CreativityCode
Senior Member
- Aug 8, 2020
- 158
- 653
Huyu mgombea ambaye ndiye Rais amalizaye muda wake na anaomba tena watanzania wampe tena miaka mingine 5 ili aendeleze kipaumbele chake kwenye kununua ndege, kujenga madaraja, kujenga reli, kujenga viwanja vya ndege na yanayofanana na hayo.
Lakini hebu tujiulize ameyafanya hayo miaka yote 5, Je! Mtanzania wa kawaida anayependa kumuita mnyonge amenufaika na nini? zaidi ya kushuhudia ugumu wa maisha kila kukicha?
Rais ambaye unapotaja maendeleo yeye akilini mwake huja flyover, madaraja, reli na midege huyu hatufai.
Rais amabye unapotaja kuboresha afya yeye akilini mwake huja majengo anayoyaita hospitali bila kuangalia soft elements ambazo ndiyo muhimu mfano idadi ya madaktari wanaolipwa vizuri, madawa na vifaa vya matibabu.
Nawakumbusha watanzania kuwa kwa sasa hakuna nchi yenye miundombinu ya kustaajabisha mfano wa flyovers, madaraja, reli duniani kama China lakini raia wake kila kukicha wanazamia kuja Ulaya, kila siku wanakamatwa kwenye makontena. Ukiwauliza tatizo nini ukiwa unafahamu kuwa China ni nchi tajiri kimiundombinu, watakwambia wanahitaji maisha bora na uhuru.
Sasa huyu kila siku yeye anasema anataka kuifanya Tanzania iwe kama Ulaya sijui anajua China iko Ulaya? ni bora angekuwa anasema anataka kuifanya Tanzania kuwa kama China (kitu amabacho nacho hawezi) tungekubaliana naye lakini kwa ubora wa maisha amekwishafeli.
NI WAKATI SASA WANANCHI KUCHAGUA IKIWA MNATAKA RAIS AMBAYE ATAJENGA MIUNDOMBINU AKIBORESHA MAISHA YENU PIA, AU RAIS AMBAYE KWAKE YEYE MAENDELEO NI MIUNDOMBINU PEKEE BILA KUBORESHA MAISHA HALISI YA MWANANCHI NA KUMPATIA UHURU WAKE.
Ni wakati wa kuchagua Tundu Lissu ili ujengewe miundombinu huku maisha yako na uhuru vikiboreshwa ama John Magufuli ambaye tafsiri ya maendeleo kwake yeye ni ujenzi pekee huku akiminya haki za binadamu na kufuta uhuru wa kujieleza.
Jioni njema