Mnielimishe: Ni kitu gani haswa Nyerere alikitaka kwenye Muungano, maana nachoona tunapigwa wazi wazi

Nyerere alikuwa na lengo moja tu kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara wa Zanzibar waje kuwekeza Tanzania bara uwekezaji mkubwa serikali ipate Kodi kwani wazawa kipindi kile wakiwemo wachaga matongitongo ya kufanya biashara kubwa yakikuwa yamejaa hayajaamka .Wachaga walikuwa migombani tu kulima kahawa wamelala fofo kibiashara.Akaona heri alete wazanzibari waje huku kwa wingi bara apate Kodi ya kuendesha serikali na alifanikiwa Hadi leo wafanyabiashara wakubwa Wenye biashara kubwa na viwanda vikubwa bara Ni wazanzibari kuanzia akina Bakhresa nk wameshika sekta kubwa ziwe usafiri,mafuta,viwanda nk

Wachaga Ni wachuuzi yaani machinga waliochangamka kuliko machinga wa makabila mengine

Kwa kulipa Kodi TRA wazanzibari walioko bara wanaoongoza kuliko waswahili wote watanganyika

Nyerere aliangalia zaidi TRA kuukubali huu muungano mnaouona umekaa mguu kushoto ukiwa kulia na wa kulia ukiwa kushoto.

Ukiwaangalia kiingiacho TRA Hadi leo Huwezi mtu kubali muungano uvunjike kirahisi hivi ukiuvunja halafu Bakhresa arudi kwao Zanzibar Mswahili yupi mtanganyika aweza kuwa na mtaji na uwezo wa kuendesha business chain kubwa za Bakhresa kuhakikisha TRA inapata chake bila athari? Wata take over Nani Hawa malofa akina Lisu wapiga Domo ambao hata kufuga kuku tu wa biashara watano hawawezi kazi kubweka tu kuwa muungano mbaya? Mkono mtupu haulambwi

Nyerere alikubali muungano wa aina ilyopo akijua mkono aulambao una kitu.Mfano tukisema tulambe mkono wa Chadema wasiotaka muungano una Nini? Mbowe ana Nini,Lisu ana Nini,Msigwa ana Nini? Chadema wengi choka mbaya wamepigika kimaisha wanaishi kwa kuchonga midomo tu
Unaonekana muelewa ila siasa na chuki zako kwa wasiokua sawa kitazamo na ww inakufanya uongee vitu vya ovyo
 
Ni miungano ya mikataba iliyo wazi. Kila nchi imebaki nchi kamili na mamlaka yake yote na uhuru wake wote na nchi yoyote inaweza kujitoa wakati wowote kama ilivyofanya Uingereza.
Wewe unaye ielewa tujuze
 
Watanganyika tulipigwa, tunapigwa na tutaendelea kupigwa....

Hoja yako ni fikirishi sana... Sijui nani alitudanganya sisi Wadanganyika????????????????

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Huwezi kuleta muungano wa nchi mbili ili baadaye moja ya hizo nchi igeuke mkoa! ... NONSENSE!
Ubovu wa muungano ni kuwa na serikali mbili na sio tatu, na hili ni kosa la makusudi lililofanywa ili baadaye Zanzibar igeuzwe mkoa! ... ANOTHER PIECE OF NONSENSE!
PAMOJA NA UDOGO WAKE ZANZIBAR NI NCHI KAMA TANGANYIKA, RWANDA AU COMORO!
 
hapana mkuu..........nyerere alipiga hesabu kali sana muungao una faida kubwakiulinzi.........imagine zanzibar ni free ste alafu ikulu yetu ipo pemben mwa bahari
Nyerere mwenyewe hajawahi kutamka kwamba sababu ya Muungano ni ulinzi.

Alikufa anasema nia ilikuwa ni umajumui wa Afrika, kuelekea nchi moja ya Afrika, period.

Dhana ambayo imeshindikana, na Tanganyika tumebaki tunabeba mzigo mzito wa kuilea na kuitunza Zanzibar.

Muungano uvunjike, kila mtu aende la lwake, Tanganyika tupumue, please.
 
Hiyo 1964 kabla ya muungano mipaka ilikuwaje! Tuanzie hapo.
Wengine wanadai, mamlaka ya sultan, yalikuwa yanachukua hadi km 16 za ukanda wa pwani, toka somalia hadi Mozambique,
Wajerumani na waingereza walipokuja kutawala, waluongea na sultan na waka lease hilo eneo,
Wakati kenya inapata uhuru, waingereza walimuomba sultan akaridhia, kenya protectorate(mombasa) ziungwe na kenya colony ili iwe nchi moja ya kenya, sultan akaridhia,
Kuhusu ukanda wa pwani,Tanganyika,history haisemi popote baada ya wajerumani kulease kwa sultan,kulitokea nini,kwani mjerumani alishindwa vita vya pili akafurushwa toka Tanganyika, na pia baadae sultan wa zanzibar alipinduliwa,
Hivyo baada ya mapinduzi hali ya zanzibar ilikua dhoofu kiusalama na walihofia sultan anaweza kurudi,,
 
Aisee mi nimekusamehe na sina cha kuongeza.
Naelewa kulikua na ugaidi wa kina Ben Gurion, kipindi wanapigana na uingereza ili kujipatia uhuru huko israel,, au kipindi Lawlenci of arabia anawasaidia waarabu kujipatia uhuru toka kwa Uturuki , lakini term terrorists ilikua haijaanza kuwa applied kivile mpaka miaka ya 70 wakati wa harakati za BLACK SEPTEMBER
 
mali gani ya kugawana, ipo wapi? TRA wao wanayo ya kwao na sisi tunayo ya kwetu, kuna mambo kadhaa tu ya kimuungano ndio waangalia kama kuna pesa huko and after all hata wao walishafaidika nayo kwasababu wanaishi hapa. waache ujinga.
Nyuma misaada ikitolewa kwa Tanzania, hawapati ,,,
 
Siku mkitaka kuvunja muungano watataka mgawane mali pasu kwa pasu,hela za benki, Silaha, Nk.
Hivi wewe unategemea siku moja Hong Kong waachane tena na China?

Zanzibar hata siku moja haitaachana na Tanzania. Sasa hivi wanajazwa ujinga tu, itafika mahali wataambiwa hizo 'privileges' za upendeleo hakuna tena, na watakuwa hawana la kufanya.
 
Hivi wewe unategemea siku moja Hong Kong waachane tena na China?

Zanzibar hata siku moja haitaachana na Tanzania. Sasa hivi wanajazwa ujinga tu, itafika mahali wataambiwa hizo 'privileges' za upendeleo hakuna tena, na watakuwa hawana la kufanya.
Hong Kong na China wana historia ndefu. Historia ya Tanzania kama taifa ilianza 1964, ni nchi changa. Huwezi kulinganisha China na Tanzania. Kuachana kunawezekana sana kwenye nchi hizi changa, Sudan wameachana na Sudan Kusini. Kule Iraq unaona wale WaKurds wanataka nao kuachana na Iraq waendelee na Kurdistan, Syria vile vile. Tatizo ni kutambulika kimataifa, international legitimacy. Je Zanzibar kama nchi itakubalika kule UN?
 
Kuna mawazo yanaweza kuwa sawa leo lakini miaka ya mbele ukitafakari kwa kina unaona kabisa hayakuwa sawa Nyakati zinabadilika na fikra za binadamu zinabadilika pia Mtazamo wa leo unaweza kua bora lakini kesho ukawa tofauti kulingana na ukuwaji na upanukaji wa fikra za binadamu.

Mwalimu Nyerere na karume waliweza kuonekana mawazo yao yalikuwa bora kipindi kile lakini leo yanaonekana kuwa na kasoro kubwa kutokana na kukua kwa fikra na mtazamo wa wananchi wa leo.
Kama ndivyo hivyo mbona ccm wameukumbatia mfumo uleule,fikra na akili zilezile zenye athari kwa sasa?

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Sio lazima mtu wa bara ukajenge nyumba ya kuishi Zanzibar, zipo fursa nyingi sana hasa biashara za vyakura peleka mchele, maharage na vinginevyo hamna atayekuuliza , bara ardhi ilivyo kubwa na mapori matupu hata Wanzanzibar wakipewa viwanja wote bado mapori yatasalia mahekta na mahekta, Wanzanzibar tembeeni kidogo muone nchi yenu msijifungie Zanzibar pekee tembelea kisalawe, Chalinze Nenda Mtwara nunua kiwanja panda hata mikorosho piga mjengo wako enjoy maisha.
 
Dodo limewaangukia wazanzibari, kwa kweli kutesa kwa zamu, hakuna kipya maana tushazoea kila raisi aingiae madarakani hupeleka mboga kwao, shauri yenu wazenji msipo endelea muhula huu, nauhakika bila shaka mtaisoma namba chafu, kama mnabisha waulizeni Chatto , Genova ya Africa imeishia wapi, Mungu amewapenda kwa kweli

Ndio maana kuna haja ya kubadili katiba, wanaharakati wanavyopambana kuhusu hili swala mnawaona wapiga kelele na kuwatukana, hakuna kipya maana ukipanda mabua lazima uvune mabua usitegemee kuvuna zabibu, hii katiba ya mataga inabidi ibadirishwe bila hivyo zitabaki kelele za kila mtu kuvutia ngoma kwake
Mimi sielewi kwanini mzanzibar anaweza kuwa Rais wa huku kwetu na Mtu wa bara hawezi kuwa Rais wa Zanzibar. Nafikiri kwa kuwa Rais wa Muungano ndio Rais wa bara, na bara ndo Ina eneo kubwa na watu wengi zaidi, basi wazanzibar walitakiwa waishie kwenye umakamu wa Rais tuu, ikiwa hatutaki serikali tatu. Na ikiwa Mzanzibar anaweza kuwa Rais wa Muungano ambaye pia anakuwa Rais wa huku bara, inabidi kuwe na Rais wa huku bara kama ilivyo Zanzibar wana Rais wao. Kwangu mimi kumfanya Mzanzibar kuishia umakamu wa Rais tuu linawezekana, kama ilivyo Zanzibar kwenye serikali shirikishi, chama kinachoshika nafasi ya pili kinatoa Makamu wa kwanza wa Rais, na hata Rais wa Zanzibar akifa, Makamu wa kwanza hawezi kuwa Rais. Kama kwa Zanzibar wamefanya hivyo, same should be applied kwenye serikali ya Muungano, yaani wazanzibar ambao ni wachache watoe Makamu wa Rais tuu wa Muungano, na Rais awe anatoka bara kuliko na watu wengi na eneo kubwa la Nchi. Au njia bora zaidi ni kuwa na serikali tatu. Katiba ya sasa imepitwa na wakati, ni muhimu tuwe na katiba inayolinda maslahi ya wananchi wa pande zote.
 
Back
Top Bottom