Mnataka Rais Samia awe mkali na mbabe, kwani anaongoza mbuzi?

Ni wapuuzi kabisa! Pale uchumi utakapodhoofika kwa ufisadi,usimamizi mbaya wa rasilimali,ubadhirifu,ujangili na uzembe ndipo watakapopata akili! Baadhi ya watanzania wanadhani hii nchi ni kama Sweden,Uholanzi n.k kumbe hawajui bado ni nchi masikini inahitaji usimamizi mkubwa!

Uchumi udhoofike mara ngapi Boss??
 
Matumizi ya nguvu Ili kulazimishwa kufuata Sheria ni matokeo ya madhara ya watoto kupigwa viboko watoto uoga viboko na sio utii.Jiwe alikuwa anaogopwa na sio kuheshimiwa
 
Watu wanafikiri kiongozi ni mpaka ubweke kama mbwa. Waende huko shimoni aliko wakabwekewe. Watuachie Rais wetu SSH
 
Ambao hawakuwahi kufungiwa viwanda na biashara zao kwa kuwa waaminifu wa kulipa kodi miaka yote mpaka tukaingia uchumi wa kati wanajisikiaje??

Anayelipa kodi na asiyelipa kodi wanaweza kushindana sokoni??

Namhurumia sana Mwigulu Nchemba amepewa target ya Trillion 2 kwa mwezi.

Lakini Sasa hivi kutoa receipt ya EFD machine imeanza kuonekana ni ulofa.
Waziri wa fedha kazi anayo.
Inajengwa picha ya kwamba biashara zilizofungwa ni nyingi sana kuliko ambazo hazikufungwa
 
Lini uchumi ulidhoofika? Kutoka nchi masikini hadi uchumi wa kati daraja la chini sio kukua kwa uchumi?
Data za kupikwa zile na walipingana na JK hadharani kabisa. Sasa hivi umaskini ndiyo umeshika kasi kuliko awamu zote na kuna bado mikoa inaongoza kwa umaskini
 
Data za kupikwa zile na walipingana na JK hadharani kabisa. Sasa hivi umaskini ndiyo umeshika kasi kuliko awamu zote na kuna bado mikoa inaongoza kwa umaskini
Akili yako itakuwa na shida kidogo.Kwa hiyo Bank kuu ya Tanzania,Maprofesa wote wa Tanzania,IMF,World Bank,Aljazeera,BBC na taasisi nyingine kubwa ulimwengu walishirikiana kupika data? Au unaishi ulimwengu upi ambao ukweli ni mgumu kiasi hicho kupatikana? Hata google pia hauna?
 
Hakika fasihi imetulia. Kongole kwako.

Hao wanaotaka Mama aongoze kwa ukali, wajiundie ka-jamhuri kao cha wendawazimu. Kwa sasa mawazo yao hayana nafasi, yamekwenda na mwendazake.

Wastaarabu huongozwa kistaarabu, waungwana huongozwa kiungwana. Lakini pia nadhani washenzi huongozwa kishenzi; na watumwa huongozwa kitumwa.

Sisi ni jamii ya waungwana. Tunataka kuongozwa kiungwana. Hatutaki kufokewa-fokewa, kusimangwa-simangwa (tena kusimangiwa vyetu), tunahitaji kujadiliana na kuafikiana.

HIYO NDIO TANZANIA TUNAYOITAKA.
HAKI HUINUA TAIFA
 
Akili yako itakuwa na shida kidogo.Kwa hiyo Bank kuu ya Tanzania,Maprofesa wote wa Tanzania,IMF,World Bank,Aljazeera,BBC na taasisi nyingine kubwa ulimwengu walishirikiana kupika data? Au unaishi ulimwengu upi ambao ukweli ni mgumu kiasi hicho kupatikana? Hata google pia hauna?
Kwa maisha yapi ya uchumi wa kati? MATAGA mkatage huko mbali msituletee misifa ambayo haiendani na uhalisia wa uchumi.
 
Back
Top Bottom