Mnenguaji Rukia Bruno afariki dunia

Faith

Member
Jul 9, 2008
52
11
MNENGUAJI maarufu wa Bendi ya FM Academia, Rukia Bruno amefariki leo mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam .
Lukwangule imehabarishwa na mdau Emmanuel Mrema wa habariLeo kuwa taarifa ya kifo ameipata kupitia balozi Credo aliyejitambulisha kama kaka wa Mwanamuziki Nyoshi el Saadat ambaye mkewe amefariki.
Katika mazungumzo ya simu alisema shemeji yake alikuwa Muhimbili ambako alilazwa kabla ya kujifungua mtoto aliyefariki wiki moja iliyopita na kuzikwa hospitalini hapo.
“Habari za msiba za Bruno ni kweli na upo Sinza nyumbani kwa Nyoshi ambako familia ya marehemu ipo katika kikao cha kupanga siku ya maziko ya marehemu yatakayofanyika siku yoyote kuanzia sasa,” alisema Credo.
Aidha, Bruno alisema hafahamu chanzo umauti wa Rukia ambaye ameacha mume na mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Staloni.
Kabla ya kuwa bendi ya FM Academia mnenguaji huyo alikuwa katika bendi ya Twanga Pepeta, Bendi ya Tamutamu ambazo alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa kuwapa burudani mashabiki.

source:http://lukwangule.blogspot.com/

RIP RUKIA!
 
Back
Top Bottom