Mnavyofikiria Tanzania inakosea wapiI?

john uloto

New Member
Mar 21, 2016
2
0
Kwangu mimi sehemu ambayo Tanzania inakosea, na kama ningekuwa Magufuli vitu ambavyo ningerekebisha.

1. RUSHWA
Zinahitajika sheria kali za kupambana na rushwa sio hizi za kwenda jela miaka michache alafu ukirudi mtaani unakula bata kwa zile pesa ulizoiba.kama tungefanya mtu akikamatwa na kosa la kuiba hela za serikari ANAFIRISIWA mali zake zote na serikari unafikiri nani angethubutu kuiba au nani angethubutu kuiba juu juu hivi.najua ufisadi upo kote duniani lakini ukienda ichi zilizoendelea zipo sheria kali ndo maana ufisadi aupo juu juu kama Tanzania.

2.UWEKEZAJI
Serikari zote zilizopita zinawekeza katika miundombinu tena kwa asilimia ndogo tu,lakini haiwekezi kwa wananchi wa Tanzania kivip CCM ipo tayari kwenda china kumtoa engineer wa kujenga majengo na kati hapa Tanzania kuna watu wana uwezo wa kujenga kuliko hata hao wachina kama tungewaamini mafundi wetu hapa nyumabani tungetengeneza kazi nyingi na sio tenda maana sahivi tunatengeneza tenda tuu,kampuni zote za natural resources zinabidi zimilikiwe na viwanda vya Tanzania kwa sabau hizi kampuni za nche sisi wazawa tunafaidika kwenye kodi na kazi lakini faida zote zinaenda nchini kwao badala ya kuwekeza nchini kwetu.,serikari iwekeze kwenye viwanda vya finishing and processing mfano tunachimba coal na tunauza nje lakini hapa nyumbani tunahangaika hakuna umeme nakati tuna coal,gas,jua,maji.uranium,upepo,mawimbi hivi vitu vyote vinaweza kuzarisha umeme lakini tanesco wanategemea maji kwanini nakati hivi vitu vyote tunaweza kutumia kuzarisha umeme lakini instead tunapeleka nje ya nchi wenzetu wanatumia kuzarishia umeme kwanini sisi tushindwe na hivi vitu vyote tunafundishwa mashuleni .

3.KILIMO NA UFUGAJI.
Serikari iwekeze kwenye packaging industry na hivyo viwanda viwe vina process mazao na kutengeneza finished goods na serikali ipige marufuku kwa wafanya biashara wadogo kuuza bidhaa ambazo hazipo kwenye package mfano unga,mchele,maharage,nk wauza maduka wote wasipime bali wanunue kwenye packaging industry.kufanya hivyo tutawapa moyo wakulima wazidi kulima Zaidi kwasababu watakuwa wamesainishwa kwenye packaging industry ambapo watapata soko imara na wavuvi pia hivi viwanda pia vitasafirisha hivi vyakula afrika nzima na kuongeza pato la kodi.

4.RASILIMALI.
vyuma vyote vinavyochimbwa Tanzania vinabidi tuviuze vikiwa bado havijakamilika kuwa finished product na pia tuuze vikiwa vimekamilika mfano tunachimba iron na carbon lakini sasa tunanua steel china nakati tunauwezo wa kutengeneza hivi vyuma hapa nyumbani

Haya ni machache tu. SASA SWALI PESA ZINATOKA WAPI ZA KUKAMILISHA HIVI VITU.

MAJIBU.
wabunge wanapokea mshahara wa bei gani tuseme tu kwa mfano million 5 kwa mwezi.haya kwa miezi 12 mbunge mmoja anachukua Zaidi ya million 50 kwa kazi gani wanayofanya.tukikata mishahara ya wabunge na raisi kwa asilimia hamsini hatujapata hela ya kutatua tatizo moja kila mwaka. kila siku tunasikia bajeti haitoshi lakini lini umesikia leo bajeti ndogo tunabidi tukate mishahara ya wabunge, mawaziri na raisi tuongezee kwenye bajeti lini utasikia ahh tunabidi tuombe mikopo.

Tourisim. wanyama wanazidi kufa kila siku harafu utalii ni moja ya sehemu ambayo serikari inategemea, tuwabane hawa wawindaji haramu kwa sheria kali pia tuwahamishe watu wote wanao kaa karibu na mbunga maana simba wengi wanakufa kutokana na sumu zinazowekwa ndani ya mifugo wewe fikiria Tanzania bila simba nani hatakuja kuangalia wanyama.

Kitu chingine cha muhimu ni AFRICA TUUNGANE TUWEKE FREE MOVEMENT ZA WAFANYABIASHARA NA WATALII KUTOKA AFRICA, WAAFRIKA WOTE WAPATE FREE MOVEMENT CARd.

HAYA NI KWA UFUPI TU NYIE NDUNGU ZANGU MNASEMAJE KWA NILIVYOANDIKA HAPO JUU,HAYO NI MACHACHE TU MAANA NINAYO MENGI YA KUSEMA.
 
Back
Top Bottom