Uchaguzi 2020 Mnataka haki na usawa, kwanini wanawake mmemtenga Queen Cuthbert Sendiga, Mgombea Urais kupitia ADC?

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,731
21,132
Kwa nini wanawake mnadai haki na usawa wa kijinsia huku mnashindwa kuonyesha umoja kwenye njia mnayoipitia katika kudai usawa na ile nadhalia ya kutaka kupewa nafasi kwenye mabalaza ya maamuzi?

👉 Wanawake wanadai usawa kwenye kila jambo wanaloona wameachwa nyuma, tuzungumzie siasa na uongozi, taasisi na mikusanyiko ya kila aina inayokaa ili kudai nafasi kwenye siasa inafanyika kila siku.

Bahati mbaya au nzuri ni kwamba kupitia sehemu hiyo wao wenyewe wanashindwa kujua hawana ubavu kupata usawa au kuingia kwenye nafasi kubwa pasipo upendeleo au kusukumwa.

Queen Cuthbert Sendiga ni mgombea urais kupitia chama cha alliance for democratic ni mwanamke pekee kati ya wagombea wote wa nafasi ya urais, lakini mpaka sasa hakuna sehemu yoyote inayopiga kelele kama si kampeni kumnadi mama huyu.

Kwa nini tunasema haki wanayodai wanawake siyo ile ya kutoka moyoni, picha tunayoiona kupitia mgombea huyu ndiyo ukweli halisi wa tabia za jinsia hii pendwa.

Nilidhani kupitia mama huyu basi wanawake kama siyo wote wangeonyesha umoja angalau tushangae na kusema kitu, ila mpaka hapa wamekwama.

Mgombea mwenyewe alishasema kama siyo kulalamika kuwa "Wanawake hawana umoja" sasa haifahamiki kama tatizo ni chama au ni nini?

Karibu kwa mjadala.
 
Uraisi sio swala la jinsia, ni swala la Sera
Hawa hawa wanawake wa Tz kipindi Trump kashinda walituma messages za sympathy kwa Hillary kuonesha simanzi zao kwa mwanamke kukosa fursa ya kuitawala 'dunia'.

Lakini muda mchache nyuma (2015) Anna Mughwira (mwanamke mwenzao) aligombea urais na hakufikisha hata kura laki moja, unafki wa kiwango cha lami.
 
Kwahiyo hata kama hafai tumchague kwasababu tu ni mwanamke?
Tunachojadiri si kama hafai ila tunachoangalia ni kumpa hamasa ikifahamika hawezi kushinda.

Pamoja na hilo nafasi yake ni kubwa kuliko baadaye mnavyoendeleza pirika za nafasi za kusukumwa ambazo kwa sasa tunaona zinavyo watoa jasho huko kwenye majimbo.
 
Hamasa anayohitaji yeye si nyingine zaidi ya kupigiwa kampeni ashinde Urais kama nia yake ilivyo. Hatuwezi kumdanganya anafaa kumbe hafai. Urais ni issue serious kila mtu yupo busy na mgombea anayeona anafaa.
Kama ni hamasa kila mgombea anafaa apatiwe, wagombea wapo wengi na sidhani Kama wote wanapata hamasa hiyo unayoisema.
Wanawake tunampongeza kwa ujasiri na uthubutu, anatengeneza CV yake itamsaidia huko mbeleni.
Muda wa kuwapamba wanawake hata kama hawana vigezo umepitwa na wakati.
 
Kwa nini wanawake mnadai haki na usawa wa kijinsia huku mnashindwa kuonyesha umoja kwenye njia mnayoipitia katika kudai usawa na ile nadhalia ya kutaka kupewa nafasi kwenye mabalaza ya maamuzi?

Wanawake wanadai usawa kwenye kila jambo wanaloona wameachwa nyuma, tuzungumzie siasa na uongozi, taasisi na mikusanyiko ya kila aina inayokaa ili kudai nafasi kwenye siasa inafanyika kila siku.

Bahati mbaya au nzuri ni kwamba kupitia sehemu hiyo wao wenyewe wanashindwa kujua hawana ubavu kupata usawa au kuingia kwenye nafasi kubwa pasipo upendeleo au kusukumwa.

Queen Cuthbert Sendiga ni mgombea urais kupitia chama cha alliance for democratic ni mwanamke pekee kati ya wagombea wote wa nafasi ya urais, lakini mpaka sasa hakuna sehemu yoyote inayopiga kelele kama si kampeni kumnadi mama huyu.

Kwa nini tunasema haki wanayodai wanawake siyo ile ya kutoka moyoni, picha tunayoiona kupitia mgombea huyu ndiyo ukweli halisi wa tabia za jinsia hii pendwa.

Nilidhani kupitia mama huyu basi wanawake kama siyo wote wangeonyesha umoja angalau tushangae na kusema kitu, ila mpaka hapa wamekwama.

Mgombea mwenyewe alishasema kama siyo kulalamika kuwa "Wanawake hawana umoja" sasa haifahamiki kama tatizo ni chama au ni nini?

Karibu kwa mjadala.
Mtu hatakiwi kupewa support just because ni member wa jinsia fulani
 
Sasa kama yeye kuwa member katika hiyo jinsia ndio hufanya kuwa kikwazo hata kwa ule uwezo alionao kutoonekana ama kuthaminiwa,je hapo kuna ubaya gani kumpa support? Mfano 2015 Mama Anna Mghwila alikuwa mgombea mzuri kushinda hata wagombea wengine ambao ni wanaume,aliweza kushiriki hadi mdahalo(na tuliona uwezo wake) hali ya kuwa wagombea wa ccm na chadema waliogopa kushiriki ila ajabu akapata kura chache sana.

Na hata huyo mwana mama wa ADC naye yupo vizuri ila jinsi yake ni kikwazo,kama si hivi vikwazo vya jinsia tungekuwa tunaona wakina mama wenye uwezo wakigombea nafasi za urais kwenye vyama vikubwa kama chadema na ccm.
 
Hatujamtenga huyo mgombea maana angekuwa chama ccm na akabebwa na Dolla angeonekana tu, Mimi mwenyewe ndio nasoma hapa kuwa ni mgombea Raisi. So usitulaumu wanawake laumu media coverage inapoibeba ccm kuliko wagombea wengine
 
Hawa hawa wanawake wa Tz kipindi Trump kashinda walituma messages za sympathy kwa Hillary kuonesha simanzi zao kwa mwanamke kukosa fursa ya kuitawala 'dunia'.

Lakini muda mchache nyuma (2015) Anna Mughwira (mwanamke mwenzao) aligombea urais na hakufikisha hata kura laki moja, unafki wa kiwango cha lami.
Mimi nachagua mtu kulingana na uwezo na sera na sio jinsia
 
Sasa kama yeye kuwa member katika hiyo jinsia ndio hufanya kuwa kikwazo hata kwa ule uwezo alionao kutoonekana ama kuthaminiwa,je hapo kuna ubaya gani kumpa support? Mfano 2015 Mama Anna Mghwila alikuwa mgombea mzuri kushinda hata wagombea wengine ambao ni wanaume,aliweza kushiriki hadi mdahalo(na tuliona uwezo wake) hali ya kuwa wagombea wa ccm na chadema waliogopa kushiriki ila ajabu akapata kura chache sana.

Na hata huyo mwana mama wa ADC naye yupo vizuri ila jinsi yake ni kikwazo,kama si hivi vikwazo vya jinsia tungekuwa tunaona wakina mama wenye uwezo wakigombea nafasi za urais kwenye vyama vikubwa kama chadema na ccm.
Shida ya huyo mama sio jinsia chama chake bado kichanga na Hana rasilimali nyingi pia sio sahihi eti mtu vile ni mwanamke achaguliwe kwa kigezo Cha ujinsia wake
 
Sasa kama yeye kuwa member katika hiyo jinsia ndio hufanya kuwa kikwazo hata kwa ule uwezo alionao kutoonekana ama kuthaminiwa,je hapo kuna ubaya gani kumpa support? Mfano 2015 Mama Anna Mghwila alikuwa mgombea mzuri kushinda hata wagombea wengine ambao ni wanaume,aliweza kushiriki hadi mdahalo(na tuliona uwezo wake) hali ya kuwa wagombea wa ccm na chadema waliogopa kushiriki ila ajabu akapata kura chache sana.

Na hata huyo mwana mama wa ADC naye yupo vizuri ila jinsi yake ni kikwazo,kama si hivi vikwazo vya jinsia tungekuwa tunaona wakina mama wenye uwezo wakigombea nafasi za urais kwenye vyama vikubwa kama chadema na ccm.
Huyo mama naamini hata mwenyewe anajitambua hana uwezo. Angekuwa nao hata asingetumia nguvu angepata sapoti.
Aende kwenye majukwaa yanayoonekana tumuone tumjue.
Naamini mtu kama fatma karume angegombea ungeona sapoti ya wanawake . Hizi ni zama za kuonyesha ujuzi na sio upite kwa kuonewa huruma.
 
Back
Top Bottom