Mnataka Rais Samia awe mkali na mbabe, kwani anaongoza mbuzi?

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
3,385
2,000
MNATAKA RAIS SAMIA AWE MKALI NA MBABE, MLIAMBIWA ANAONGOZA MBUZI?

Na, Robert Heriel

Kuna kundi la watu mtandaoni na mitaani wanapiga kelele na kumuona Rais Samia kuwa ni Mpole, wengine wanasema haongozi yeye bali anafuata maelekezo ya watu fulani. Kundi hilo linadai kuwa Mama Samia hafai kuwa Rais kwani kazidisha upole. Wao wanataka Rais mkali ambaye ndiye atawaongoza. Ni haki yao kutoa maoni yao vile waonavyo na jinsi wanavyofikiri kama vile na mimi nitakavyotoa maoni yangu hapa.

Kuna tofauti kubwa kati ya kuongoza watu na kuongoza Mbuzi. Hapa ndipo watu wanaposhindwa kuelewa.

Kuongoza mbuzi lazima uwe mwendawazimu kidogo kwa sababu mbuzi akili zao ni machepele. Wanakimbia kimbia huku na huku. Kuongoza Mbuzi lazima uwe mkali na uwe msema hovyo tena uwe na akiba ya matusi na sauti kubwa ya kuwakemea mbuzi. Kuongoza mbuzi lazima uwe na fimbo ya kuwachapa lakini kwa jinsi mbuzi ninavyowajua hata hiyo fimbo hutaweza kuwachapa kwani wanakimbia kimbia mno. Hivyo lazima uwe na fuko kubwa la mawe ambayo utawarushia hao mbuzi pale wanapoenda sehemu isiyo sahihi.

Kuongoa mbuzi hakuhitaji sheria wala katiba, kunahitaji utashi wa mchungaji. Yaani vile mchungaji atakavyoona ndivyo itavyokuwa.
Unaweza fungulia mbuzi saa nne asubuhi sawa, ukifungulia saa sita sawa, usipofungulia kabisa sawa, yaani mbuzi ni mbuzi tuu hata ukisema uwaletee majani hapohapo ni sawa tuu.

Mbuzi hata ukimpiga jiwe akavunjika mguu mbuzi wenzake wala hawatasema kitu, wataona ni sawa kabisa na ni haki yako kuwapiga kama sio kuwaua kabisa.

Rais anayeongoza watu wake kama Mbuzi, haoni ajabu kuwapiga watu wake, haoni shida kuwafunga kamba miguuni ili wasimkimbie, haoni shida kuwapiga mawe na kuwavunja miguu watu wake na kwa vile anawachukulia ni mbuzi hataki waseme wala wamlalamikie. Nao kwa vile ni mbuzi wanajiona ni halali yao kubondwa mawe, kufungwa kamba, na ikifika siku ya sikukuu kuchinjwa kama sio kuuzwa kwa bei nzuri au ya hasara.

Rais anayeongoza mbuzi lazima awe mkali kama kichaa, lazima awe msema hovyo na anayekimbia kimbia kukimbizana na mbuzi wasumbufu.

Sema kwenye uchungaji wa mbuzi kwa sisi tuliowahi kufuga, wale mbuzi wasumbufu ndio wanaoshiba vizuri na ndio wenye kuzaa sana kutokana na kushiba vizuri. Mbuzi hao ndio wenye akili. Kwani hawatosheki na malisho waliyopelekwa na bwana wao.

Hata kwenye nyumba, Baba anapokuwa mkali sana ni kwa sababu anawachukulia mke na watoto wake kama mbuzi wasio na akili.
Unakuwa mkali kupitiliza.

Ukali na ubabe vinatumika kwenye uchungi wa mbuzi hasa wale korofi ambao hawana akili za mwanadamu.

Rais Samia Suluhu anaongoza Watu, tena watu wenye akili zao.
Kuongoza watu hakuhitaji ukali na ubabe usio na maana, kunahitaji Hekima na busara.
Kuongoza watu kunahitaji katiba na sheria, sio utashi wa mtu jinsi aonavyo.
Kuongoza watu kunahitaji mfumo imara na sio mtu mmoja. Sio kama kuongoza mbuzi ambapo mtu mmoja anaweza kuongoza mbuzi hata elfu moja.

Kuongoza watu hakuhitaji kuropoka ropoka kama mwendawazimu.
Hakuhitaji kuwarushia watu mawe na kuwavunja miguu kama sio kuwachinja kabisa.

Kuongoza watu hakuhitaji kila kitu ufanye wewe bali unapaswa uwaachie wasaidizi wako nao wafanye.

Rais Samia anaongoza watu sio mbuzi.

Nafahamu familia zetu za kiafrika zimezoea na kulelewa kimbuzi mbuzi, unakuta Baba au Mama ni mkatili, mbabe na mshenzi kwa kisingizio cha malezi. Nafahamu familia za kiafrika wazazi wetu walikuwa na dhana kuwa Mtoto hana haki kwa sababu ni kama mbuzi tuu.
Huwezi ukalelewa kama mbuzi alafu ukawa na akili ya kibinadamu, huwezi ukalelewa kama mnyama alafu ukawa na utu.
Lazima nawe utakuwa na tabia za kinyama, ukatili na huna utu.

Sio ajabu kusikia mtu anampiga mke wake mpaka anamkata kata na mapanga. Sio ajabu kusikia mzazi anamchapa mtoto wake mpaka anamjeruhi. Ni kwa sababu halei mtu kwa utu, bali analea mtu kama mbuzi (mnyama).

Mnataka Mama awe mkali au mbabe kwani anaongoza mbuzi?

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Dar es salaam
 

LUPEM

JF-Expert Member
Aug 10, 2020
355
500
Uwa unaweka namba za simu ili upigiwe na upewe uteuzi.Baada ya kujipendekeza kwa ,kuandika upupu.Nakushauri ,uendelee na kiajira chako hicho.Ukija huku utakufa mapema.Maana una majungu ya kipumbavu sana.
 

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
3,603
2,000
Wangekuwa na akili wangelalamika kuwa Rais hafuati katiba wala sheria tungewaunga mkono.
Lakini wanasema kazidi upole, sijui wanamaanisha nini
Nukuu ya Mzee Mwinyi


Screenshot_20210519-231429.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom