Mnawafahamu waliompachika Dkt. Salim Ahmed Salim jina la Hezbollah katika kugombea Madaraka?

Unaongea nini SASA?

Tunachokueleza sisi ni maneno wanavyosema jamaa zako wagalatia kuwa kila kiongoz Muislam akiwa MADARAKANI na akichagua mtu ambae ni Muislam anaitwa mdini na hao wagalatia,Ila akija kiongoz mkristo akafanya uteuzi wa upendeleo waz waz mnageuka,

Unaona sasa,unasema Magufuli akiteua kwa ukabila na siyo udini,unahamisha goli sasa,Magufuli katika baraza lake la mawazir Kulikuwa kuna mawazir 24, waislam walikuwa wanne tuh na hao 20 ni christians unasemaje hakuwa na udini, manaibu wazir walikuwa 16 na waislam wap wakijua sita unasemaje hakuwa na udini,hapo hujaenda KWA makatibu na manaibu katibu wakuu,so unataka kusema kwamba waislam hawana shule bado,?Hii hoja hamna pa kuchomokea
Bro, tuanze na wewe na boriti lako jichoni kwako, je unajua kuwa wewe ni mdini? Au hujui
 
..Je,habari kwamba Salim Ahmed Salim alikataa kuwa Makamu wa Raisi baada ya Dr.Omar Ali Juma kufariki ni kweli?

..kuna habari nyingine kwamba Salim A Salim aliombwa na Mwalimu arudi kugombea Uraisi mwaka 1995 wakati Mzee Mwinyi amemaliza muda wake lakini Salim akasita.

..kama ni kweli habari hizo ni kweli basi kilichomkosesha Uraisi Salim Ahmed Salim ni kigugumizi chake cha kupokea fursa za kisiasa zilizomtokea.
 
Kawawa ni next level

Nyerere aliandika kwny Kitabu chake kuwa Mungu kaumba watu wachache sana wa aina ya Kawawa

Alipochoka kukaa na Kawawa kama PM kwa muda mrefu anasema alimwita Kawawa Mwenyewe amsaidie kuchagua Waziri Mkuu mwingine, alimshauri amchague Sokoine na ndio ikawa chaguo bora zaid

Kawawa ndio alikuwa 'Taulo' la Nyerere, Lawama na mabaya yote akawa analaumiwa Yeye

Wazee wanakwambia 'Operation vijiji vya Ujamaa' ya 1972 aliipinga sana Kawawa ndani ya Cabinet, lakin Maamuzi yalipofanyika alisimamia maamuzi yale na lawama akazibeba, Ingekuwa hawa kina Hamisi Maboda boda angesema 'niliwaambia lakin wakaniona mjinga'

Kawawa ndio Waziri pekee alieanza na kumaliza na Nyerere miaka yote ya Utawala wake na ndio chaguo la Nyerere la kwanza 1985 hadi Kamati kuu sema Wajumbe Nyoko wapo kitambo sana
Hatari sana!!
 
Niliwahi mjibu mtu humu 19/12/2017

Mwinyi hakumgeuka Dr salim
Inaelezwa kuwa mwaka 1985 wakati wa kumtafuta mrithi wa mwalimu.

Inasemekena mwalimu nyerere alikuwa akimtaka sana Dr.salim ila mwalimu aliogopa fitna za makundi hasimu ya wanamstari(frontliners) na wale wagombozi (linerators) hii ilipelekea mwalimu nyerere kusuka njama.

Mwalimu nyerere alimfuata Rais Mwinyi wakati huo alikuwa ni Rais wa Zanzibar akamwambia Ali ntakupendekeza kuwa mrithi wangu kwa urais wa bara ila wewe ukatae..inasemekana Ali (Mwinyi) alikubali lakini kabla ya kikao kuanza Ali(Mwinyi) alimfuata sheikh Thabit Kombo(mshauri mkuu wa mwalimu Nyerere kuhusu maswala ya Zanzibar na huyu ndo alimpendekeza Mwinyi kuwa rais wa Zanzibar)

Akamwambia sheikh Thabit mwalimu kanambia "anipendekeze kuwa mrithi wake lakini akasema niikatae nafasi".
Sheikh Thabit akamwambia "ataka kukufanya punda wa dobi eeee, usikubali yeye akishakupendekeza kwenye mkutano wewe kubali"

Basi baadae kikao kikaanza huku mwalimu hajui hili wala lile, ana confidence kuwa atampendekeza Ali(Mwinyi) kuwa mrithi wake alafu Mwinyi atakaa basi kwake itakuwa rahisi kupendekeza jina la Dr. Salim.

Basi ghafla mwalimu akapendekeza jina la Rais wa Zanzibar Mwinyi kuwa mrithi wake JMT kwa kujiamini kabisa.
Ilipofika zamu ya kuzungumza Mwinyi AKAKUBALI dah mwalimu akatahayari hakuamini macho yake aliona kama Mwinyi kamgeuka.

Kwa hiyo mchezo ukaisha pale pale

Mwalimu 0-3 Mwinyi na makundi hasimu ya Dr. Salim.
Hizi ndio yale yale mastori ya mjini, ni uongo mtupu huu.
 
Kawawa ni next level

Nyerere aliandika kwny Kitabu chake kuwa Mungu kaumba watu wachache sana wa aina ya Kawawa

Alipochoka kukaa na Kawawa kama PM kwa muda mrefu anasema alimwita Kawawa Mwenyewe amsaidie kuchagua Waziri Mkuu mwingine, alimshauri amchague Sokoine na ndio ikawa chaguo bora zaid

Kawawa ndio alikuwa 'Taulo' la Nyerere, Lawama na mabaya yote akawa analaumiwa Yeye

Wazee wanakwambia 'Operation vijiji vya Ujamaa' ya 1972 aliipinga sana Kawawa ndani ya Cabinet, lakin Maamuzi yalipofanyika alisimamia maamuzi yale na lawama akazibeba, Ingekuwa hawa kina Hamisi Maboda boda angesema 'niliwaambia lakin wakaniona mjinga'

Kawawa ndio Waziri pekee alieanza na kumaliza na Nyerere miaka yote ya Utawala wake na ndio chaguo la Nyerere la kwanza 1985 hadi Kamati kuu sema Wajumbe Nyoko wapo kitambo sana
alikuwa Mr yes mzee! Watu wa hivo ni hatari sana.
Hautasogea kimaslahi utadumaa!

Waongo.
wanafiki.
roho mbaya
Wachawi
Wezi
Majungu
ndo wazuri hao unapata changa moto.
Km yusufu asingeuzwa na watu wenye roho mbaya tungekuwa bado tuko middle east.
 
Mzee Mwinyi jana kuna sehemu pia alizungumzia Fitna alizopigwa Dr Salim japo hakumtaja Jina

Anasema 1985 wakati wanajadili jina la Mgombea Urais wa Jamhuri kutokea Upande wa Znz kulikuwa na Majina mawili;
1) Jina lake Ally Hasan Mwinyi akiwa Rais wa Znz wakati huo
2) Jina la pili ambalo amestahi kwa kutolitaja alikuwa Dr Salim Ahmed Salim (wakati huo alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri) ambae anakiri alipigwa Jungu kuwa kila akiongea huwa hatumii ile kauli mbiu ya 'Mapinduziiii Daimaaaa' kwa hiyo ikaonekana alikuwa mpinga Mapinduzi

Fitna zimeanza kitambo
Salim alikuwa mwanachama Afro Shirazzi Party ujana wake. Uarabu wake umekuwa "liability". Wabaguzi ,CCM ZNZ wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka tu.
 
Mi navojua !ukishatoa kitabu cha historia ya maisha yako ujue kifo kinafuata!!!
Halafu jk hakuwa sawa coz alijua mechi itaahirishwa badae!!halafu yeye ndio alishauri mechi isogezwe mbele!alicheza boko usipime!!!
 
Hawakupiga kura

Halmashauri kuu iliweka vigezo 13 ili kumpata mrithi wa Mwalimu.

Wagombea walikuwa 3
1.Ally Hassan Mwinyi(Rais wa SMZ)
2.Rashid Mfaume Kawawa
3.Dr Salim Ahmed Salim

Mzee kawawa alijitoa mwanzoni kabisa na akasema jina lake lisijadiliwe ana akajenga hoja 2 kuu
1.Yeye na Mwalimu walionekana kama mapacha hivyo kama angelirithi mikoba ya Mwalimu watu wasingelihisi mabadiliko yoyote akapendekeza aje mtu mpya na fikra mpya.
2. Sababu za kiafya
Halmashauri kuu ikamkubalia na kuondoa jina lake.
Majina yakabaki mawili.

Aliyefuatwa kujadiliwa ni Ally Hassan mwinyi ambaye wajumbe walionekana kumtaka sana wakiongozwa na wahafidhin( Liberators wakombozi) kutoka Zanzibar kazi yao kuu ilikuwa ni kuhakikisha mu hizbu Dr. Salim ambaye ni chaguo la Mwalimu kuwa hawi Rais wa Jamhuri.
Hii ilipelekea Mzee Mwinyi kupata vigezo karibia vyote 13.
Na hapa Mwalimu akasimama akasema "Kama ni hivyo haya...hakuna haja ya kujadili jina la tatu, mgombea wetu ni Ally Hassan Mwinyi Rais wa SMZ..."

NB
Kwahiyo Dr. Salim hakujadiliwa kwenye kikao wala hakukupigwa kura.
kwanini Nyerere alimpendekeza Ali Hassan kwasababu alikuwa na khofu kwamba Zanzibar itapata maendeleo sana nchini ya Ali Hassan na Seif Sharif hiyo ndio sababu ya Nyerere kumpendekeza Ali Hassan mwinyi kutoka Mkuranga
 
Wakati inasimuliwa historia ya maisha ya Mzee Ali Hassan Mwinyi kwenye maisha yake ya uongozi na Professor Mukandala kipengele hiki alikizungumzia, ni kinani hao tuwafahamu kwa mlio na kumbukumbu mpaka ilipelekea Mzee Mwinyi atengeneze nafasi ya naibu waziri mkuu na nafasi hizo na ile ya wizara ya ulinzi kukabidhiwa Dkt. Salim?

Kwangu mimi nakumbuka nikiwa na utimamu wa kufuatilia siasa nchini hali hii ilijitokeza pia wakati hayati Mzee Mkapa anamaliza muda wake, fimbo hii pia ilitumika kumchapia Dr. Salim tena kwenye kinyang'anyiro cha awamu ya nne.

Cha kustaajabisha Dr Salim sikuwahi kwenye maisha yangu kumskia akilalamika sehemu yoyote ile bali alibaki kimya kwenye kigoda cha Mwalimu bila ya kuwa na nongwa.

Nionavyo Maisha ya Mzee Mwinyi na Dr Salim ni kama yanashabihiana kwa namna moja ama nyingine
Ahmed Salim alikua kiongozi mwenye nidhamu na mwanamapinduzi. Nadhani hii ilimfanya kutokua na ubinafsi kiasi cha kukaa kimya adui zake walipomfanyia hila.
 
Wakati inasimuliwa historia ya maisha ya Mzee Ali Hassan Mwinyi kwenye maisha yake ya uongozi na Professor Mukandala kipengele hiki alikizungumzia, ni kinani hao tuwafahamu kwa mlio na kumbukumbu mpaka ilipelekea Mzee Mwinyi atengeneze nafasi ya naibu waziri mkuu na nafasi hizo na ile ya wizara ya ulinzi kukabidhiwa Dkt. Salim?

Kwangu mimi nakumbuka nikiwa na utimamu wa kufuatilia siasa nchini hali hii ilijitokeza pia wakati hayati Mzee Mkapa anamaliza muda wake, fimbo hii pia ilitumika kumchapia Dr. Salim tena kwenye kinyang'anyiro cha awamu ya nne.

Cha kustaajabisha Dr Salim sikuwahi kwenye maisha yangu kumskia akilalamika sehemu yoyote ile bali alibaki kimya kwenye kigoda cha Mwalimu bila ya kuwa na nongwa.

Nionavyo Maisha ya Mzee Mwinyi na Dr Salim ni kama yanashabihiana kwa namna moja ama nyingine
Ali Hassan Mwinyi ni mnufaika wa ghiliba, fitina na mizengwe ya kutisha dhidi ya Dr Salim Ahmed Salim, rejea mchakato wa kumpata mrithi wa Mwalimu Nyerere alipong'atuka 1985 utanielewa!
 
Na mwinyi ndiye alimtengenezea njia kikwete kwa kumbeba kwa mambo mengi
Ali Hassan Mwinyi ni mnufaika wa ghiliba, fitina na mizengwe ya kutisha dhidi ya Dr Salim Ahmed Salim, rejea mchakato wa kumpata mrithi wa Mwalimu Nyerere alipong'atuka 1985 utanielewa!
 
Dr Salim alitifuana na Wamarekani pale alivyopiga kura UN kuisaidia China mpaka Ronald Reagan akawakashifu Waafrika na kuwaita manyani

Back
Top Bottom