thetallest
JF-Expert Member
- Oct 21, 2017
- 8,256
- 9,085
Wakati inasimuliwa historia ya maisha ya Mzee Ali Hassan Mwinyi kwenye maisha yake ya uongozi na Professor Mukandala kipengele hiki alikizungumzia, ni kinani hao tuwafahamu kwa mlio na kumbukumbu mpaka ilipelekea Mzee Mwinyi atengeneze nafasi ya naibu waziri mkuu na nafasi hizo na ile ya wizara ya ulinzi kukabidhiwa Dkt. Salim?
Kwangu mimi nakumbuka nikiwa na utimamu wa kufuatilia siasa nchini hali hii ilijitokeza pia wakati hayati Mzee Mkapa anamaliza muda wake, fimbo hii pia ilitumika kumchapia Dr. Salim tena kwenye kinyang'anyiro cha awamu ya nne.
Cha kustaajabisha Dr Salim sikuwahi kwenye maisha yangu kumskia akilalamika sehemu yoyote ile bali alibaki kimya kwenye kigoda cha Mwalimu bila ya kuwa na nongwa.
Nionavyo Maisha ya Mzee Mwinyi na Dr Salim ni kama yanashabihiana kwa namna moja ama nyingine