Mnataka Iddi Simba aue mashirika yote ya umma anayosimamia ikiwemo PRIDE...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnataka Iddi Simba aue mashirika yote ya umma anayosimamia ikiwemo PRIDE...?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sisimizi, Aug 16, 2011.

 1. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 488
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kwanza tuelewe kwamba hakuna shirika au kampuni ya Umma ambayo Iddi Simba amekuwa sehemu ya wasimamizi ikafanikiwa. Kama ipo itajwe hapa!

  1. Tukianzia na kampuni tu binafsi ya NICOL iliyoasisiwa na akina Mosha na Iddi Simba na nikaingia mtaani kukusanya fedha kwa watanzania kwa lengo la kuwa kampuni ya uwekezaji, hivi sasa ni kwisha habari yake!

  2. Hivi karibuni tumesikia kwamba IDDI SIMBAni sehemu ya Board of Trustees wa UDA iliyouzwa kwa utata, ambayo ni mali ya umma. Kuna tuhuma kwamba akaunti yake ilikutwa na lundo la fedha zinazohisiwa kuwa ni sehemu ya 10%.

  3. IDDI Simba ni mwenyekiti wa Board of Trustees ya PRIDE Tanzania ambalo nalo ni shirika la umma lililoundwa kwa kutumia "Revolving fund", mali ya serikali ya Tanzania. Cha ajabu mtu anapouliza mmiliki wa PRIDE utasikia IDDI SIMBA... Hivi sasa PRIDE nayo ipo katika mzigo mkubwa wa madeni na uendeshaji wake unakuwa ni mugumu.

  Je! wahusika mnasubiri mpaka hata PRIDE ife ili mmwondoe IDDI SIMBA, mtu mbadhilifu mahali pale
   
Loading...