Elections 2010 Mnasemaje kuhusu hili...???

Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
4,107
2,506
Samahanini sana sana sana kwa kulipua hili mada mbele yenu, lakini lengo langu si kuchafua mioyo yenu na ubongo wenu, lengo kujua kitakachotokea huko mbele nchini juu ya Dr. W. Slaa(PhD).

Swali:

Si mnakumbuka JK tulivomwamini kipindi kile 2005, tukamchagua kwa mbwembwe nyiiiingi hadi akaibuka kwa ushindi wa zaidi ya 80% (asilimia themanini), akiwa madarakani tumeshuhudia vituko vyake vyooooote hadi akapoteza uaminifu kwa wananchi wake, vituko kama vile kuwateua maswahiba zake, kutowachukua hatua za kisheria baadhi ya mafisadi na mengineyo mengi. Vyote hivyo vimempelekea kuanguka kwa CCM katika uchaguzi mkuu.

Sasa tuje kwa Dr. Slaa, tumempigia KURA nyingi hapo jana, akitangazwa kuwa mshindi, je, akiwa madarakani, akifanya madudu yoyote yatakayofanana na ya Mkwere, ninyi kama wananchi mnachukuliaje?? Maana yule naye ni binadamu.

Samahanini lakini kwa any inconvenience!!

Mapinduzi Daima...
 
anatolewa 2015 and we elect new person, until we can get it right:smile:
 
Nani kakuambia tulichagua wafalme???????????? Hatuna mawazo mgando ya CCM kutawala milele.. Malecela, Kingunge, Makamba et al
 
Jibu liko wazi, akifanya madudu na yeye uchaguzi ujao 2namtupilia mbali, kwani lazimaaaa!
 
Kwa kuwa itakuwa hamtujamchangua ili akafanye madudu, then akifanya madudu na yeye tunatoa tu haina mjadala hiyo..
 
Tulimchagua awe kiongozi wa wananchi,si kibaraka wa tabaka fulani..kanuni ipo wazi akivurunda tutamtoa kwa kura zetu..hakuna aliye juu ya sheria..ingekua hivyo zizzou alipomzidane Materazi angeachwa tu apete maana upara mkuuuuubwa!
 
kwa nyakati hizi sio rahisi tena kiongozi kuwa na madaraka makubwa maana nchi zote zinafanya madaliko makubwa sana ya katiba za nchi zao. Hivyo kama mtu atafanya mambo ya ajabu basi atakuwa amejichimbia kaburi. Hii ni dunia ya dot com.
Jiulize maswali yafuatayo: Kwa nini mpaka leo hakuna hospital kubwa kama muhimbili, bugando kcmc iliyokwisha jengwa tangu tuapate uhuru??? kwa nini sehemu nyingi hapo tz ni slum areas? Unajenga chuo kikuu wkt cha zamani kinaoza mpaka wanafunzi wanakaa chini. na mnauza eneo la kupanua chuo eti mnaweka shopping mall???? mnazo kweli??? ccm ndio cahanzo ya yote maana hakuna anayewajali wananchi ila matumbo yao na familia zao. Malecela kafanya kwao? hakuna JK kafanya nini kwao hakuna. Mnasikia sasa wanataka kuktaa kuisgn kwamba wameshindwa uchaguzi akina tyson na matlida yote hayo anajua atakufa baada ya siku mbili maana wamezoa kuibwa
 
Samahanini sana sana sana kwa kulipua hili mada mbele yenu, lakini lengo langu si kuchafua mioyo yenu na ubongo wenu, lengo kujua kitakachotokea huko mbele nchini juu ya Dr. W. Slaa(PhD).

Swali:

Si mnakumbuka JK tulivomwamini kipindi kile 2005, tukamchagua kwa mbwembwe nyiiiingi hadi akaibuka kwa ushindi wa zaidi ya 80% (asilimia themanini), akiwa madarakani tumeshuhudia vituko vyake vyooooote hadi akapoteza uaminifu kwa wananchi wake, vituko kama vile kuwateua maswahiba zake, kutowachukua hatua za kisheria baadhi ya mafisadi na mengineyo mengi. Vyote hivyo vimempelekea kuanguka kwa CCM katika uchaguzi mkuu.

Sasa tuje kwa Dr. Slaa, tumempigia KURA nyingi hapo jana, akitangazwa kuwa mshindi, je, akiwa madarakani, akifanya madudu yoyote yatakayofanana na ya Mkwere, ninyi kama wananchi mnachukuliaje?? Maana yule naye ni binadamu.

Samahanini lakini kwa any inconvenience!!

Mapinduzi Daima...

Sijui upo wapi? Kikwete tayari anaongoza kwa matokeo ya jumla. Slaa apiganie kuwa mwenyekiti wa Chadema sasa!
 
Sure? Hahahaha haya ngoja tuone, ila nina hakika hakuna kitakachoharibika au?
Kumbe swali lilikuwa mtego, nimeanza kukustukia......!
Habari ndy hiyo, ukimweka mtu akavurunda unamtoa unaweka mwingine.
 
Back
Top Bottom