Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa kiuchumi?

hapa tunamshauri magufuli na sio ccm na ndio maana kwenye uchaguzi alikuwa anasema chagua magufuli na sio ccm...acha upuuzi huu uzi umekupita uwezo na iq yako kama dental formula ya kuku.
Hujajibu nilichokihoji bwa mdogo!
Nimehoji hivi....Mtetezi wa ufisadi atamshauri nini muadilifu?....fanya assumption unayoitaka ya kuwa Magufuli sio mwanaccm..

kumbuka kwenye huo huo uchaguzi mlikuwa mnazungushwa mikono kwa ajili ya lowasa na sio Chagadema au Ukiwa!
 
Unafahamu hasara ya kumfukuza kazi mtu ambaye baadaye anakushtaki na kushinda kesi??? Usiongee kama hujui mkuu. Magufuri yuko sahihi kabisa na hiyo ndio haki yenyewe. Wamesimamishwa si kwasababu wanamakosa bali wamesimamishwa kwa sababu wanahisiwa ili kupisha uchunguzi. Uchunguzi ukigundua kuwa wanamakosa basi watafukuzwa kazi na ukibaini kuwa hakuna makosa watarudishwa kazini kwa kuendelea na nafasi ileile au kwa kupangiwa majukumu mengine
Nimekupata vema Mkuu, tunamtimua mtu kazi, then!!!!?????? Au mtu anajiuzuru, harafu!!!!!??????
Mimi nachotaka mtu akimuliwa au akijiuzuru maisha yake yachunguzwe na mali anazomiliki, unamtimua mtu kazi harafu kavuna 10Bilionz, ukimtimua kuna hasara gani kwake, tena katia hasara mpaka kwa taifa. Kutimua mtu haitoshi bali ataifishwe kabisa, tena tuanze na mawaziri waliojiuzuru ka akina Lowassa, viongozi kama akina Rostam, twende mpaka ktk familia ya Kikwete. Leo hii mtaani watu tunapigika kutokana na Ufisadi wao. Wanaolipa deni la Taifa ni sisi na sisi ndio tunaumia harafu wao pesa wamejiwekea majumbani kwao. Afsa mdogo wa TRA kakutwa na 250Milionz, hao akina Karamagi utawakuta na sh.ngapi?
 
Hujamuelewa mleta mada, yeye anasema kwanini wasitimuliwe moja kwa moja kuliko kusimamishwa? Mtu akisimamishwa bado pesa anapokea yaani mshahara wake upo palepale. Ni kweli Magufuli kafanya jambo la maana ila watu wahujumu uchumi kama hawa walipaswa kutimuliwa moja kwa moja na kushtakiwa.
Utawala wa sheria huwezi kumtimua mtumishi bila kufata taratibu ndugu. Kwa michango bora ya pasco hapa jf wala siamini kama alimaanisha hivyo.

Pasco nakukubali sana kwa mada zako ila kwa leo nahisi umechemka ndugu yangu.

Hawa watu huenda wanaliingizia taifa hasara mara 1000 ya mishahara yao.

Huu utamaduni wa Kuanza kutetea watu wenye tuhuma naona unaanza kuzoeleka.

Pole tanzania.
 
Ni hulka ya kina Pasco kuwatetea watuhumiwa!!
Labda ni kutokana na uanasheria wake!!
 
Nimekupata vema Mkuu, tunamtimua mtu kazi, then!!!!?????? Au mtu anajiuzuru, harafu!!!!!??????
Mimi nachotaka mtu akimuliwa au akijiuzuru maisha yake yachunguzwe na mali anazomiliki, unamtimua mtu kazi harafu kavuna 10Bilionz, ukimtimua kuna hasara gani kwake, tena katia hasara mpaka kwa taifa. Kutimua mtu haitoshi bali ataifishwe kabisa, tena tuanze na mawaziri waliojiuzuru ka akina Lowassa, viongozi kama akina Rostam, twende mpaka ktk familia ya Kikwete. Leo hii mtaani watu tunapigika kutokana na Ufisadi wao. Wanaolipa deni la Taifa ni sisi na sisi ndio tunaumia harafu wao pesa wamejiwekea majumbani kwao. Afsa mdogo wa TRA kakutwa na 250Milionz, hao akina Karamagi utawakuta na sh.ngapi?
Kwa hilo upo sahihi mkuu. Kila anayefukuzwa kazi anatakiwa kuchunguzwa pia na akithibitika kuhusika na matumizi mabaya ya madaraka anapaswa kuchukuliwa hatua. Kumfukuza kazi mtu aliyeiba 1bilioni bila kumbana arudishe hiyo pesa haisaidii, tena huko ni kuwahadaa watanzania. Kuna haja ya kuwafilisi wote wanaothibitika kuhujumu uchumi wa taifa hila. Ila ushahidi uwepo, sio kuwaonea watu.
 
Hivi Mkuu unadhani ushahidi kuhusu RICHMOND haupo? Meremeta, Rada, TPA, ESCROW n.k kote huko ushahidi upo
Ni sawasawa na yale Makontena 340 yaliyokamatwa harafu unaambiwa hawana majina ila wana idadi tu ya Makontena, haya kama sio matusi kwa Watanzania ni nini hasa?
Ushahidi hata ukipatikana wakufilisi ni nani? Hao watu mwisho wa siku ni kutimuliwa kazi tuu, HAKUNA ZAIDI YA HAPO.
Eti taifa lina deni la 49Trilionz, sasa hizi pesa zimefanyia nini Uraiani? Watanzania tumenufaika na nini na hili deni?
Mimi nikikaa na kutafakari siasa Tanzania huwa nashikwa na hasira za ajabu sana.
Soko la mafuta dunia nzima limeshuka, angalia Tanzania mafuta unanunua kwa sh.ngapi? Ukichunguza chanzo ni nini utagundua wao ndo wanamiliki sheli.
 
pasco at least ungequantify hiyo hasara/gharama kuliko kuongea maneno matupu...sahihisho,mtumishi wa umma akisimamishwa anaendelea kupokea mshahara kamili hadi shauri lake linapoamriwa...pasco uwe unapitia nyaraka mpya za serikali
Huo ndo ukweli hakuna nyaraka mpya ukisimamishwa unaendelea kula mshahara mpk ukutwe na hatia ndo upelekwe mahakamani au ufukuzwe
 
Pasco aka Mwanaukawa damu unadhani Mzee wa kubana matumizi (magu) hajaliona hilo? Baada ya mwezi fuatilia hao waliosimamishwa watakuwa wapi halafu utapata jibu kama wanakula mishahara ya bure au bado wapo kwenye payroll.
Siku za karibuni humu kumegeuzwa sehemu ya matusi zaidi kuliko kujibu hoja
. Mtu hajaisoma hoja na kuielewa anananza kubwabwaja tu. Tusiendekeze ushabiki. Kwenye ukweli pabaki ni ukweli
tuweze kusogeza taifa mbele. Bila kukosolewa mwanadamu hatakaa ajifunze.
 
Na siku za karibuni Kuna watu mmeibuka mnajifanya mnaelewa hoja. Mnasoma thread na bado hamuelewi. Kama wewe Ni mtu makini hiyo hoja unayoongelea haipo zaidi ya shabiki wa UKAWA anajaribu kukosoa mambo ambayo yapo very clear.
 
Back
Top Bottom