Mnataka Rais Magufuli na Serikali yake wasipongezwe na kukosolewa?


M

Mpangawangu

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2014
Messages
721
Likes
304
Points
80
M

Mpangawangu

JF-Expert Member
Joined Mar 5, 2014
721 304 80
Watu wakimsikia mtu anakosoa au kupongeza jambo flani la serikali anaambiwa si Mzalendo au Anajipendekeza kwa watawala. Hivi nchi ikimpata Rais Mzuri au mtendaji mnataka asipongezwe anapofanya vizuri? Je akifanya vibaya hamtaki watu watoe mawazo mbadala? Hivi kuna nchi iliyoendelea Duniani kama Marekani? Mmeshasikia kuwa wameamua kuacha siasa kwakuwa sasa wanamaendeleo? Wale mnaosema huu ni muda wa maendeleo watu waache siasa mnatumia kigezo cha nchi gani iliyoendelea baada ya kuacha siasa?

Siasa ni maisha,siasa ni marumbano ya mawazo mbadala,siasa inawaongezea viongozi uwezo wa kufikiri. Bila siasa tungekuwa bado tunalipa ili kodi ya kichwa iliyosababisha watu kukimbia kujificha porini,ni kupitia siasa watu wanalipa VAT bila kujificha porini maana VAT ipo kwenye bidhaa ambazo ni lazima uzitumie hata kama umejificha huko porini. Marekani pamoja na maendeleo makubwa lkn hawajawahi kujenga hoja dhaifu ya kuacha siasa.

Chama cha Demokratic(Chama cha Obama)kimefanya mengi makubwa kwa nchi ya Marekani lkn hiyo haikuwa Kigezo cha kuwanyamanzisha Wapinzani wao wa Republican(Chama cha Bush) Republican waliikosoa serikali bila kujali kuwa Marekani ndio Taifa kubwa Duniani. Jambo muhimu kufahamu ni kuwa Maendeleo ni matokeo ya Msuguano wa Mawazo,unatoa wazo na wenzako wanatoa wazo,mnashindanisha hoja kisha mnakubaliana kuwa wazo fulani likobireshwa kwa wazo la flani basi mtapata mwelekeo mzuri.ukiona hakuna mgongano wa mawazo basi ujue mmeamua kumuachia mtu mmoja ndio afikirie.

Hata kwenye ngazi ya familia ,Baba au Mama ukiona anafanya mambi bila kwanza kuvutana kwa kila mmoja kuweka vipaumbele vyake na kisha kuafikiana kipi mfanye kwa Pamoja basi hiyo familia itakuwa duni miaka yote.

Hivyo tunapokosoana na kupongezana tufanye hivyo kwa maslahi ya taifa,tufanye hivyo tukilenga kulifanya taifa letu kuwa taifa kubwa, Lakini tukiwa na misimamo mikali dhidi ya wanaopongeza au kukosoa, tutajenga taifa la watu wenye chuki na visasi,watu wanaoombeana mabaya,taifa lililogawanyika na mwisho taifa lenye watu wanaowasaidia maadui zetu kutushughulikia. Kupongezana na kukosoana kwa lengo la kujenga ni afya kwa nchi yetu.
 
successor

successor

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2012
Messages
2,944
Likes
5,199
Points
280
successor

successor

JF-Expert Member
Joined Oct 25, 2012
2,944 5,199 280
Mungu wa Chattle hakosei, ni marufuku kumkosoa. Kwani hukumuona jana alitimua mbio kuonyesha yuko fit?
 
D

Danny Jully

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Messages
3,105
Likes
1,917
Points
280
D

Danny Jully

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2013
3,105 1,917 280
Ukipongeza wewe ni mzalendo na mpenda maendekeo, ukikosoa wewe ni mchochezi, mpinga maendeleo na msaliti.....!
 

Forum statistics

Threads 1,235,767
Members 474,742
Posts 29,234,625