Mnaweza Kuwatawanya Viongozi CDM; ila Umma hadi 2016 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnaweza Kuwatawanya Viongozi CDM; ila Umma hadi 2016

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHOST RYDER, May 21, 2012.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mnaweza Kuwatawanya Viongozi CDM; ila Umma hadi 2016

  Chatu aliyebatizwa jina na migogoro anabisha hodi katika kibanda kinachozizima kwa hekaheka huko ndani nacho kibanda hicho kimebatizwa jina la CHADEMA huku jirani anapita kwa kando na mavazi ya kijani akiashiria CCM na kumwambia mtani wake, mgeni huyo anabisha hodi mfungulie!!!

  Afanaeleik huu mchezo wa kutumia rupia kuhakikisha unamomonyoa nguvu ya umma unaelekea kushika kasi ya gari moshi tena lile la makaa ya mawe, kudhihiri kama ni moto umeshakolea bila kujua wanakokwenda kumbe reli ilishakatika siku nyiiingi Maskini ya Mungu na kwamba mwisho wao watakumbwa tu na umauti.

  Nasukumwa kuamini upepo wa kisiasa ambao binafsi nimepata fursa ya kuwepo katika tathmini ya mapokeo ya wananchi juu ya majaaliwa yao kisiasa kwa sasa na baadae unachagizwa na karibu asilimia 80 ambayo ni UMMA unaohitaji a mabadiliko dhidi ya DOLA bila kujalisha anatoka itikadi ipi ya kisiasa.

  Hakuna chembe ya shaka juu ya kauli mbiu ya CDM ya ‘’NGUVU YA UMMA’’ kuwa inajibu moja kwa moja hitajio la wananchi hawa katika hamasa yao kubwa ya sasa ya UMMA dhidi ya UTAWALA ama DOLA ukipenda, na wao hili wanaliona kama hadithi ya jogoo na kiza ima akatae kuwika ama awike kutakucha tu kwa kuwa ndio ada ya uumbaji wa Mola.

  Bado mengi sana yatazungumzwa na bado mengi sana yataandikwa na kurushwa katika televisheni, Radio na vyombo vingine vya habari zikiwemo mitandao jamii, lakini kamwe hayatabadili mioyo ya Watanzania waliokinahi zaidi ya miongo mitano ya ukali wa maisha,elimu duni, huduma za afya zisizokidhi viwango na miundo mbinu iliyojikatia tamaa kwa hakika.

  Linapokuja suala la mgeni anayebisha hodi ndani ya CDM, hakika mgeni huyu kafika wala sitii neon katika hili kwa kuwa mgeni mwenyewe kakusudiwa kufanya safari hiyo ambayo sitashangaa kwani mapokezi yake pia yatakuwa si kama alivyotarajia.

  Mgeni ukimtazama kwa yakini anategemea atapata kuku na mapochopocho mengine mengi kumfanya aendelee kufurahia kuwepo na kujitanua kwa njozi za Alinacha zisizokauka ila hapa kwa mipango ya familia atakunywa shubiri ambayo kama ataamua kukaa ni hiari yake.

  Shubiri nayoizungumzia hapa si ya ndungu yangu Profesa Ndumba Nangai, bali ni umma uliokwishajaa hamasa na uliotambua maana ya mabadiliko kamwe hautoyumba kwa dhihaka hizi za viongozi waliolewa madaraka na wanaokusudia kuifanya nchi hii mali yao binafsi.

  Rupia imetumika Mwanza kuwahadaa wapiganaji wasiokuwa makini, lakini Umma umewaambia kwa hili hatuko pamoja nanyi, na si hilo tu mifano mingine unaweza kuiongoza katika kubaini hujuma hizi.

  Namaliza waraka huu kwa kusema ni kupoteza muda kuweweseka na CDM kwa sasa ati kwamba itakufa ndani ya mwaka ujao?!, inawezekana kweli mkaiua na hasa wala si kuiu bali kuwatawanya viongozi na hasa wale mapandikizi lakini Umma huu hamasa yao itapoa baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2015, na hiyo itakuwa 2016 hebu elekezeni macho huko ndo mtajua kuwa kumbe mnapigana na kivuli chenu wenyewe.

  Kwa mtaji huo CDM kinabaki kuwa tumaini jipya kama kilivyo na baada ya kuwa mmeusambaratisha uongozi kupitia mapandikizi, nguvu mpya itasimikwa na umma kuwaongoza katika mabadiliko, kama ni mchezo wa karata utakuwa umesaliwa na majike yote huku mpinzani wako na madumu yote hayumkini utamchenga walau jike moja ila matatu yote atayaooa mzee wangu Wassira.  ADIOS
   
Loading...