Mnawafahamu waliompachika Dkt. Salim Ahmed Salim jina la Hezbollah katika kugombea Madaraka?

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
8,233
9,059
Wakati inasimuliwa historia ya maisha ya Mzee Ali Hassan Mwinyi kwenye maisha yake ya uongozi na Professor Mukandala kipengele hiki alikizungumzia, ni kinani hao tuwafahamu kwa mlio na kumbukumbu mpaka ilipelekea Mzee Mwinyi atengeneze nafasi ya naibu waziri mkuu na nafasi hizo na ile ya wizara ya ulinzi kukabidhiwa Dkt. Salim?

Kwangu mimi nakumbuka nikiwa na utimamu wa kufuatilia siasa nchini hali hii ilijitokeza pia wakati hayati Mzee Mkapa anamaliza muda wake, fimbo hii pia ilitumika kumchapia Dr. Salim tena kwenye kinyang'anyiro cha awamu ya nne.

Cha kustaajabisha Dr Salim sikuwahi kwenye maisha yangu kumskia akilalamika sehemu yoyote ile bali alibaki kimya kwenye kigoda cha Mwalimu bila ya kuwa na nongwa.

Nionavyo Maisha ya Mzee Mwinyi na Dr Salim ni kama yanashabihiana kwa namna moja ama nyingine
 
Mzee Mwinyi jana kuna sehemu pia alizungumzia Fitna alizopigwa Dr Salim japo hakumtaja Jina

Anasema 1985 wakati wanajadili jina la Mgombea Urais wa Jamhuri kutokea Upande wa Znz kulikuwa na Majina mawili;
1) Jina lake Ally Hasan Mwinyi akiwa Rais wa Znz wakati huo
2) Jina la pili ambalo amestahi kwa kutolitaja alikuwa Dr Salim Ahmed Salim (wakati huo alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri) ambae anakiri alipigwa Jungu kuwa kila akiongea huwa hatumii ile kauli mbiu ya 'Mapinduziiii Daimaaaa' kwa hiyo ikaonekana alikuwa mpinga Mapinduzi

Fitna zimeanza kitambo
 
Mzee Mwinyi jana kuna sehemu pia alizungumzia Fitna alizopigwa Dr Salim japo hakumtaja Jina

Anasema 1985 wakati wanajadili jina la Mgombea Urais wa Jamhuri kutokea Upande wa Znz kulikuwa na Majina mawili;
1) Jina lake Ally Hasan Mwinyi akiwa Rais wa Znz wakati huo
2) Jina la pili ambalo amestahi kwa kutolitaja alikuwa Dr Salim Ahmed Salim ( wakati huo alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri) ambae anakiri alipigwa Jungu kuwa kila akiongea huwa hatumii ile kauli mbiu ya 'Mapinduziiii Daimaaaa' kwa hiyo ikaonekana alikuwa mpinga Mapinduzi

Fitna zimeanza kitambo

Salim alikuwa kijana Sana wakati anaanza siasa..
Kumbuka anaenda kuwa Balozi Misri ana miaka 18 Tu ndo akaenda kusoma huko huko..

Alipaswa kuandika historia yake..
Alikuwa anapigwa vita na wengi
 
Mtandao wa Jakaya ulitumika kumuangusha Dr. Gharib Bilal mwaka 2000 kwenye NEC ya Bara na kumuibua Karume aliekuwa wa pili kutoka mwisho kwenye kura za NEC ya Znz

JK akajigeuza akiwa Waziri wa Mambo ya nje nakumbuka akajigeuza Kampen Manager wa Aman Karume hadi nakumbuka alionekana kwenye Magazeti akimfungulia Mlango wa Gari Karume wakati anaingia Dodoma Chimwaga kwenye kura kuashiria ndio Mgombea wake hivyo Wanamtandao wote wampe kura na ndicho kilichotokea

Ilipofika 2005 ikawa sasa zamu ya Karume kulipa fadhila kwa kuhakikisha Salim kwanza hapati kura za Wa Znz wenzie lakini pia aoneshwe yeye ni Hizbu na Mpinga Mapinduzi na baya zaidi akapakaziwa alikuwa kwenye mpango uliofanikiwa wa April 7, 1972 pale Kisiwandui
Ni kina Karume wakishirikiana nq mtandao wq kina Kikwete
 
Jana wakati inasimuliwa historia ya maisha ya Mzee Ali Hassan Mwinyi kwenye maisha yake ya uongozi na Professor Mukandala kipengele hiki alikizungumzia,ni kinani hao tuwafahamu kwa mlio na kumbukumbu mpaka ilipelekea Mzee Mwinyi atengeneze nafasi ya naibu waziri mkuu na nafasi hizo na ile ya wizara ya ulinzi kukabidhiwa Dr Salim?

Kwangu mimi nakumbuka nikiwa na utimamu wa kufuatilia siasa nchini hali hii ilijitokeza pia wakati hayati Mzee Mkapa anamaliza muda wake ,fimbo hii pia ilitumika kumchapiaDr Salim tena kwenye kinyang'anyiro cha awamu ya nne
Cha kustaajabisha Dr Salim sikuwahi kwenye maisha yangu kumskia akilalamika sehemu yoyote ile ,bali alibaki kimya kwenye kigoda cha Mwalimu,bila ya kuwa na nongwa .nionavyo Maisha ya Mzee Mwinyi na Dr Salim ni kama yanashabihiana kwa namna moja ama nyingine

Genge lilioongoza kumpiga vita Salim mwaka 1985 liliongozwa na Getrude Mongela..
Mongela alikuwa anafata maagizo ya 'taaasis' Fulani ya kidini
Iliyosema waunguja ndo moderate muslim so bora Mwinyi.. wapemba hawaaminiki ..wengi extremists..

Salim kusoma Misri pia kulimuongezea maadui...kuna mtu mmoja hapa Maarufu sana
Aliwahi kujaribu kum link Salim na Muslim Brotherhood'..

So fitina dhidi ya Salim ziko deep sana
 
Genge lilio ongoza kumpiga vita Salim mwaka 1985 liliongozwa na Getrude Mongela..
Mongela alikuwa anafata maagizo ya 'taaasis' Fulani ya kidini
Iliyosema waunguja ndo moderate muslim so bora Mwinyi.. wapemba hawaaminiki ..wengi extremists..

Salim kusoma Misri pia kulimuongezea maadui...kuna mtu mmoja hapa Maarufu sana
Aliwahi kujaribu kum link Salim na Muslim Brotherhood'..

So fitina dhidi ya Salim ziko deep sana
Nakubaliana na hoja ya mama Mongela ila sababu haikuwa dini sababu kubwa ni watu wazima kuona kwanini Salim kijana mdogo anapewa urais nsio wakampenyezea hoja mama Mongella ambaye alimkabili Nyerere na kumwuliza kwanini anamwacha makamu wake wa rais na kuchagua mtu mwingine dunia itamwelewaje au alikuwa amemweka makamu wa Rais kama boya hapa waliungana na wazanzibar wa unguja wasiotaka kutawaliwa na wapemba pamoja na wafidhihina wa bara
 
Mzee Mwinyi jana kuna sehemu pia alizungumzia Fitna alizopigwa Dr Salim japo hakumtaja Jina

Anasema 1985 wakati wanajadili jina la Mgombea Urais wa Jamhuri kutokea Upande wa Znz kulikuwa na Majina mawili;
1) Jina lake Ally Hasan Mwinyi akiwa Rais wa Znz wakati huo
2) Jina la pili ambalo amestahi kwa kutolitaja alikuwa Dr Salim Ahmed Salim ( wakati huo alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri) ambae anakiri alipigwa Jungu kuwa kila akiongea huwa hatumii ile kauli mbiu ya 'Mapinduziiii Daimaaaa' kwa hiyo ikaonekana alikuwa mpinga Mapinduzi

Fitna zimeanza kitambo
Kila ntu au kitu. Asipofanya vizuri katika ushindani wowote ule kisiasa basi hutafuta sababu.
za eti majungu yalipigwa si na wewe upige Majungu hayo? Tena zaidi yao hao wapinzani wako ...
ili ushinde?, km hukuweza tu ku-organise majungu rahisi hayo ndo umeshindwa sasa baba kalime mihogo tu.

Majungu ya kimataifa utayawezaje? Unalialia tuuu!! Km toto yatima

Siasa ni kugangamara!! ikibidi nyonga mtu live ili wengi tubaki salama.km jiwe alivoipata.leo nuru ipo.
Mnalia lia leo ooh! Majungu majungu sasa tumfanyeje??? Lazima alikuwa dhaifu maeneo flani.

Jk nyerere jabali lile kambona alipojipendekeza kumharibia ugsli wake. Heee!!
Mzanaki yule alitumia siraha rahisi kabisa
Mnajua wote kambona alitimka bila kugeuka mwenyewe bila kuguswa hata ukucha. Huyu alivunjwa vunjwa moyo kisiasa ni sawa.
Km alipigwa fitina alishindwa kupangua basi ni za ukweli.

Siasa siyo uji wa kupoozewa na ndugu au rafiki eti unywe.no!!!
Mleta mada japo ni mzee una mawazo finyu mnoo.
 
Wanasema Nyerere aliwahi kuwapenda viongozi 2 tu ,Sokoine na Salim.mliokuwepo kipindi hicho tuambieni ukweli kuhusiana na hili.

Salim alipewa ubalozi na Nyerere wakati ana miaka 18 tu..
Alilelewa na Nyerere..
Alijongezea sifa alipokuwa balozi wa Tz UN
Aliiongoza wajumbe wa UN kuipa China
Permanent membership..
USA walimchukia milele..
Wachina hadi wakasema Nyerere nabii wa Africa...Salim alimfanya Nyerere awe so proud..
Usisahau pia Salim katika nyazifa zote hakuwahi kupata kashfa ya kupiga hela yeyote na alikuwa na nafasi ya kujitajirisha.
Hata Bakhresa inasemekana alisaidiwa na Salim kuweza kupata nafasi ya biashara
Enzi hizo kuagiza kitu Ulaya sio kitu rahisi..
 
Nakubaliana na hoja ya mama Mongela ila aababu haikuwa dini sababu kubwa ni watu wazima kuona kwanini Salim kijana mdogo anapewa urais nsio wakampenyezea hoja mama Mongella ambaye alimkabili Nyerere na kumwuliza kwanini anamwqcha makamu wake wq rais nq kuchagua mtu mwingine dunia itamwelewaje au alikuwa amemweka makamu wa rais kama boya hapa waliungana na wazanzibar wanunguja wasiotaka kutawaliwa na wapembapamoja na wqfidhihina wa bara

Nafurahi watu kama wewe moo humu
Mnaweza kuthibitisha mambo kama haya tukiongea...

Wengine watoto wa juzi kazi kupinga kila kitu hata history hawaijui
 
Hapa inazungumzwa historia ya mambo na vijimambo vya zamani,

Sio Malalamiko Mkuu!
kila ntu au kitu. Asipofanya vizuri ktk ushindani wowote ule kisiasa basi hutafuta sababu.
za eti majungu yalipigwa si na wewe upige Majungu hayo? Tena zaidi yao hao wapinzani wako ...
ili ushinde?, km hukuweza tu ku-organise majungu rahisi hayo ndo umeshindwa sasa baba kalime mihogo tu.

Majungu ya kimataifa utayawezaje? Unalialia tuuu!! Km toto yatima

Siasa ni kugangamara!! ikibidi nyonga mtu live ili wengi tubaki salama.km jiwe alivoipata.leo nuru ipo.
Mnalia lia leo ooh! Majungu majungu sasa tumfanyeje??? Lazima alikuwa dhaifu maeneo flani.

Jk nyerere jabali lile kambona alipojipendekeza kumharibia ugsli wake. Heee!!
Mzanaki yule alitumia siraha rahisi kabisa
Mnajua wote kambona alitimka bila kugeuka mwenyewe bila kuguswa hata ukucha. Huyu alivunjwa vunjwa moyo kisiasa ni sawa.
Km alipigwa fitina alishindwa kupangua basi ni za ukweli.

Siasa siyo uji wa kupoozewa na ndugu au rafiki eti unywe.no!!!
Mleta mada japo ni mzee una mawazo finyu mnoo.
 
Mahusiano ya Nyerere na Sokoine ni kama ilivyokuwa kwa Jakaya na Magufuli wakati Jk Rais na Magu Waziri
Wanasema Nyerere aliwahi kuwapenda viongozi 2 tu ,Sokoine na Salim.mliokuwepo kipindi hicho tuambieni ukweli kuhusiana na hili.
 
Kawawa ni next level

Nyerere aliandika kwny Kitabu chake kuwa Mungu kaumba watu wachache sana wa aina ya Kawawa

Alipochoka kukaa na Kawawa kama PM kwa muda mrefu anasema alimwita Kawawa Mwenyewe amsaidie kuchagua Waziri Mkuu mwingine, alimshauri amchague Sokoine na ndio ikawa chaguo bora zaid

Kawawa ndio alikuwa 'Taulo' la Nyerere, Lawama na mabaya yote akawa analaumiwa Yeye

Wazee wanakwambia 'Operation vijiji vya Ujamaa' ya 1972 aliipinga sana Kawawa ndani ya Cabinet, lakin Maamuzi yalipofanyika alisimamia maamuzi yale na lawama akazibeba, Ingekuwa hawa kina Hamisi Maboda boda angesema 'niliwaambia lakin wakaniona mjinga'

Kawawa ndio Waziri pekee alieanza na kumaliza na Nyerere miaka yote ya Utawala wake na ndio chaguo la Nyerere la kwanza 1985 hadi Kamati kuu sema Wajumbe Nyoko wapo kitambo sana
Kawawa je?
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom