwa maono mafupi yanayonifanga nione Zanzibar inatunyonya

Kwa upeo wangu mfupi najionea mambo haya, Naombeni mnipe maarifa, huenda mtazamo wangu haupo sawa.

Mambo ya huku bara lazima yawe na mchanganyiko wa mtanganyika na mzanzibari kuanzia ajira, uongozi, jeshini, mahakama, n.k kwenye uongozi kukiwa na msaidizi wa bara basi mkuu inabidi awe wa Zanzibar, kwenye ajira nako katika kila ajira 100 basi 21 za wazanzibar, jeshini huko wapo wengi pia sana sana polisi na jwtz, ila sasa huko kwao mambo yao ni ya wao hawataki mchanganyiko, hapa Tanganyika tunanufaika kivipi????

Ukija kwenye ardhi, wazanzibari kibao wanamiliki mashamba makubwa na viwanja huku bara lakini mtanganyika harusiwi kufanya hivyo, Je tunanufaika kivipi??

Ukija kwenye Power, hakuna kabila wala kundi linalowafikia wala kuwasogelea wazanzibar, yani si mchaga wala msukuma wala kabila lolote unaloweza kulifikiria, hawa wenzetu wapo wachache lakini wamesambazwa si mchezo kwenye vyeo vizito. kuna mawaziri, wakuu wamikoa, wakuu wa wilaya, ma rpc, vyeo vikubwa jwtz, mabalozi wa nchi za nje, majaji wa mahakama, maprofesa vyuoni, waajiriwa kwenye mashirika yenye mishahara minono kama bandarini, Bot, Tanapa, Tra, Nssf, n.k hii ni kwasababu muungano unahitaji mchanganyiko wa pande mbili.

Mtanganyika hana nafasi kwenye serikali ya zanzibar kuanzia kwenye uongozi, ajira, mahakama, n.k Wana serikali yao kwajili yao kuanzia uraisi, makamu wa raisi, spika wa bunge, n.k hawa inabidi wawe wa zanzibar. pia wana taasisi zao kama Zff ambayo ni kama tff ya huku, Zrb ambayo ni kama Tra ya huku, Zssf ambayo ni kama Nssf ya huku, Jku ambayo ni kama jkt ya huku, yani taasisi zipo kibao kwakweli, hizo taasisi zinatoa ajira kwa wazanzibar tu, mtu wa Tanganyika huna sifa, lakini cha ajabu mzanzibar anaweza kupata ajira pande mbili za bara na huko kwao, vya bara ni vya wote ila vya zanzibar ni vya wao pekee, Patamu happ aisee 🤔🤔

Tukubali kwamba wazanzibar "WALITUZIDI AKILI" na wanafaidi mno muungano bila kujijua.

Kwa upeo wangu nimegundua Karume alimzidi akili Nyerere, Alipoona kwamba Nyerere anambembeleza sana kuwe na muungano, Karume akatumia nafasi hii kumbana Nyerere aipe Zanzibar upendeleo kama huu tunaouona ama sivyo hakuna muungano, Pia akaongezea kipengere kwamba endapo kukiwa na muungano basi Zanzibar iwe kwajili ya Zanzibar lakini Tanganyika ibanwe iwe kwajili ya wote, Kwa lugha nyepesi "changu ni changu ila chako tutagawana" matokeo yake leo Tanganyika tunashuhudia inapigwa nje ndani na wazanzibar, haya malalamiko kutoka Zanzibar kwamba wananyonywa yaliwekwa kimkakati ili iwe silaha kwa wazanzibar kuridhika na kujitapa kwamba wametuzidi akili, ingekuwa hivi muungano ungekufa mapema. lakini pia haya malalamiko yapo kimkakti kuizubaza Tanganyika idhani kwamba Zanzibar ni kama mkoa wake kumbe kiukweli wazanziba ndio wanaonufaika.
Kikubwa sanaaaa nikuwa alitaka kuuwa Muslim na kuimarisha imani yake
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
12,922
2,000
Kwanza kabisa nimeona ramani na hutwo Tu dot tuwili nikacheka. Hivi ndo hutwo tunashare kweli kwamba tuliungana?

Pili ,sikujua kama ajira Wana apply kama Sisi nikajua zipo nsfasi maalum kama uhamiaji NK

Tatu , ukikutana na mzanzibar yeyoye ni mwendo kubweka kuwa hawautaki muungamo huko wakitunyonya.

Nne hivi hao vichwa vinavuoangalia Kero vya upande wetu havioni kuwa hiyo ni Kero ? Huku wanajitapa wanataka Zanzibar Kamili ? Huu ni uzwazwa
Mkuu 'Escrowseal1', umegusia habari ya "KERO ZA MUUNGANO".

Kwa ufahamu wangu najuwa kero zote hadi hii leo zinatoka upande mmoja wa muungano.

Kwa hiyo unaposema "hao vichwa vinavyoangalia kero upande wetu havioni kuwa hiyo ni kero", ujuwe kwamba hakuna vichwa vya upande wetu (bara). Hakuna kero hata moja iliyokwishawasilishwa kutoka upande wa bara.

Nadhani sasa ni wakati mwafaka kabisa kuanza kuwasilisha hizi kero zinazolalamikiwa mara kwa mara toka upande huu, ili nazo zianze kushughulikiwa na hivyo vichwa.
 
Bugsy

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
228
500
Mbona hatusikii wazanzibari kulalamika tena kero zao za muungano kama ilivyo kawaida yao, wamenyuti kimyaa safari hii , waje walalamike wapewe nchi huru kamili ijitegemee kama walivyokua wanadai zamani haki yao, sie wabara tutakua pamoja nao kwa hilo kuwasupport
 
silent lion

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
878
1,000

Naombeni wenye jicho la ziada mnitoe ujinga maana huu ujinga nilionao ndio unanifanya niwe napatwa na hasira kwa maono mafupi yanayonifanga nione Zanzibar inatunyonya

Kwa upeo wangu mfupi najionea mambo haya, Naombeni mnipe maarifa, huenda mtazamo wangu haupo sawa.

Mambo ya huku bara lazima yawe na mchanganyiko wa mtanganyika na mzanzibari kuanzia ajira, uongozi, jeshini, mahakama, n.k kwenye uongozi kukiwa na msaidizi wa bara basi mkuu inabidi awe wa Zanzibar, kwenye ajira nako katika kila ajira 100 basi 21 za wazanzibar, jeshini huko wapo wengi pia sana sana polisi na jwtz, ila sasa huko kwao mambo yao ni ya wao hawataki mchanganyiko, hapa Tanganyika tunanufaika kivipi????

Ukija kwenye ardhi, wazanzibari kibao wanamiliki mashamba makubwa na viwanja huku bara lakini mtanganyika harusiwi kufanya hivyo, Je tunanufaika kivipi??

Ukija kwenye Power, hakuna kabila wala kundi linalowafikia wala kuwasogelea wazanzibar, yani si mchaga wala msukuma wala kabila lolote unaloweza kulifikiria, hawa wenzetu wapo wachache lakini wamesambazwa si mchezo kwenye vyeo vizito. kuna mawaziri, wakuu wamikoa, wakuu wa wilaya, ma rpc, vyeo vikubwa jwtz, mabalozi wa nchi za nje, majaji wa mahakama, maprofesa vyuoni, waajiriwa kwenye mashirika yenye mishahara minono kama bandarini, Bot, Tanapa, Tra, Nssf, n.k hii ni kwasababu muungano unahitaji mchanganyiko wa pande mbili.

Mtanganyika hana nafasi kwenye serikali ya zanzibar kuanzia kwenye uongozi, ajira, mahakama, n.k Wana serikali yao kwajili yao kuanzia uraisi, makamu wa raisi, spika wa bunge, n.k hawa inabidi wawe wa zanzibar. pia wana taasisi zao kama Zff ambayo ni kama tff ya huku, Zrb ambayo ni kama Tra ya huku, Zssf ambayo ni kama Nssf ya huku, Jku ambayo ni kama jkt ya huku, yani taasisi zipo kibao kwakweli, hizo taasisi zinatoa ajira kwa wazanzibar tu, mtu wa Tanganyika huna sifa, lakini cha ajabu mzanzibar anaweza kupata ajira pande mbili za bara na huko kwao, vya bara ni vya wote ila vya zanzibar ni vya wao pekee, Patamu happ aisee 🤔🤔

Tukubali kwamba wazanzibar "WALITUZIDI AKILI" na wanafaidi mno muungano bila kujijua.

Kwa upeo wangu nimegundua Karume alimzidi akili Nyerere, Alipoona kwamba Nyerere anambembeleza sana kuwe na muungano, Karume akatumia nafasi hii kumbana Nyerere aipe Zanzibar upendeleo kama huu tunaouona ama sivyo hakuna muungano, Pia akaongezea kipengere kwamba endapo kukiwa na muungano basi Zanzibar iwe kwajili ya Zanzibar lakini Tanganyika ibanwe iwe kwajili ya wote, Kwa lugha nyepesi "changu ni changu ila chako tutagawana" matokeo yake leo Tanganyika tunashuhudia inapigwa nje ndani na wazanzibar, haya malalamiko kutoka Zanzibar kwamba wananyonywa yaliwekwa kimkakati ili iwe silaha kwa wazanzibar kuridhika na kujitapa kwamba wametuzidi akili, ingekuwa hivi muungano ungekufa mapema. lakini pia haya malalamiko yapo kimkakti kuizubaza Tanganyika idhani kwamba Zanzibar ni kama mkoa wake kumbe kiukweli wazanziba ndio wanaonufaika.
Nyerere hakua mjinga, Lengo kuu la Muungano kwa mujibu wa Lukuvi ni kuidhibiti Zanzibar na kuikakalia kimabavu, na hilo limefanikiwa , hayo mengine unayoyasema ni small sacrifice tu ili kuwazubaisha Wazanzibari.

Na mfumo huu wa Muungano ni kama mtego tu, Sera ya CCM inaeleza wazi kuwa Muundo wa Muungano ni serikali mbili kuelekea moja, na ni suala la muda tu kabla serekali ya Zanzibar haihafutwa.
 
Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
12,793
2,000
Tatizo nyie vijan hamuelewi, Nyerere aliona mbali sana for security reasons kwasababu hata leo hii zanzbar wakijitenga hawata survive coz watakua week kijeshi kitendo cha nyerere kuleta muungano ni kutaka ku access eneo kubwa la bahari ya hind
Week?
 
Muuza viatu

JF-Expert Member
May 14, 2020
3,288
2,000
hivo visiwa havina risk impact kubwa kuliko zenj.................. comoro , Madagascar havina muingiliano sana na waarabu........ kuliko zenji........
najua unajua uhusiano wa nchi za kiarabu na ugaidi
Asilimia kubwa ya wanaharakat na wanasiasa wa zanzibar wenye ushawish nyakat hizo walikua ni wasomi walioelimika kutoka nchi za kikomunist na misimamo yao ilikua ni muelekeo huo ukizingati kwa nyakat zile presha ilikua kubwa mno kati ya ukomunist na umagharib na ndio maana ukatumika muungano ili kuwapiga pini ref;kwa heri Uhuru kwa heri ukoloni by Ghassany km sijakosea
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom