Mnasemaje hapa -DPP,Ushahidi wa viungo vya Albino polisi vipo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnasemaje hapa -DPP,Ushahidi wa viungo vya Albino polisi vipo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Feb 12, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  DPP awaachia watuhumiwa wa mauaji ya maalbino

  2009-02-12 10:32:05
  Na Pendo Fundisha, Mbeya


  Mahakama ya Wilaya ya Rungwe imewaachia huru washitakiwa wawili waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya albino, Henry Mwakajila, aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha pili wa Shule ya Sekondari ya Ukukwe iliyopo Wilaya ya Ileje.

  Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Stephen Mbungu jana alisema kuwa washtakiwa hao wanaachiwa huru kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) baada ya kuagiza kuwa hakuna haja ya kuendelea kusikilizwa kwa kesi hiyo.

  Mbungu aliwataka waliochiwa kuwa ni Mganga wa jadi maarufu kama sangoma, Asangalwisye Katite na Gererde Kalonga, Wakazi wa Wilaya ya Ileje.

  Mara baada ya mahakama hiyo kutangaza kuwaachia huru, washitakiwa hao walijikuta furaha yao ikikatishwa ghafla na kupigwa bumbuwazi kisha kupiga kelele baada ya kukamatwa tena na askari polisi na kupelekwa katika kituo cha Wilaya ya Rungwe kichopo mjini Tukuyu.

  Akizungumza na waandishi wa habari Hakimu huyo alisema tatizo la mauaji ya malbino lisichukuliwe mzaha hata kidogo la sivyo jitihada zote za viongozi wakuu wa nchi hazitazaa matunda kuyakomesha.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Rungwe , Mariamu Lugaila alisema maamuzi hayo yanaweza kuleta matatizo katika jamii na kukwamishwa mauaji ya maalbino.

  Washtakiwa hao walikamatwa na polisi Febuari 27, mwaka jana kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya viungo vya binadamu.

  Inadaiwa polisi waliwafanyia upekuzi na kuwakamata na baadhi ya viungo vya binadamu vilivyosadikiwa kuwa ni vya albino na kuhusishwa na mauaji ya mwanafunzi huyo baada ya kupotea nyumbani kwao katika Kijiji cha Kiwira februari 27, mwaka jana katika mazingira ya kutatanisha.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mwiba, sasa tutaingilia uhuru wa mahakama mpaka lini? kama mahakama imejiridhisha kuwa kuwa watuhumiwa hawakutenda kosa sasa hapakuwa na fursa ya kuwaachiwa huru?
   
 3. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tatizo polisi, ofisi ya DPP inawezekana wanafanya kazi kwa mazoea tu. Ingekuwa vyema tungekujua ushahidi uliowasilishwa mahakamani ukoje maana inawezekana prosecutors hawakuandaa kesi yao kama inavyotakiwa. Kwa maoni yangu vile vile elimu ya askari wetu inaweza kuwa inachangia pia kuwa na poor judgement.

  Sijui hata kama polisi wetu huwa wanakuwa na camera wanapokwenda kusachi watuhumiwa au equipment za kuweza kuchukua fingerpints kwenye maeneo ya matukio.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hicho ndicho alichoogopa PM. Kuwapeleka watu mahakamani utatakiwa uje na ushahidi wenye uzito wa kutosha siyo tuhuma tu! NI rahisi sana kumtuhumu mtu kwa vile umemkuta na viungo fulani vya binadamu, ni jambo jingine kabisa kuthibitisha pasipo chembe ya shaka kuwa yeye ndiye muuaji au amevunja sheria fulani.

  Ndiyo maana yeye alipendekeza wauawe papo kwa papo, maana mtu unaweza kuumbuka hivi hivi.
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hivi umesoma ile habari kule mwisho wake pale inaposema Polisi waliwakamata na viungo vya albino au polisi hawana uwezo wa kutambua mkono wa nyani na wabinadamu, au polisi walisema uongo ,au polisi walibambikiza,itabidi mkuu wa polisi wa wilaya na mkoa watoe ufafanuzi ?

  Na hii habari ni ya upumbavu maana mwandishi nae hajui anachokiandika, kama utaisoma na kuisoma unaweza usifahamu ,utaona ni mauza uza tu au uchonganishi, kuna sehemu mwandishi alisema walikamatwa tena hakuendeleza walikamatwa kwa sababu gani ? Au labda jaji alikuwa hana habari kama walikamatwa na viungo vinavyoaminika ni vya albino iwe iwavyo kukamatwa na kiungo cha binadamu ni kosa tena linaweza kukuweka katika hatia ya mauaji ,vipi utakutwa na kiungo cha binadamu ?

  Hebu someni hiyo habari halafu muniambie kama hao watu waliachiwa au walikamatwa , na ni nani wa kulaumiwa muandishi au mhariri ?
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwanakijiji,

  Mkuu huishi kunimaliza!..
  Nimecheka hadi nashindwa hata kuandika, ama kweli sheria ni somo moja zito sana...
  Duh! sasa mkuu huyu mtu anayekutwa na viungo vya buandamu kuna maelezo gani au sheria gani inayomlinda!..au ndio fashion asilia inayokubalika kikatiba..
  I mean nashindwa kabisa kuelewa kwa nini mtu ame store viungo vya binadamu nyumbani kwake karne hii..
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Feb 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  mzee.. hapa ni lazima uelewe ukimkamata mtu hakikisha unamshtaki kwa mashtaka sahihi na ushahidi uoneshe mashtaka ya kosa linalotakiwa. Polisi walipowakamata hawa watu waliwafikisha mahakamani kwa kukutwa na viungo vya Albino na kudaiwa kwa namna moja wanahusika na mauaji ya kijana mwanafunzi.

  Sasa ukimpeleka mtu mahakamani kwa tuhuma hizo, you better back them up. Kitu pekee walichokutwa nacho ni vinavyodhaniwa kuwa ni viungo vya binadamu. Sasa mwendesha mashtaka atatakiwa mbele ya jaji kuonesha kuwa viungo hivyo ni vya marehemu mtajwa, kuwa wahusika walionekana au kwa namna fulani kuwa katika eneo ambalo marehemu aliuawa na ushahidi mwingine.

  Sasa baada ya kuangalia ushahidi wote wanajikuta hawawezi kuthibitisha kuwa masalio ya viungo ni vya marehemu na hakuna ushahidi kuwa wahusika waliwahi au walionekana na marehemu wakati wowote. Sasa, utaweza vipi kuendelea na kesi ya awali? Huwezi kwa sababu utashindwa.

  Sasa, kwamba wamekutwa na vinavyodhaniwa kuwa ni viungo vya binadamu laweza kuwa kosa jingine kabisa. Lakini itakuwa kama viungo hivyo ni vya sokwe mtu? Kiumbe ambaye tunauhusiano naye wa kijenetiki kwa asilimia 98? Kule kijijini mtu akakuta masalio ya kidole cha Sokwe utafikiri atajua ni sokwe..?

  So, umuhimu wa mahakama ndipo unapokuja hapo, kuwa ukinishtaki mimi hakikisha unaushahidi wa kutosha kuthibitisha kosa langu. Si unakumbuka mambo ya OJ.. ? "If it doesn't fit, you must acquit"! Simply put, if the evidence doesn't fit the accusation of an alleged crime, the accused must walk.

  Sasa kwa vile wamekamatwa tena, the burden of proof is on the government to show that these people broke any law.
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Feb 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwanakijiji,
  Je, hii ni tunzi au ukweli unazungumza!...
  Yaani mtu akutwe na viungo vya binadamu kisha sisi hapa JF tuanze kusema/kuunda hoja kuwa inawezekana kuwa ni viungo vya Sokwe?..Hii tumeipata wapi ya kusema inawezekana wakati Polisi wanasema ni viungo vya binadamu lakini huyo mwandishi ndiye aliyesema inasadikiwa kuwa...
  Ebu nambie mkuu wangu wewe umekamatwa na viungo vya Sokwe lakini unashtakiwa kuwa umeua binadamu, utashindwa kuwambia Polisi kuwa hivyo viungo ni vya Sokwe sii binadamu!..
  Kwanza, hii habari ya waganga wa kienyeji kuwa na viungo vya binadamu ni sheria gani inayowalinda?.. ati unaingia nyumbani kwa mganga.. unakuta fuvu la kichwa cha mtu limetundikwa ukutani na ramli inapigwa kwa kutumia vipande vya mifupa ya vidole vya mikono toka mwili wa binadamu.. Na mtu anaingia kwa heshima akiogopa kuuliza badala yake yeye ni mgonjwa asiyeumwa hivyo kaa kimya upewe nguvu ya ajabu kufufua dhahabu na Utajiri... Mbona huyo mganga mwenyewe hana kitu! hivi kweli yeye hataki kuwa tajiri?..kama hataki sasa fee kubwa ya nini wanapodai kulipwa..

  Come on now, jamani tunapolalamika Polisi wetu, mahakama zetu na serikali yetu kwa kutofanya kazi vizuri inabidi nasi tuwe na picha tofauti na ile wanayoitumia wao..
  Mkuu umegusia ktk mada moja jinsi serikali yetu inavyoshindwa kuwalinda wabunge na viongozi wetu wakati ktk kila kifo kuna circumstantial evidence ambazo zinatatanisha...Lakini tumechagua kazi ya Mungu kuwa mbele wakati hata mauaji ya kweli ni kazi ya Mungu kwa marehemu na kazi ya shetani kwa muuaji..
  Inaonyesha wazi sisi tunachotazama ni upande mmoja tu wa kazi ya Mungu ktk kutoa maamuzi yetu, ile kazi ya shetani hutumika kulingana na mkoswa..
  Kama hawa wakisiwa wangekuwa wametuhumiwa kwa kumuua mbunge au waziri wangekiona cha Moto na pengine huyo hakimu angekosa kazi..kwani ushahidi wa viungo vya binadamu hata kama vinakisiwa kuwa vya binadamu ni lazima vifanyiwe uchunguzi zaidi kuhakikisha sio vya binadamu kabla ya kesi kusimama...nazungumza kwa emotions pia kutokana na mazingira yetu kuwa magumu sana ktk kuthibitisha mambo mengi kisayansi..Huwezi ku dismiss kesi kwa ukosekanaji wa ushahidi tosha ktk maswala ambayo hayawezi kuwa na ushahidi tosha kama vile nchi za Ulaya..Sote tunafahamu kuwa hatuna vitengo vingi vya uchunguzi na hasa huko vijijini ndio kabisa!..Badala yake huyo mchawi ndiye mwenye vitengo na yawezekana kabisa huyo hakimu kaambiwa asipowaachia atakiona cha moto!...Nina hakika inawezekana kabisa hata ile search ilifanyika bila warrant hivyo ushahidi huo umetupiliwa mbali..wakati kuna mifani kibao ya kesi ambazo watu wamekuwa searched bila warrant na leo hii wamefungwa miaka 20 kwa wizi wa mbuzi.

  Mkuu, kusema kweli sote tunachoogopa ni kumfunga ama kumhukumu mtu asiyekuwa na makosa lakini pia tunahitaji kuzingatia ukosekananaji wa nidhamu na ufundi wa kukusanya ushahidi nchini..Ndio yale yale ya kutaka kuanzisha mahakama ya Kadhi wakati waislaam wenyewe wengi wao wanaoa na kuzaa bila kufuata misingi ya dini yao, sasa sijui hiyo sheria inaweza kusimama vipi?.
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wamekutwa na viungo vya binadamu haya maelezo yaliwakilishwa kwa Jaji hivyo jaji asingeweza kuwaachia bila ya kuwapa hukumu kwa kosa lao la kukutwa na viungo vya binadamu ni lazima wangeishia jela japo miaka kumi ,iwe ni fundisho.Lakini unawaachia eti hakuna kosa ,huoni kma rushwa imeshafanya kazi yake hapo ?
   
 10. I

  Ilongo JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 292
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  Tukawasaidie Sengerema tafadhali. Hali inazidi kuwa mbaya ....

  Albino auawa, anyofolewa miguu
  David Azaria, Sengerema
  Daily News; Wednesday,February 18, 2009 @19:50


  Mlemavu wa ngozi mkazi wa Kijiji cha Butonga, Kata ya Sima, wilayani hapa, Yunis Bati (14) ameuawa kikatili na kukatwa miguu yake na kutoweka nayo. Kabla ya kukatwa miguu, Yunis alipigwa panga kisogoni na kufa papo hapo.

  Tukio lilitokea saa 5.30 usiku wa kuamkia leo katika kitongoji cha Kahindaga B baada ya mlemavu huyo msichana kuvamiwa na watu wasiofahamika nyumbani kwao. Hili ni tukio la pili kutokea katika kata na wilaya hiyo katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja, kwani katikati ya Januari mwaka huu mlemavu mwingine wa Kijiji cha Sogoso katani humo aliuawa na kunyofolewa mguu mmoja.

  Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Elinasi Pallangyo, alithibitisha tukio hilo na kueleza kwamba serikali imesononeshwa kwa kuwa limetokea siku chache tu tangu yeye na viongozi wengine wa wilaya watoke katika kijiji hicho kuwaelimisha wananchi jinsi ya kupambana na mauaji hayo. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya alisema:

  “Inakua vigumu sana kusimulia tukio hilo, lakini hali halisi ndiyo hiyo, ni mauaji ya kinyama sana sijawahi kuyaona, lakini kibaya zaidi ni kwamba mauaji haya yanakuja wakati tuko katika mchakato wa kuelimisha wananchi namna ya kupambana na matukio ya aina hii katika maeneo yao, imetusononesha na kutusikitisha sana,” alisema Mkuu wa Wilaya huku akijifuta machozi.

  Akisimulia tukio hilo baba wa marehemu, Bahati Lugwisha (53), alidai kuwa usiku akiwa amelala ndani na mkewe na watoto wake wanne wa kike akiwamo marehemu, ghafla alisikia mlango ukivunjwa na watu asiowafahamu na kuingia ndani. Alisema baada ya kuingia, mmoja alipitiliza hadi chumbani mwake na kumbamiza na ubapa wa panga usoni na kumwekea panga shingoni huku akimtaka atulie; alitii amri huku wengine wakiwasimamia watoto wawili ambao nao ni albino waliokuwa wamelala chumbani.

  “Wakati mmoja akiwadhibiti wale wawili chumbani ili wasipige kelele, mmoja aliendelea kumkata miguu marehemu huku mwingine akiwa nje, akimbana mke wangu ambaye alikuwa akifanya jitihada za kutoka nje kupitia dirishani,’’ alidai baba huyo. Aliongeza kuwa kabla ya kumkamata na kumnyofoa miguu mtoto huyo, kwanza alimwamuru kulala kifudifudi na kisha kumkata panga kisogoni kwenye mishipa ya fahamu, na kumkata miguu na kuinyofoa.

  “Nadhani yule mtoto alikufa palepale, kwa sababu pamoja na kumkata miguu hiyo kwa tendo lililochukua karibu nusu saa, hatukusikia akipiga kelele za maumivu na baada ya watu hao kuondoka, tulipomwangalia alikuwa akitetemeka tu mwili wote,’’ alisimulia. Hadi mwandishi wa habari hizi anaondoka eneo la tukio jana mchana, zaidi ya wananchi 3,000 wa vijiji sita vya kata hiyo, waliofika katika eneo la tukio ili kuwasaka watuhumiwa hao, walikuwa wakiendelea kupiga kura za siri ili kuwabaini walihusika chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi.
   
Loading...