Mnawafahamu waliompachika Dkt. Salim Ahmed Salim jina la Hezbollah katika kugombea Madaraka?

Huo ndio ukweli, mtu dhaifu katika siasa anabaki kulalamika anapigwa fitna na majungu. Siasa kupambana kweli.
 
Vijiji vya Ujamaa vilikuwa 1972 wakati huo Kambona kishavurugana na Nyerere miaka kadhaa, nadhan umechanganya na Azimio la Arusha

Kawawa alikuwa Yes Sir baada ya makubaliano sio kuwa hakuwa na mawazo binafsi kwny mijadala
ahaa
 
Hapana kura zilipigwa kwenye halmashauri kuu mwinyi akashinda
Hawakupiga kura

Halmashauri kuu iliweka vigezo 13 ili kumpata mrithi wa Mwalimu.

Wagombea walikuwa 3
1.Ally Hassan Mwinyi(Rais wa SMZ)
2.Rashid Mfaume Kawawa
3.Dr Salim Ahmed Salim

Mzee kawawa alijitoa mwanzoni kabisa na akasema jina lake lisijadiliwe ana akajenga hoja 2 kuu
1.Yeye na Mwalimu walionekana kama mapacha hivyo kama angelirithi mikoba ya Mwalimu watu wasingelihisi mabadiliko yoyote akapendekeza aje mtu mpya na fikra mpya.
2. Sababu za kiafya
Halmashauri kuu ikamkubalia na kuondoa jina lake.
Majina yakabaki mawili.

Aliyefuatwa kujadiliwa ni Ally Hassan mwinyi ambaye wajumbe walionekana kumtaka sana wakiongozwa na wahafidhin( Liberators wakombozi) kutoka Zanzibar kazi yao kuu ilikuwa ni kuhakikisha mu hizbu Dr. Salim ambaye ni chaguo la Mwalimu kuwa hawi Rais wa Jamhuri.
Hii ilipelekea Mzee Mwinyi kupata vigezo karibia vyote 13.
Na hapa Mwalimu akasimama akasema "Kama ni hivyo haya...hakuna haja ya kujadili jina la tatu, mgombea wetu ni Ally Hassan Mwinyi Rais wa SMZ..."

NB
Kwahiyo Dr. Salim hakujadiliwa kwenye kikao wala hakukupigwa kura.
 
Sheikh adui wetu ni wanafiq waislamu wenzetu...tusijidanganye
Mzee mwinyi kwenye kitabu chake kaandika kuwa kwa kuwa yeye Muislam eti walikuwa wanamtuhum kuwa alikuwa anateua viongoz kwa upendeleo wa kidini,kumbe wagalatia drama hizi za fitna za udini hawakuanza leo hawa jamaa
 
Wakati inasimuliwa historia ya maisha ya Mzee Ali Hassan Mwinyi kwenye maisha yake ya uongozi na Professor Mukandala kipengele hiki alikizungumzia,ni kinani hao tuwafahamu kwa mlio na kumbukumbu mpaka ilipelekea Mzee Mwinyi atengeneze nafasi ya naibu waziri mkuu na nafasi hizo na ile ya wizara ya ulinzi kukabidhiwa Dr Salim?

Kwangu mimi nakumbuka nikiwa na utimamu wa kufuatilia siasa nchini hali hii ilijitokeza pia wakati hayati Mzee Mkapa anamaliza muda wake ,fimbo hii pia ilitumika kumchapiaDr Salim tena kwenye kinyang'anyiro cha awamu ya nne
Cha kustaajabisha Dr Salim sikuwahi kwenye maisha yangu kumskia akilalamika sehemu yoyote ile ,bali alibaki kimya kwenye kigoda cha Mwalimu,bila ya kuwa na nongwa .nionavyo Maisha ya Mzee Mwinyi na Dr Salim ni kama yanashabihiana kwa namna moja ama nyingine
Kwa sasa inaonekana kana masikhara, lakini tusisahahu hii SMZ ni serkali ya mapinduzi (mapindizi ya kikwelikweli, yale ya chama cha mapinduzi). Ni watu walimwaga damu kujikomboa. Mwaka huu viongozi wa mapinduzi at least 6 walikuwa hai, wakiwamo Saidi Natepe, Ramadhani Haji, Seif Bakari na Ali Anmeir. There is no way wangemwachia Mwarabu atawale tena, no way. Watakuwa walikumbuka mwenzao Karume alivyouliwa 1972. Iwapo utafikiria vinginevyo hujui maana ya mapinduzi,
 
Wanasema Nyerere aliwahi kuwapenda viongozi 2 tu, Sokoine na Salim. Mliokuwepo kipindi hicho tuambieni ukweli kuhusiana na hili.
Nyerere aliwaamini ndio mawaziri wakuu vijana zaidi kutokea kwa kifupi Nyerere aliandaa viongozi wazuri kiasi walipoenda kimataifa walifanya vizuri sana kama Salim, Mahiga, Mwakawago
 
Salim alipewa ubalozi na Nyerere wakati ana miaka 18 tu..
Alilelewa na Nyerere..
Alijongezea sifa alipokuwa balozi wa Tz UN
Aliiongoza wajumbe wa UN kuipa China
Permanent membership..
USA walimchukia milele..
Wachina hadi wakasema Nyerere nabii wa Africa...Salim alimfanya Nyerere awe so proud..
Usisahau pia Salim katika nyazifa zote hakuwahi kupata kashfa ya kupiga hela yeyote na alikuwa na nafasi ya kujitajirisha.
Hata Bakhresa inasemekana alisaidiwa na Salim kuweza kupata nafasi ya biashara
Enzi hizo kuagiza kitu Ulaya sio kitu rahisi..
So Salim was the best president we never had?
 
Genge la Mkwere! Wapo hapo nje wanapasha kuingia uwanjani!
(Nipo kwenye ibada nikitoka nitaeleza kwa marefu na mapana, nimepata nafasi ya kuja JF kwakuwa naona kunachozungumziwa hapa kanisani sio kuacha dhambi, tunaambiwa kuchanga pesa tu haijalishi umezipata kwa njia ipi Mungu anahitaji pesa Sana siku hizi!)


Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Salim alikuwa kijana Sana wakati anaanza siasa..
Kumbuka anaenda kuwa Balozi Misri ana miaka 18 Tu ndo akaenda kusoma huko huko..

Alipaswa kuandika historia yake..
Alikuwa anapigwa vita na wengi
Duuuh 18 yrs anakuwa balozi wa nchi? Heeeeh mbna ilikua hatareeeh.

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Niliwahi mjibu mtu humu 19/12/2017


Mwinyi hakumgeuka Dr salim
Inaelezwa kuwa mwaka 1985 wakati wa kumtafuta mrithi wa mwalimu.

Inasemekena mwalimu nyerere alikuwa akimtaka sana Dr.salim ila mwalimu aliogopa fitna za makundi hasimu ya wanamstari(frontliners) na wale wagombozi (linerators) hii ilipelekea mwalimu nyerere kusuka njama.

Mwalimu nyerere alimfuata Rais Mwinyi wakati huo alikuwa ni Rais wa Zanzibar akamwambia Ali ntakupendekeza kuwa mrithi wangu kwa urais wa bara ila wewe ukatae..inasemekana Ali (Mwinyi) alikubali lakini kabla ya kikao kuanza Ali(Mwinyi) alimfuata sheikh Thabit Kombo(mshauri mkuu wa mwalimu Nyerere kuhusu maswala ya Zanzibar na huyu ndo alimpendekeza Mwinyi kuwa rais wa Zanzibar)

Akamwambia sheikh Thabit mwalimu kanambia "anipendekeze kuwa mrithi wake lakini akasema niikatae nafasi".
Sheikh Thabit akamwambia "ataka kukufanya punda wa dobi eeee, usikubali yeye akishakupendekeza kwenye mkutano wewe kubali"

Basi baadae kikao kikaanza huku mwalimu hajui hili wala lile, ana confidence kuwa atampendekeza Ali(Mwinyi) kuwa mrithi wake alafu Mwinyi atakaa basi kwake itakuwa rahisi kupendekeza jina la Dr. Salim.

Basi ghafla mwalimu akapendekeza jina la Rais wa Zanzibar Mwinyi kuwa mrithi wake JMT kwa kujiamini kabisa.
Ilipofika zamu ya kuzungumza Mwinyi AKAKUBALI dah mwalimu akatahayari hakuamini macho yake aliona kama Mwinyi kamgeuka.

Kwa hiyo mchezo ukaisha pale pale

Mwalimu 0-3 Mwinyi na makundi hasimu ya Dr. Salim.
Aiseeeeeh hii nchi ina historia ndefu hivi kumbe? Duuuuh

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Mfumo wa Ulinzi dhidi ya Makombora kule Msoga ni mkali sana …naambiwa 'ukirusha kombora' halitunguliwi bali linarudishwa lilipotoka kwa kasi zaidi

Huenda 'uranium' inayorutubisha vinu vya Nuclear kule Mwandiga kwa kina Zitto ndiyo hiyo hiyo inayochakatwa kule Msoga
hatareeeeh sana.

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Hawakupiga kura

Halmashauri kuu iliweka vigezo 13 ili kumpata mrithi wa Mwalimu.

Wagombea walikuwa 3
1.Ally Hassan Mwinyi(Rais wa SMZ)
2.Rashid Mfaume Kawawa
3.Dr Salim Ahmed Salim

Mzee kawawa alijitoa mwanzoni kabisa na akasema jina lake lisijadiliwe ana akajenga hoja 2 kuu
1.Yeye na Mwalimu walionekana kama mapacha hivyo kama angelirithi mikoba ya Mwalimu watu wasingelihisi mabadiliko yoyote akapendekeza aje mtu mpya na fikra mpya.
2. Sababu za kiafya
Halmashauri kuu ikamkubalia na kuondoa jina lake.
Majina yakabaki mawili.

Aliyefuatwa kujadiliwa ni Ally Hassan mwinyi ambaye wajumbe walionekana kumtaka sana wakiongozwa na wahafidhin( Liberators wakombozi) kutoka Zanzibar kazi yao kuu ilikuwa ni kuhakikisha mu hizbu Dr. Salim ambaye ni chaguo la Mwalimu kuwa hawi Rais wa Jamhuri.
Hii ilipelekea Mzee Mwinyi kupata vigezo karibia vyote 13.
Na hapa Mwalimu akasimama akasema "Kama ni hivyo haya...hakuna haja ya kujadili jina la tatu, mgombea wetu ni Ally Hassan Mwinyi Rais wa SMZ..."

NB
Kwahiyo Dr. Salim hakujadiliwa kwenye kikao wala hakukupigwa kura.
Maskini baba wa watu sijui alikosa nn huyo SALIM.

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Ambalo liko dhahiri ni hili, Mwinyi hakuwa chaguo la Mwalimu hata kidogo na haya yalikuwa wazi kabisa. Mwinyi ni kati ya marais ambao hawakuwahi kufurahia uraisi wao, Mwalimu kila alichofanya mwinyi alipinga ama kumsakama. Kuna za chini chini kwamba kuna kipindi Mwinyi alichoka na kashfa za Mwalimu akataka kumweka detention ama kumuua. Ni bahati mbaya kwamba mpango ulivuja na mwalimu akamuendea Mwinyi na kumuabia 'nasikia unataka kuniua, haya nimalize hapa hapa'
 
Mtandao wa Jakaya ulitumika kumuangusha Dr. Gharib Bilal mwaka 2000 kwenye NEC ya Bara na kumuibua Karume aliekuwa wa pili kutoka mwisho kwenye kura za NEC ya Znz

JK akajigeuza akiwa Waziri wa Mambo ya nje nakumbuka akajigeuza Kampen Manager wa Aman Karume hadi nakumbuka alionekana kwenye Magazeti akimfungulia Mlango wa Gari Karume wakati anaingia Dodoma Chimwaga kwenye kura kuashiria ndio Mgombea wake hivyo Wanamtandao wote wampe kura na ndicho kilichotokea

Ilipofika 2005 ikawa sasa zamu ya Karume kulipa fadhila kwa kuhakikisha Salim kwanza hapati kura za Wa Znz wenzie lakini pia aoneshwe yeye ni Hizbu na Mpinga Mapinduzi na baya zaidi akapakaziwa alikuwa kwenye mpango uliofanikiwa wa April 7, 1972 pale Kisiwandui
Kundi la watu wa siasa chafu za maji taka, kundi la 'do whatever it takes'. Mkwere ni mahiri sana kwenye siasa hizi, Karume(mtu wa bapa) yeye alikuwa analipa 'fadhila' kwa kuwa anakumbuka bila ya Mkwere asingeukwaa urias wa Zenji.
 
Back
Top Bottom