Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,220
MNASHINDWA KWENYE MAMBO MENGI KWASABABU HAMPO MAKINI , BADILIKENI
Kukosa umakini kwenye vitu ambavyo tunafanya kumekuwa chanzo cha matatizo makubwa sana.
Watu wengi wamepata hasara kubwa, watu wengi wamepoteza maisha yao, watu wengi wamejikuta kwenye hali nagumu kwa sababu tu kuna mtu hakuwa makini kwenye kutimiza majukumu yake.
Na kwa nini watu hawapo makini kwenye kutimiza majukumu yao?
Kwa sababu akili yao haipo pale kwenye kile kitu wanachofanya. Unafanya kazi lakini akili yako inafikiria vitu vingine. Mwishowe unafanya kazi ambayo ni mbovu sana na mbaya zaidi inakwenda kuwadhuru watu wengine.
Kama kila mtu angeweka akili yake kwenye kile anachofanya na akakifanya kwa umakini mkubwa, tungekuwa na maisha bora sana. Kwa sababu tungekuwa na vitu vilivyo bora sana ambavyo vingerahisisha maisha yetu.
Kuwa makini unaposikiliza. Mazungumzo yamekuwa yanakosa maana kwa sababu wasikilizaji hawapo makini. Mwenzako anaongea, badala ya kusikiliza kwa makini uelewe anachosema ni nini, wewe akili yako inafikiria umjibu nini. Kwa njia hii mawasiliano yanakuwa sio mazuri na ujumbe uliotakiwa kufika haufiki sawasawa.
Kuwa makini unapozungumza, usiongee tu kwa sababu na wewe unaweza kuongea, na usiongee tu kwa sababu umesukumwa kuongea, kuwa makini kwenye kila neno unalotoa, kila neno linaweza kujenga au kubomoa. Tumia maneno ya kujenga tu.
Umakini ni muhimu sana kwenye kila jambo unalofanya kwenye maisha yako

Last edited: