Mnataka Rais Samia awe mkali na mbabe, kwani anaongoza mbuzi?

MNATAKA RAIS SAMIA AWE MKALI NA MBABE, MLIAMBIWA ANAONGOZA MBUZI?

Na, Robert Heriel

Kuna kundi la watu mtandaoni na mitaani wanapiga kelele na kumuona Rais Samia kuwa ni Mpole, wengine wanasema haongozi yeye bali anafuata maelekezo ya watu fulani. Kundi hilo linadai kuwa Mama Samia hafai kuwa Rais kwani kazidisha upole. Wao wanataka Rais mkali ambaye ndiye atawaongoza. Ni haki yao kutoa maoni yao vile waonavyo na jinsi wanavyofikiri kama vile na mimi nitakavyotoa maoni yangu hapa.

Kuna tofauti kubwa kati ya kuongoza watu na kuongoza Mbuzi. Hapa ndipo watu wanaposhindwa kuelewa.

Kuongoza mbuzi lazima uwe mwendawazimu kidogo kwa sababu mbuzi akili zao ni machepele. Wanakimbia kimbia huku na huku. Kuongoza Mbuzi lazima uwe mkali na uwe msema hovyo tena uwe na akiba ya matusi na sauti kubwa ya kuwakemea mbuzi. Kuongoza mbuzi lazima uwe na fimbo ya kuwachapa lakini kwa jinsi mbuzi ninavyowajua hata hiyo fimbo hutaweza kuwachapa kwani wanakimbia kimbia mno. Hivyo lazima uwe na fuko kubwa la mawe ambayo utawarushia hao mbuzi pale wanapoenda sehemu isiyo sahihi.

Kuongoa mbuzi hakuhitaji sheria wala katiba, kunahitaji utashi wa mchungaji. Yaani vile mchungaji atakavyoona ndivyo itavyokuwa.
Unaweza fungulia mbuzi saa nne asubuhi sawa, ukifungulia saa sita sawa, usipofungulia kabisa sawa, yaani mbuzi ni mbuzi tuu hata ukisema uwaletee majani hapohapo ni sawa tuu.

Mbuzi hata ukimpiga jiwe akavunjika mguu mbuzi wenzake wala hawatasema kitu, wataona ni sawa kabisa na ni haki yako kuwapiga kama sio kuwaua kabisa.

Rais anayeongoza watu wake kama Mbuzi, haoni ajabu kuwapiga watu wake, haoni shida kuwafunga kamba miguuni ili wasimkimbie, haoni shida kuwapiga mawe na kuwavunja miguu watu wake na kwa vile anawachukulia ni mbuzi hataki waseme wala wamlalamikie. Nao kwa vile ni mbuzi wanajiona ni halali yao kubondwa mawe, kufungwa kamba, na ikifika siku ya sikukuu kuchinjwa kama sio kuuzwa kwa bei nzuri au ya hasara.

Rais anayeongoza mbuzi lazima awe mkali kama kichaa, lazima awe msema hovyo na anayekimbia kimbia kukimbizana na mbuzi wasumbufu.

Sema kwenye uchungaji wa mbuzi kwa sisi tuliowahi kufuga, wale mbuzi wasumbufu ndio wanaoshiba vizuri na ndio wenye kuzaa sana kutokana na kushiba vizuri. Mbuzi hao ndio wenye akili. Kwani hawatosheki na malisho waliyopelekwa na bwana wao.

Hata kwenye nyumba, Baba anapokuwa mkali sana ni kwa sababu anawachukulia mke na watoto wake kama mbuzi wasio na akili.
Unakuwa mkali kupitiliza.

Ukali na ubabe vinatumika kwenye uchungi wa mbuzi hasa wale korofi ambao hawana akili za mwanadamu.

Rais Samia Suluhu anaongoza Watu, tena watu wenye akili zao.
Kuongoza watu hakuhitaji ukali na ubabe usio na maana, kunahitaji Hekima na busara.
Kuongoza watu kunahitaji katiba na sheria, sio utashi wa mtu jinsi aonavyo.
Kuongoza watu kunahitaji mfumo imara na sio mtu mmoja. Sio kama kuongoza mbuzi ambapo mtu mmoja anaweza kuongoza mbuzi hata elfu moja.

Kuongoza watu hakuhitaji kuropoka ropoka kama mwendawazimu.
Hakuhitaji kuwarushia watu mawe na kuwavunja miguu kama sio kuwachinja kabisa.

Kuongoza watu hakuhitaji kila kitu ufanye wewe bali unapaswa uwaachie wasaidizi wako nao wafanye.

Rais Samia anaongoza watu sio mbuzi.

Nafahamu familia zetu za kiafrika zimezoea na kulelewa kimbuzi mbuzi, unakuta Baba au Mama ni mkatili, mbabe na mshenzi kwa kisingizio cha malezi. Nafahamu familia za kiafrika wazazi wetu walikuwa na dhana kuwa Mtoto hana haki kwa sababu ni kama mbuzi tuu.
Huwezi ukalelewa kama mbuzi alafu ukawa na akili ya kibinadamu, huwezi ukalelewa kama mnyama alafu ukawa na utu.
Lazima nawe utakuwa na tabia za kinyama, ukatili na huna utu.

Sio ajabu kusikia mtu anampiga mke wake mpaka anamkata kata na mapanga. Sio ajabu kusikia mzazi anamchapa mtoto wake mpaka anamjeruhi. Ni kwa sababu halei mtu kwa utu, bali analea mtu kama mbuzi(mnyama)

Mnataka Mama awe mkali au mbabe kwani anaongoza mbuzi?

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Dar es salaam
Mimi mbuzi zangu za ilyamchele kijijini kule wala huwa sizifokei mbona na huwa si mkali kwazo
 
Sasa kuna tofaut gani kati ya mbuzi na watumishi wa tanesco wanaoharibu mtandao na wananchi kukosa huduma ya umeme kwa takribani siku 4?

Kuna tofaut gani kati ya mbuzi na watumish wa bandari wanaochezea mifumo ya kulipa na kusababisha mizigo kukwama kwa takribani siku 5?

Ukimchunguza mbuzi vzur bas utajua kabisa hana tofauti na mambo wanayofanya watu ambao bila kukaripiwa na kuongozwa kibabe...

Mbuzi sio mnyama bali mbuzi ni tabia..
 
Uwa unaweka namba za simu ili upigiwe na upewe uteuzi.Baada ya kujipendekeza kwa ,kuandika upupu.Nakushauri ,uendelee na kiajira chako hicho.Ukija huku utakufa mapema.Maana una majungu ya kipumbavu sana.
Katika hayo yote ina maana umeyaona hayo tu?
 
Vyovyote itakavyokuwa tanzania tumeshakuwa na maraisi wakali (nyerere, jpm), marasi wapole (mwinyi now samia+kikwete) na pia tumewahi kuwa na raisi mwenye sifa zote izo na mipango mingi (mkapa) na bado tulipigwa wote, tulikuwa duni, waliolalala njaa walikuwepo, waliouawa walikuwepo, na uchafu wote ulikuwepo. unachotakiwa kujua TZ ni kichwa cha mwendawazimu, kila anayekuja anakuja na mambo yake
 
Wanataka mama atuswage kama mbuzi mnadani - style ya mwendazake haikuwa ya kiuugwana kabisa!! na ndiyo maana tunasema ni lazima turekebishe Katiba yetu - unaweza akaja Rais akili na tabia zake haziko sawa akaivuruga nchi kabisa, tusiruhusu hili lifanyike kwa kuleta katiba mpya kupunguza mamlaka.

Mama piga kazi - watanzania wanataka utamaduni wa Upendo, kuheshimiana, kusaidiana kidugu, tofauti za kiitikadi zitumike kama utani na si vita, visasi na umwagaji damu kama ilivyo wakati wa mwendazake.
 
MNATAKA RAIS SAMIA AWE MKALI NA MBABE, MLIAMBIWA ANAONGOZA MBUZI?

Na, Robert Heriel

Kuna kundi la watu mtandaoni na mitaani wanapiga kelele na kumuona Rais Samia kuwa ni Mpole, wengine wanasema haongozi yeye bali anafuata maelekezo ya watu fulani. Kundi hilo linadai kuwa Mama Samia hafai kuwa Rais kwani kazidisha upole. Wao wanataka Rais mkali ambaye ndiye atawaongoza. Ni haki yao kutoa maoni yao vile waonavyo na jinsi wanavyofikiri kama vile na mimi nitakavyotoa maoni yangu hapa.

Kuna tofauti kubwa kati ya kuongoza watu na kuongoza Mbuzi. Hapa ndipo watu wanaposhindwa kuelewa.

Kuongoza mbuzi lazima uwe mwendawazimu kidogo kwa sababu mbuzi akili zao ni machepele. Wanakimbia kimbia huku na huku. Kuongoza Mbuzi lazima uwe mkali na uwe msema hovyo tena uwe na akiba ya matusi na sauti kubwa ya kuwakemea mbuzi. Kuongoza mbuzi lazima uwe na fimbo ya kuwachapa lakini kwa jinsi mbuzi ninavyowajua hata hiyo fimbo hutaweza kuwachapa kwani wanakimbia kimbia mno. Hivyo lazima uwe na fuko kubwa la mawe ambayo utawarushia hao mbuzi pale wanapoenda sehemu isiyo sahihi.

Kuongoa mbuzi hakuhitaji sheria wala katiba, kunahitaji utashi wa mchungaji. Yaani vile mchungaji atakavyoona ndivyo itavyokuwa.
Unaweza fungulia mbuzi saa nne asubuhi sawa, ukifungulia saa sita sawa, usipofungulia kabisa sawa, yaani mbuzi ni mbuzi tuu hata ukisema uwaletee majani hapohapo ni sawa tuu.

Mbuzi hata ukimpiga jiwe akavunjika mguu mbuzi wenzake wala hawatasema kitu, wataona ni sawa kabisa na ni haki yako kuwapiga kama sio kuwaua kabisa.

Rais anayeongoza watu wake kama Mbuzi, haoni ajabu kuwapiga watu wake, haoni shida kuwafunga kamba miguuni ili wasimkimbie, haoni shida kuwapiga mawe na kuwavunja miguu watu wake na kwa vile anawachukulia ni mbuzi hataki waseme wala wamlalamikie. Nao kwa vile ni mbuzi wanajiona ni halali yao kubondwa mawe, kufungwa kamba, na ikifika siku ya sikukuu kuchinjwa kama sio kuuzwa kwa bei nzuri au ya hasara.

Rais anayeongoza mbuzi lazima awe mkali kama kichaa, lazima awe msema hovyo na anayekimbia kimbia kukimbizana na mbuzi wasumbufu.

Sema kwenye uchungaji wa mbuzi kwa sisi tuliowahi kufuga, wale mbuzi wasumbufu ndio wanaoshiba vizuri na ndio wenye kuzaa sana kutokana na kushiba vizuri. Mbuzi hao ndio wenye akili. Kwani hawatosheki na malisho waliyopelekwa na bwana wao.

Hata kwenye nyumba, Baba anapokuwa mkali sana ni kwa sababu anawachukulia mke na watoto wake kama mbuzi wasio na akili.
Unakuwa mkali kupitiliza.

Ukali na ubabe vinatumika kwenye uchungi wa mbuzi hasa wale korofi ambao hawana akili za mwanadamu.

Rais Samia Suluhu anaongoza Watu, tena watu wenye akili zao.
Kuongoza watu hakuhitaji ukali na ubabe usio na maana, kunahitaji Hekima na busara.
Kuongoza watu kunahitaji katiba na sheria, sio utashi wa mtu jinsi aonavyo.
Kuongoza watu kunahitaji mfumo imara na sio mtu mmoja. Sio kama kuongoza mbuzi ambapo mtu mmoja anaweza kuongoza mbuzi hata elfu moja.

Kuongoza watu hakuhitaji kuropoka ropoka kama mwendawazimu.
Hakuhitaji kuwarushia watu mawe na kuwavunja miguu kama sio kuwachinja kabisa.

Kuongoza watu hakuhitaji kila kitu ufanye wewe bali unapaswa uwaachie wasaidizi wako nao wafanye.

Rais Samia anaongoza watu sio mbuzi.

Nafahamu familia zetu za kiafrika zimezoea na kulelewa kimbuzi mbuzi, unakuta Baba au Mama ni mkatili, mbabe na mshenzi kwa kisingizio cha malezi. Nafahamu familia za kiafrika wazazi wetu walikuwa na dhana kuwa Mtoto hana haki kwa sababu ni kama mbuzi tuu.
Huwezi ukalelewa kama mbuzi alafu ukawa na akili ya kibinadamu, huwezi ukalelewa kama mnyama alafu ukawa na utu.
Lazima nawe utakuwa na tabia za kinyama, ukatili na huna utu.

Sio ajabu kusikia mtu anampiga mke wake mpaka anamkata kata na mapanga. Sio ajabu kusikia mzazi anamchapa mtoto wake mpaka anamjeruhi. Ni kwa sababu halei mtu kwa utu, bali analea mtu kama mbuzi(mnyama)

Mnataka Mama awe mkali au mbabe kwani anaongoza mbuzi?

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Dar es salaam
Hii ni insha (essay) kiwango cha shule ya upili. Mlinganisho wa nchi na mbuzi unaanzia wapi? Nchi ina systems ambazo hata ziwe bora vipi bila usimamizi madhubuti hufeli.
 
Vyovyote itakavyokuwa tanzania tumeshakuwa na maraisi wakali (nyerere, jpm), marasi wapole (mwinyi now samia+kikwete) na pia tumewahi kuwa na raisi mwenye sifa zote izo na mipango mingi (mkapa) na bado tulipigwa wote, tulikuwa duni, waliolalala njaa walikuwepo, waliouawa walikuwepo, na uchafu wote ulikuwepo. unachotakiwa kujua TZ ni kichwa cha mwendawazimu, kila anayekuja anakuja na mambo yake
Ila Mkapa alikuwa Raisi bora kabisa hapa Tanzania
 
"Mathepele"; hiyo kali.
Lakini tuseme hivi. Hakuna sera ya upole au ya ukali. Kila kitu kinategemea causes and conditions_ sababu na masharti au mazingara.
 
MNATAKA RAIS SAMIA AWE MKALI NA MBABE, MLIAMBIWA ANAONGOZA MBUZI?

Na, Robert Heriel

Kuna kundi la watu mtandaoni na mitaani wanapiga kelele na kumuona Rais Samia kuwa ni Mpole, wengine wanasema haongozi yeye bali anafuata maelekezo ya watu fulani. Kundi hilo linadai kuwa Mama Samia hafai kuwa Rais kwani kazidisha upole. Wao wanataka Rais mkali ambaye ndiye atawaongoza. Ni haki yao kutoa maoni yao vile waonavyo na jinsi wanavyofikiri kama vile na mimi nitakavyotoa maoni yangu hapa.

Kuna tofauti kubwa kati ya kuongoza watu na kuongoza Mbuzi. Hapa ndipo watu wanaposhindwa kuelewa.

Kuongoza mbuzi lazima uwe mwendawazimu kidogo kwa sababu mbuzi akili zao ni machepele. Wanakimbia kimbia huku na huku. Kuongoza Mbuzi lazima uwe mkali na uwe msema hovyo tena uwe na akiba ya matusi na sauti kubwa ya kuwakemea mbuzi. Kuongoza mbuzi lazima uwe na fimbo ya kuwachapa lakini kwa jinsi mbuzi ninavyowajua hata hiyo fimbo hutaweza kuwachapa kwani wanakimbia kimbia mno. Hivyo lazima uwe na fuko kubwa la mawe ambayo utawarushia hao mbuzi pale wanapoenda sehemu isiyo sahihi.

Kuongoa mbuzi hakuhitaji sheria wala katiba, kunahitaji utashi wa mchungaji. Yaani vile mchungaji atakavyoona ndivyo itavyokuwa.
Unaweza fungulia mbuzi saa nne asubuhi sawa, ukifungulia saa sita sawa, usipofungulia kabisa sawa, yaani mbuzi ni mbuzi tuu hata ukisema uwaletee majani hapohapo ni sawa tuu.

Mbuzi hata ukimpiga jiwe akavunjika mguu mbuzi wenzake wala hawatasema kitu, wataona ni sawa kabisa na ni haki yako kuwapiga kama sio kuwaua kabisa.

Rais anayeongoza watu wake kama Mbuzi, haoni ajabu kuwapiga watu wake, haoni shida kuwafunga kamba miguuni ili wasimkimbie, haoni shida kuwapiga mawe na kuwavunja miguu watu wake na kwa vile anawachukulia ni mbuzi hataki waseme wala wamlalamikie. Nao kwa vile ni mbuzi wanajiona ni halali yao kubondwa mawe, kufungwa kamba, na ikifika siku ya sikukuu kuchinjwa kama sio kuuzwa kwa bei nzuri au ya hasara.

Rais anayeongoza mbuzi lazima awe mkali kama kichaa, lazima awe msema hovyo na anayekimbia kimbia kukimbizana na mbuzi wasumbufu.

Sema kwenye uchungaji wa mbuzi kwa sisi tuliowahi kufuga, wale mbuzi wasumbufu ndio wanaoshiba vizuri na ndio wenye kuzaa sana kutokana na kushiba vizuri. Mbuzi hao ndio wenye akili. Kwani hawatosheki na malisho waliyopelekwa na bwana wao.

Hata kwenye nyumba, Baba anapokuwa mkali sana ni kwa sababu anawachukulia mke na watoto wake kama mbuzi wasio na akili.
Unakuwa mkali kupitiliza.

Ukali na ubabe vinatumika kwenye uchungi wa mbuzi hasa wale korofi ambao hawana akili za mwanadamu.

Rais Samia Suluhu anaongoza Watu, tena watu wenye akili zao.
Kuongoza watu hakuhitaji ukali na ubabe usio na maana, kunahitaji Hekima na busara.
Kuongoza watu kunahitaji katiba na sheria, sio utashi wa mtu jinsi aonavyo.
Kuongoza watu kunahitaji mfumo imara na sio mtu mmoja. Sio kama kuongoza mbuzi ambapo mtu mmoja anaweza kuongoza mbuzi hata elfu moja.

Kuongoza watu hakuhitaji kuropoka ropoka kama mwendawazimu.
Hakuhitaji kuwarushia watu mawe na kuwavunja miguu kama sio kuwachinja kabisa.

Kuongoza watu hakuhitaji kila kitu ufanye wewe bali unapaswa uwaachie wasaidizi wako nao wafanye.

Rais Samia anaongoza watu sio mbuzi.

Nafahamu familia zetu za kiafrika zimezoea na kulelewa kimbuzi mbuzi, unakuta Baba au Mama ni mkatili, mbabe na mshenzi kwa kisingizio cha malezi. Nafahamu familia za kiafrika wazazi wetu walikuwa na dhana kuwa Mtoto hana haki kwa sababu ni kama mbuzi tuu.
Huwezi ukalelewa kama mbuzi alafu ukawa na akili ya kibinadamu, huwezi ukalelewa kama mnyama alafu ukawa na utu.
Lazima nawe utakuwa na tabia za kinyama, ukatili na huna utu.

Sio ajabu kusikia mtu anampiga mke wake mpaka anamkata kata na mapanga. Sio ajabu kusikia mzazi anamchapa mtoto wake mpaka anamjeruhi. Ni kwa sababu halei mtu kwa utu, bali analea mtu kama mbuzi (mnyama).

Mnataka Mama awe mkali au mbabe kwani anaongoza mbuzi?

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Dar es salaam
Hakika fasihi imetulia. Kongole kwako.

Hao wanaotaka Mama aongoze kwa ukali, wajiundie ka-jamhuri kao cha wendawazimu. Kwa sasa mawazo yao hayana nafasi, yamekwenda na mwendazake.

Wastaarabu huongozwa kistaarabu, waungwana huongozwa kiungwana. Lakini pia nadhani washenzi huongozwa kishenzi; na watumwa huongozwa kitumwa.

Sisi ni jamii ya waungwana. Tunataka kuongozwa kiungwana. Hatutaki kufokewa-fokewa, kusimangwa-simangwa (tena kusimangiwa vyetu), tunahitaji kujadiliana na kuafikiana.

HIYO NDIO TANZANIA TUNAYOITAKA.
 
MNATAKA RAIS SAMIA AWE MKALI NA MBABE, MLIAMBIWA ANAONGOZA MBUZI?

Na, Robert Heriel

Kuna kundi la watu mtandaoni na mitaani wanapiga kelele na kumuona Rais Samia kuwa ni Mpole, wengine wanasema haongozi yeye bali anafuata maelekezo ya watu fulani. Kundi hilo linadai kuwa Mama Samia hafai kuwa Rais kwani kazidisha upole. Wao wanataka Rais mkali ambaye ndiye atawaongoza. Ni haki yao kutoa maoni yao vile waonavyo na jinsi wanavyofikiri kama vile na mimi nitakavyotoa maoni yangu hapa.

Kuna tofauti kubwa kati ya kuongoza watu na kuongoza Mbuzi. Hapa ndipo watu wanaposhindwa kuelewa.

Kuongoza mbuzi lazima uwe mwendawazimu kidogo kwa sababu mbuzi akili zao ni machepele. Wanakimbia kimbia huku na huku. Kuongoza Mbuzi lazima uwe mkali na uwe msema hovyo tena uwe na akiba ya matusi na sauti kubwa ya kuwakemea mbuzi. Kuongoza mbuzi lazima uwe na fimbo ya kuwachapa lakini kwa jinsi mbuzi ninavyowajua hata hiyo fimbo hutaweza kuwachapa kwani wanakimbia kimbia mno. Hivyo lazima uwe na fuko kubwa la mawe ambayo utawarushia hao mbuzi pale wanapoenda sehemu isiyo sahihi.

Kuongoa mbuzi hakuhitaji sheria wala katiba, kunahitaji utashi wa mchungaji. Yaani vile mchungaji atakavyoona ndivyo itavyokuwa.
Unaweza fungulia mbuzi saa nne asubuhi sawa, ukifungulia saa sita sawa, usipofungulia kabisa sawa, yaani mbuzi ni mbuzi tuu hata ukisema uwaletee majani hapohapo ni sawa tuu.

Mbuzi hata ukimpiga jiwe akavunjika mguu mbuzi wenzake wala hawatasema kitu, wataona ni sawa kabisa na ni haki yako kuwapiga kama sio kuwaua kabisa.

Rais anayeongoza watu wake kama Mbuzi, haoni ajabu kuwapiga watu wake, haoni shida kuwafunga kamba miguuni ili wasimkimbie, haoni shida kuwapiga mawe na kuwavunja miguu watu wake na kwa vile anawachukulia ni mbuzi hataki waseme wala wamlalamikie. Nao kwa vile ni mbuzi wanajiona ni halali yao kubondwa mawe, kufungwa kamba, na ikifika siku ya sikukuu kuchinjwa kama sio kuuzwa kwa bei nzuri au ya hasara.

Rais anayeongoza mbuzi lazima awe mkali kama kichaa, lazima awe msema hovyo na anayekimbia kimbia kukimbizana na mbuzi wasumbufu.

Sema kwenye uchungaji wa mbuzi kwa sisi tuliowahi kufuga, wale mbuzi wasumbufu ndio wanaoshiba vizuri na ndio wenye kuzaa sana kutokana na kushiba vizuri. Mbuzi hao ndio wenye akili. Kwani hawatosheki na malisho waliyopelekwa na bwana wao.

Hata kwenye nyumba, Baba anapokuwa mkali sana ni kwa sababu anawachukulia mke na watoto wake kama mbuzi wasio na akili.
Unakuwa mkali kupitiliza.

Ukali na ubabe vinatumika kwenye uchungi wa mbuzi hasa wale korofi ambao hawana akili za mwanadamu.

Rais Samia Suluhu anaongoza Watu, tena watu wenye akili zao.
Kuongoza watu hakuhitaji ukali na ubabe usio na maana, kunahitaji Hekima na busara.
Kuongoza watu kunahitaji katiba na sheria, sio utashi wa mtu jinsi aonavyo.
Kuongoza watu kunahitaji mfumo imara na sio mtu mmoja. Sio kama kuongoza mbuzi ambapo mtu mmoja anaweza kuongoza mbuzi hata elfu moja.

Kuongoza watu hakuhitaji kuropoka ropoka kama mwendawazimu.
Hakuhitaji kuwarushia watu mawe na kuwavunja miguu kama sio kuwachinja kabisa.

Kuongoza watu hakuhitaji kila kitu ufanye wewe bali unapaswa uwaachie wasaidizi wako nao wafanye.

Rais Samia anaongoza watu sio mbuzi.

Nafahamu familia zetu za kiafrika zimezoea na kulelewa kimbuzi mbuzi, unakuta Baba au Mama ni mkatili, mbabe na mshenzi kwa kisingizio cha malezi. Nafahamu familia za kiafrika wazazi wetu walikuwa na dhana kuwa Mtoto hana haki kwa sababu ni kama mbuzi tuu.
Huwezi ukalelewa kama mbuzi alafu ukawa na akili ya kibinadamu, huwezi ukalelewa kama mnyama alafu ukawa na utu.
Lazima nawe utakuwa na tabia za kinyama, ukatili na huna utu.

Sio ajabu kusikia mtu anampiga mke wake mpaka anamkata kata na mapanga. Sio ajabu kusikia mzazi anamchapa mtoto wake mpaka anamjeruhi. Ni kwa sababu halei mtu kwa utu, bali analea mtu kama mbuzi (mnyama).

Mnataka Mama awe mkali au mbabe kwani anaongoza mbuzi?

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Dar es salaam
Hata Mungu ni mkali acheni tanzania ilikua inaenda kubaya bila ukali wa JPM sijui hali ingekuaje kunawatu muda wote ni wahanga hata uwatendee vizuri kiasi gani... Acheni ujinga mtoto mjinga ukimlea kwa kumbembeleza ayakufanya wewe kuwa extension... Mda wote anakutegemea.. Ukali wa JPM umeamsha wengi walio kua wamelala.. Mama anaturudisha kulala usingizi muda wote ni mtamu... Na mwizi huiba wakati umelala.. Acheni uvictm mentality...
 
Back
Top Bottom