Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa kiuchumi?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,679
119,314
Wanabodi,
Hii ni mada kuhusu baadhi ya maamuzi ya rais wetu, Mhe. Dr. John Pombe Joseph Mugufuli anayoyafanya sasa huku watu wanashangilia sana kila kinachofanywa na Rais wetu, wakiamini na wakidhani kila anachokifanya rais ndio the right thing to do kwa taifa letu and done at the right time and done rightly!.

No way, rais Magufuli pia ni binaadamu na sio malaika, hivyo sio lazima kila anachokifanya rais Magufuli kiwe ndio the right thing!. Kuna vitu vingi vikubwa na vizuri, rais Magufuli anafanya, he is doing the right thing hivyo ni haki tumshangilie, lakini kuna vingine rais wetu anavyofanya sio, na hakuna watu wa kumwambia mhe. rais, hili sio, kutokana na hulka yake, ila sisi watu wa mitandaoni tuu ndio tunaweza, because we have nothing to lose, waliomzunguka na sisi Watanzania kwa sasa, kwa vile tumehamanika
na Magufulification phobia, tunashangilia kila rais anachokifanya bila kufanya tathmini ya short time, medium term na long term effects ya maamuzi ya rais wetu ya sasa, madhara yake yatakuja kuonekana baadae!, wakati huo watu hawatakumbuka chanzo.

Kuna mengi rais Magufuli, is doing the right thing, at the right time, kwa mengi ya maamuzi yake, lakini sio yote!, kuna baadhi ya maamuzi
1. Rais Magufuli is doing the right thing at the right time and doing it right!.
2. Rais Magufuli is doing the right thing at the right time but doing it wrong!.
3. Rais Magufuli is doing the right thing at the wrong time and doing it right!.
4. Rais Magufuli is doing the right thing and the wrong time and doing it wrongly!.
5. Rais Magufuli is doing the wrong thing and the right time and doing it right!..
6. Rais Magufuli is doing the wrong thing and the right time and doing it wrongly!.
7. Rais Magufuli is doing the wrong thing at the wrong time and done it right.
8. Rais Magufuli is doing the wrong thing and the wrong time and done it wrongly!.

Japo rais wetu ni binadamu na sio malaika, lakini kwa vile ni mkuu wetu, ndie supreme leader wetu, hivyo sisi wananchi wake tuna the highest standards of expectations of him kumhusu yeye kuwa he has to be perfect, he got to do things right by doing the right thing at the right time and doing it right ndio maana ana wasaidizi, washauri na all instruments to make things right.

Mtu mwingine yoyote, anaweza kufanya makosa yoyote na akawa tolerated, asiwe noticed, kwa kukaushiwa au kwa kuvumiliwa, lakini kwa mtu anayepaswa kuwa perfect hata akifanya kosa dogo tuu, he will be noticed, na wakusema, tutasema!, na kusema kwenyewe hatusemi ili tuu kuonyesha the human side ya rais wetu, tutasema kwa kutumia constructive criticism ili kumsaidia kwa kushauri the right thing and the right way of doing some things na kwa kuandika wazi, openly and transparently kuweka kumbukumbu sawa, wakati tukianza kuathirika kwa maamuzi haya haya, baadhi yetu tutakuwa na justification ya kukumbusha kuwa hayakutokea kwa bahati mbaya and there will be no excuse kuwa hatukujua the consequences of our actions and decisions .
Haya ni baadhi ya yangu.
  1. Baraza Dogo la Mawaziri Jina Tuu, Sii Dogo!. Kuundwa kwa Baraza dogo la Mawaziri, lengo na maana yake ni kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali. Lakini rais Magufuli alipoamua kuunda baraza dogo la mawaziri, na kuongeza idadi ya makatibu wakuu, badala ya kupunguza gharama, kutaongeza gharama za uendeshaji!. Serikali ni makatibu wakuu ambao ndio waendeshaji, Makatibu Wakuu ni waajiriwa permanent, they are there to stay na sio mawaziri, mawaziri ni political appointees tuu, yaani ni watu wa kuja na kuitaka, yaani ni ma dispensables, bila hasara yoyote, they can just come and go!, lakini makatibu wakuu ni indispensable, ukimuondoa, lazima uendelee kumlipa mpaka muda wake ufike, hivyo serikali ndogo yenye makatibu wakuu wengi na big load ya waliokaa kijiweni tuu, gharama za uendeshaji wa serikali zitakuwa pale pale au zitaongezeka!.
  2. Kuunganisha Wizara Kusiko na Tija. Kuna wizara ambazo ameziunganisha, lakini kwa maoni yangu, hazikupaswa kuunganishwa au kuunganishwa huko hakuna tija, na hili litakuja kuwa proved mbele ya safari kwa pangua pangua!, Wizara nyingine ni too big to manage effectively na waziri mmoja tuu tena asiye hata na naibu!, mfano Prof. Mbarawa!. Naamini in due time, ama atazifumua, au atateua manaibu, ila kwa kuunda serikali ndogo, kiukweli Magufuli hajapunguza chochote na sana sana ataongeza gharama za uendeshaji na hili liutathibitishwa na wage bill, itaongezeka!.
  3. Baadhi ya Issues Zinashughulikiwa na Wizara Tofauti, Sheria Tofauti, Zitaleta Mkanganyiko Mbeleni. Ziko issues ambazo ni the same issues, zinashughulikiwa na wizara mbili tofauti kwa sheria mbili tofauti!. Mfano mzuri ni masuala ya habari, yanashughulikiwa na wizara ya habari na idara ya Maelezo kwa sheria ya habari, lakini vyombo vya utangazaji, redio, TV na online zinashughulikia na sheria ya utangazaji iliyoko chini ya TCRA ambayo iko chini ya wizara ya ujenzi!. Mbele ya safari kutakuja kutokea fumua fumua na suka suka upya ya wizara hizi!.
  4. Maofisa Kuwekwa Pembeni Kusubiri Kupangiwa Kazi Nyingine. Mfano wanaposikia maofisa wakuu fulani wa umma, wamesimamishwa kazi, na kuteuliwa wengine kukaimu nafasi zao!. Hatua hii kisiasa ni nzuri, maana ina mpa kick Magufuli kwa ku boost political mileage yake, na hivi ndivyo wafanyavyo ma populist leaders dunia nzima, boosting their political mileage tuu ila kiuchumi inatuumiza na kuliumiza taifa!. Magufuli analibebesha taifa hili mzigo mkubwa wa gharama kuliko hata serikali ya JK!. Kwa mujibu wa sheria za kazi, kila mtumishi aliyesimamishwa kazi kwa tuhuma zozote zile, anaendelea kulipwa mshahara wake wote ule ule kamili, bali marupurupu ndio yanaondolewa!. Mtumishi atalipwa nusu ya mshahara iwapo tuu atasimamishwa kazi na kushitakiwa, na mtumishi hatalipwa kabisa mshahara iwapo atafukuzwa kazi!. Tangu rais Magufuli aanze hii timua tumua, hakuna ofisa mkuu yoyote aliyefukuzwa kazi, wala aliyeshitakiwa, wote wamesimamishwa tuu kazi na kusubiri kupangiwa kazi nyingine!, au wengine teuzi zao zimetenguliwa huku wote wakiendelea kulipwa mishahara yao ile ile!.
  5. Makatibu Wakuu Wanaolipwa Bila Kazi!. Hata upande wa uteuzi wa Makatibu Wakuu, wale Makatibu Wakuu wote ambao Ukatibu wao Mkuu haukutenguliwa, au wameachwa tuu bila kupangiwa kazi nyingine yoyote, wote wanaendelea kulipwa mishahara yao ya makatibu wakuu kusubiria ama kupangiwa kazi nyingine, ama kustaafu kwa umri, au kustaafishwa kwa manufaa ya umma, lakini wakati huu wote wanaosubiria, walalipwa na kupatiwa haki na stahiki zote za level ya Katibu Mkuu!.
  6. Ununuzi wa Ndege za Bombadier Kwa Cash Kutaligharimu Taifa. Huu uamuzi wa kununua ndege ni uamuzi mzuri, lakini kununua kwa cash money badala ya hire purchase, is a wrong thing, done at the right time in a wrong way. Lengo la kununua kwa hire purchase. Inchi zinanunua kwa hire purchasepurchase kuweka bima ya performance na delivery at the place of performance, kununua kwa cash kama kununua mkate, kunafanya ndege hizo kuwa zimenunuliwa kwa direct shopping, toka Point of Sale (POS) hivyo ndege hizo kuwa zetu kule kule dukani, zikija kuwa mbovu, au zikipata ajali njiani kabla hazijafika kwa mteja, inakula kwetu!. Haya ni manunuzi kama FOB badala ya CIF, hivyo sales imefanyikia kwa muuzaji na makabidhiano ni baada ya kulipa cash, kama kununua mkate!, tulipaswa kutumia CIF, ili muuzaji azilete ndege, azitest kujiridhisha zinaweza kazi ndipo tukabidhiwe!. Madhara tutayaona ndege zikituharibikia, hatuna bima, tumeishanunua, inakula kwetu!. Ushauri: Tuendelee kununua ndege lakini not by cash. Tutumie hire purchase ili tufaidike na performance guarantee.
  7. Ununuzi wa Midege Mingi Mikubwa Bila Mpango Kazi ni Hasara na Majanga. Rais Magufuli amedhamiria kununua midege mikubwa na mingi, bila kufanya utafiti wa needs and assessment na bila mpango kazi!. Ndege hizi zinanunuliwa kwa mtindo wa kupiga tanchi. Hii maana yake ni Tanzania hatujawa na business plan, hivyo kwa shirika lenye nothing to something big without plans kuna risks za under utilisation. Ndege kubwa zinatakiwa kwenda masafa marefu, ATC yetu hapo tuu ilipo, bado haijaweza kuicover Tanzania on local routes, halafu tuje kwenye regional routes za EAC, tuje kwenye African routes ndipo twende Ulaya, Asia na America. Sasa kuleta hiyo midege mikubwa ya masafa marefu kuzirusha domestic routes ni kuzitesa bure na matokeo yake ni zitajiendesha kwa hasara na huge operation cost, matokeo yake ni kuendelea kuiendesha ATCL kwa kuibeba kwa mbeleko ya serikali ya Magufuli. Kwavile marais wanakuja na kupita, atakapokuja rais mwingine asiye na moyo wa uzalendo mshumaa, wa kurusha midege kwa pride ya national carrier huku inatuumiza Kiuchumi, mwisho wa siku serikali ikashindwa kuendelea kuumia, italibwaga chini hilo zigo la ATCL, hivyo kuwa hasara juu ya hasara. Ushauri: Tununue kidogo kidogo according to demand, tusije kununua ma white elephants ya midege!.
  8. Kushadadia Ujenzi wa Reli ya SGR, Wakati Tumeshindwa Kutumia TAZARA Ni uamuzi mzuri, done at the wrong time, bud done rightly. Kwa vile tayari tuna meter gauge railways, Reli ya Kati, na TAZARA tumeshindwa kuzi utilize, to their full capacity, tunaitumia below the capacity, the right thing to do, ilikuwa ni kuimarisha reli ya kati na TAZARA kuitumia to its full capacity tukiona tuna traffic kubwa ya mizigo ya kutosha ndipo tuanze na SGR. Kama hii iliyopo haina mzigo wa kutosha, kujenga SGR kwa uharaka huu alongside reli ile ile ndogo ni kujenga a huge, big white elephant project!. Ushauri: Tuimarishe kwanza a meter gauge na Tazara, we utilize them at full capacity ndipo tuje SGR.
  9. Tanzania ya Viwanda Bila Blue Print . Rais Magufuli ameamua kuibadili nchi yetu na kuijenga Tanzania ya Viwanda. Tanzania ya Viwanda haiwezi kujengwa kwa kauli ya “Tunajenga Tanzania ya Viwanda”. Tanzania ya viwanda vya ukweli, itajengwa kwa strategies na sio kwa kauli. Huwezi kujenga Tanzania ya Viwanda bila Blue Prints na SMART Objectives, Ni Maneno Mengi, Viendo Vichache. Hivyo hata ukimteua malaika mwenyewe kabisa kutoka mbinguni kuja kuongoza wizara ya Viwanda ili kujenga Tanzania ya Viwanda bila ya blue print yoyote, utaishia kumtumbua!. Ushauri: Tulete a blue print ya viwanda gani, kuzalisha bidhaa gani kwa malighafi gani, technology gani, kwa mitaji gani na nguvu kazi gani, na kwa masoko gani.
Hitimisho
Hivyo baadhi ya hatua zinazochukuliwa na rais wetu Dr. John Pombe Magufuli, japo ni hatua nzuri, na zimefanywa kwa nia njema kabisa, zikiachwa tuu hivi hivi jinsi hii hii inavyo fanyika, zitaligharimu sana taifa hili!, ni bora rais Magufuli angefuata ule mtindo wa Nyerere, ilikuwa hakuna kusimamisha kazi, ilikuwa ni kufukuza tuu au kustaafisha kwa manufaa ya umma!. Anapounda baraza jipya na kuteua makatibu wakuu wapya, wale wote walioachwa, walipaswa kustaafishwa there and then na mishahara yao inasimamishwa kuanzia pale pale walipostaafishwa!.

Hili ninalolisema leo, wengine mtakuja kuliona mwezi Juni /July wakati wa kusomwa kwa bajeti kuu ya serikali, mtashuhudia kuongezeka kwa bajeti ya uendeshaji wa serikali ikiwemo wage bill badala ya kupungua na mbele ya safari mtashuhudia mabadiliko mengi ya baraza za mawaziri au kwa kuwaongeza, au kuzipunguza vizara alizoziunganisha kwa kuziachanisha!. Na kila siku mawaziri watateuliwa na kutumbuliwa kama kubadili nguo, kwa sababu Magufuli huyu ambaye sasa ndie rais wetu, ni Magufuli huyu huyu niliyemzungumza hapa

Happy New Year
Paskali.
Rejea
Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!.

Jee Maendeleo ya Kweli ni Maendeleo ya Watu au Vitu?- Wachumi Tusaidieni, Magufuli Analisaidia Taifa au Ataliangamiza?.

Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike!

P
 
pasco at least ungequantify hiyo hasara/gharama kuliko kuongea maneno matupu...sahihisho,mtumishi wa umma akisimamishwa anaendelea kupokea mshahara kamili hadi shauri lake linapoamriwa...pasco uwe unapitia nyaraka mpya za serikali
 
Wanabodi,
Kuna watu wanashangilia sana kila kinachofanywa na Magufuli, wakidhani ndio the right thing!. Mfano alipoamua kuunda baraza dogo la mawaziri, na kuongeza idadi ya makatibu wakuu, badala ya kupunguza gharama, kutaongeza ghara za uendeshaji!, serikali ni makaribu wakuu ambao ndio waendeshaji, na sio mawaziri!.

Mfanowanaposikia maofisa wakuu fulani wa umma, wamesimamishwa kazi, na kuteuliwa wengine kukaimu nafasi zao!. Hatua hii kisiasa ni nzuri, maana ina mpa kick Magufuli kwa boost political mileage yake, ila kiuchumi, Magufuli analibebesha taifa hili mzigo kubwa kuliko hata serikali ya JK!.

Kwa mujibu wa sheria za kazi, kila mtumishi aliyesimamishwa kazi kwa tuhuma zozote, anaendelea kulipwa mshahara wake kamili, bali maupurupu ndio yanaondolewa!.

Mtumishi atalipwa nusu ya mshahara iwapo atasimamishwa kazi na kushitakiwa, na mtumishi hatalipwa lipwa mshahara iwapo atafukuzwa kazi!.

Tangu Magufuli aanze hii timua tumua, hakuna ofisa mkuu yoyote aliyefukuzwa, wala aliyeshitakiwa, wate wamesimamishwa tuu kusubiri kupangiwa kazi nyingine!, wote wanaendelea kulipwa mishahara yao ile ile!.

Hata upande wa uteuzi wa Makatibu Wakuu, wale makatibu wakuu wote ambao ukatibu wao mkuu haukutenguliwa, wanaendelea kulipwa mishahara ya makatibu wakuu kusubiri kupangiwa kazi nyingine!.

Hivyo baadhi ya hatua zinazochukuliwa na rrais wetu John Pombe Magufuli, japo ni hatua nzuri, na zimefanywa kwa nia njema, zitaligharimu sana taifa hili!, ni bora Magufuli angefuata ule mtindo wa Nyerere, ilikuwa hakuna kusimamisha kazi, ilikuwa ni kufukuza tuu!. Anapounda baraza jipya na kutea makatibu wakuu wapya, wale wote walioachwa, walikuwa wanastaafishwa kwa manifaa ya umma na mishahara yao inasimamishwa kuanzia hapo!.
Happy New Year
Pasco
Pasco
Pasco aka Mwanaukawa damu unadhani Mzee wa kubana matumizi (magu) hajaliona hilo? Baada ya mwezi fuatilia hao waliosimamishwa watakuwa wapi halafu utapata jibu kama wanakula mishahara ya bure au bado wapo kwenye payroll.
 
Inawezekana kuna ukweli au si kweli. Hatupo ndani ya serikali kuhakikisha kama kweli kuna gharama za ziada au la!!yeye mwenyewe anayeendesha serikali anayajua haya na wasaidizi wake. Mi nafurahi tu wezi wa TRA na Bandarini wanaokamatwa na kushitakiwa, walikuwa miungu watu huku mitaani. Mtu anakuja na bag la hela na si mfanyabiashara, eti katoka tu kazini. Kweli wali walikuwa wanakufuru.
 
Pasco

Ukitaja kustaafishwa kwa manufaa ya umma inamaana hastahili kulipwa chochote, lakini wote hao ni watumishi wa umma watapangiwa kazi nyingine ref maswi.

Muhimu pia kujua idadi ya makatibu wakuu awamu ya 4 na hii awamu ya 5 ili mjadala uwe mzuri asante
 
Huwezi kulinganisha hasara itokanayo na mtuhumiwa kuendelea kubaki katika nafasi yake na huo mshahara usio na marupurupu ambao ataendelea kuupata kwa matakwa ya kisheria.
Halafu pia ni somo kwa wengine kuliko wangeachwa tu!
 
Wanabodi,
Kuna watu wanashangilia sana kila kinachofanywa na Magufuli, wakidhani ndio the right thing!. Mfano alipoamua kuunda baraza dogo la mawaziri, na kuongeza idadi ya makatibu wakuu, badala ya kupunguza gharama, kutaongeza ghara za uendeshaji!, serikali ni makaribu wakuu ambao ndio waendeshaji, na sio mawaziri!.

Mfanowanaposikia maofisa wakuu fulani wa umma, wamesimamishwa kazi, na kuteuliwa wengine kukaimu nafasi zao!. Hatua hii kisiasa ni nzuri, maana ina mpa kick Magufuli kwa boost political mileage yake, ila kiuchumi, Magufuli analibebesha taifa hili mzigo kubwa kuliko hata serikali ya JK!.

Kwa mujibu wa sheria za kazi, kila mtumishi aliyesimamishwa kazi kwa tuhuma zozote, anaendelea kulipwa mshahara wake kamili, bali maupurupu ndio yanaondolewa!.

Mtumishi atalipwa nusu ya mshahara iwapo atasimamishwa kazi na kushitakiwa, na mtumishi hatalipwa lipwa mshahara iwapo atafukuzwa kazi!.

Tangu Magufuli aanze hii timua tumua, hakuna ofisa mkuu yoyote aliyefukuzwa, wala aliyeshitakiwa, wate wamesimamishwa tuu kusubiri kupangiwa kazi nyingine!, wote wanaendelea kulipwa mishahara yao ile ile!.

Hata upande wa uteuzi wa Makatibu Wakuu, wale makatibu wakuu wote ambao ukatibu wao mkuu haukutenguliwa, wanaendelea kulipwa mishahara ya makatibu wakuu kusubiri kupangiwa kazi nyingine!.

Hivyo baadhi ya hatua zinazochukuliwa na rrais wetu John Pombe Magufuli, japo ni hatua nzuri, na zimefanywa kwa nia njema, zitaligharimu sana taifa hili!, ni bora Magufuli angefuata ule mtindo wa Nyerere, ilikuwa hakuna kusimamisha kazi, ilikuwa ni kufukuza tuu!. Anapounda baraza jipya na kutea makatibu wakuu wapya, wale wote walioachwa, walikuwa wanastaafishwa kwa manifaa ya umma na mishahara yao inasimamishwa kuanzia hapo!.
Happy New Year
Pasco
Pasco

Tunatambua hayo yote lkn ndiyo Raisi wetu na huko kote tumeshatoka na mpaka leo hii hakuna tulichopata hivyo kwa kuwa hii ni aina nyingine ya Utawala wacha pia tuijaribu mahesabu yatakuja huko 2020, kwa sasa hivi tuko nyuma yake kwa kila analofanya na ndiyo maana ya kufanya Uchaguzi, au wewe labda ulifikiri kwa nini nchi huwa zinafanya uchaguzi na kuchagua Kiongozi wa kuwaongoza kwa kipindi cha waliojiwekea? Ulifikiri nchi huchagua Kiongozi ili zianze kumpinga baada ya mwezi mmoja?

Raisi Magufuli mpaka sasa hivi yuko vizuri sana na hata wataalamu wa mambo ya siasa na Uchumi wa kiulimwengu na siyo TZ na Afrika tu wanasema kwamba kama akiendelea hivi hivi basi nchi yetu itatoka hapa ilipo na kwenda mahali pengine bora zaidi, sasa wewe ni nani hata upingane na wataalamu ambao walizitabiria nchi kama Singapore, Taiwani, Korea Kusini na leo hii wako sahihi?

Kwa kukusadia tu mimi rafiki yangu ni mmoja wa wahanga wa kubomolewa nyumba na Halmashauri ingawaje ana huzuni sana lkn bado anasema raisi Magufuli ndiye Raisi tuliyekuwa tunamngojea kwa muda mrefu sana na kwamba amekubali utendeji wake!
 
Ukawa wanajitahidi kutafuta 'nitoke vipi'

Kama alivyosema mdau hapo juu ungeweka mchanganuo wa gharama tungekuelewa ...kwa kuwa wazee wa vibahasha hamna uwezo huo tutakusamehe.

labda nikuulize je hao wazembe waliowekwa pembeni unajua wamesababishia taifa hasara ya kiasi gani?

Huwezi kuendelea kuogopa hasara kwa kuendekeza hasara!!THINK
 
@Pasco: mimi hupenda kusoma hoja zako lakini 100% umechemsha kwa sababu mbili kuu:

1) hujabainisha kwa takwimu hiyo hasara.
2) hao unaowataja wanatuhumiwa kuliingizia hasara kubwa Taifa, kama watagundulika wana makosa (haki yao kusikilizwa), haki itandeka. Lakini kwa sasa wakae nje wakisubiri hukumu na wakati huohuo taifa likiokoa pesa lukuki kama watakuwa nje ya uongozi.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Tunatambua hayo yote lkn ndiyo Raisi wetu na huko kote tumeshatoka na mpaka leo hii hakuna tulichopata hivyo kwa kuwa hii ni aina nyingine ya Utawala wacha pia tuijaribu mahesabu yatakuja huko 2020, kwa sasa hivi tuko nyuma yake kwa kila analofanya na ndiyo maana ya kufanya Uchaguzi, au wewe labda ulifikiri kwa nini nchi huwa zinafanya uchaguzi na kuchagua Kiongozi wa kuwaongoza kwa kipindi cha waliojiwekea? Ulifikiri nchi huchagua Kiongozi ili zianze kumpinga baada ya mwezi mmoja?

Raisi Magufuli mpaka sasa hivi yuko vizuri sana na hata wataalamu wa mambo ya siasa na Uchumi wa kiulimwengu na siyo TZ na Afrika tu wanasema kwamba kama akiendelea hivi hivi basi nchi yetu itatoka hapa ilipo na kwenda mahali pengine bora zaidi, sasa wewe ni nani hata upingane na wataalamu ambao walizitabiria nchi kama Singapore, Taiwani, Korea Kusini na leo hii wako sahihi?

Kwa kukusadia tu mimi rafiki yangu ni mmoja wa wahanga wa kubomolewa nyumba na Halmashauri ingawaje ana huzuni sana lkn bado anasema raisi Magufuli ndiye Raisi tuliyekuwa tunamgojea kwa muda mrefu sana na kwamba amekubali utendeji wake!
 
Pasco ipi gharama kubwa, kumlipa mshahara kila mwezi mfanyakazi aliyesimamishwa kazi au kumwacha huyo mfanyakazi aendelee kuiingizia serikali hasara (mamilioni hadi mabilioni kila mwezi) kwa utendaji mbovu?
Kama umemuelewa vema Pasco, anamaanisha kwamba heri kuwastaafisha/kuwatimua moja kwa moja kwa moja kuliko kuwasimamisha. Ukimsimamisha bado anapokea mshahara, ila ukimtimua hakuna mshahara atakaopokea. Kwahiyo kapendekeza bora watimuliwe moja kwa moja kuliko kusimamishwa.
 
Wanabodi,
Kuna watu wanashangilia sana kila kinachofanywa na Magufuli, wakidhani ndio the right thing!. Mfano alipoamua kuunda baraza dogo la mawaziri, na kuongeza idadi ya makatibu wakuu, badala ya kupunguza gharama, kutaongeza ghara za uendeshaji!, serikali ni makaribu wakuu ambao ndio waendeshaji, na sio mawaziri!.

Mfanowanaposikia maofisa wakuu fulani wa umma, wamesimamishwa kazi, na kuteuliwa wengine kukaimu nafasi zao!. Hatua hii kisiasa ni nzuri, maana ina mpa kick Magufuli kwa boost political mileage yake, ila kiuchumi, Magufuli analibebesha taifa hili mzigo kubwa kuliko hata serikali ya JK!.

Kwa mujibu wa sheria za kazi, kila mtumishi aliyesimamishwa kazi kwa tuhuma zozote, anaendelea kulipwa mshahara wake kamili, bali maupurupu ndio yanaondolewa!.

Mtumishi atalipwa nusu ya mshahara iwapo atasimamishwa kazi na kushitakiwa, na mtumishi hatalipwa lipwa mshahara iwapo atafukuzwa kazi!.

Tangu Magufuli aanze hii timua tumua, hakuna ofisa mkuu yoyote aliyefukuzwa, wala aliyeshitakiwa, wate wamesimamishwa tuu kusubiri kupangiwa kazi nyingine!, wote wanaendelea kulipwa mishahara yao ile ile!.

Hata upande wa uteuzi wa Makatibu Wakuu, wale makatibu wakuu wote ambao ukatibu wao mkuu haukutenguliwa, wanaendelea kulipwa mishahara ya makatibu wakuu kusubiri kupangiwa kazi nyingine!.

Hivyo baadhi ya hatua zinazochukuliwa na rrais wetu John Pombe Magufuli, japo ni hatua nzuri, na zimefanywa kwa nia njema, zitaligharimu sana taifa hili!, ni bora Magufuli angefuata ule mtindo wa Nyerere, ilikuwa hakuna kusimamisha kazi, ilikuwa ni kufukuza tuu!. Anapounda baraza jipya na kutea makatibu wakuu wapya, wale wote walioachwa, walikuwa wanastaafishwa kwa manifaa ya umma na mishahara yao inasimamishwa kuanzia hapo!.
Happy New Year
Pasco
Pasco

Ongea kwa takwimu; tupe cost benefit analysis; sio kutubandikia blanket assesment zako; ambazo kimsingi zinareflect a gist of your own imaginations! Kumbuka "Every revolution has its own sacrifices! And the ends justify the means; kama upuuzi wa JK umetufikisha tulipo bora na JPM apewe muda ajaribu njia mbadala!
 
Ukawa wanajitahidi kutafuta 'nitoke vipi'

Kama alivyosema mdau hapo juu ungeweka mchanganuo wa gharama tungekuelewa ...kwa kuwa wazee wa vibahasha hamna uwezo huo tutakusamehe.

labda nikuulize je hao wazembe waliowekwa pembeni unajua wamesababishia taifa hasara ya kiasi gani?

Huwezi kuendelea kuogopa hasara kwa kuendekeza hasara!!THINK
Hujamuelewa mleta mada, yeye anasema kwanini wasitimuliwe moja kwa moja kuliko kusimamishwa? Mtu akisimamishwa bado pesa anapokea yaani mshahara wake upo palepale. Ni kweli Magufuli kafanya jambo la maana ila watu wahujumu uchumi kama hawa walipaswa kutimuliwa moja kwa moja na kushtakiwa.
 
Back
Top Bottom