Mnara wa Babeli unakaribia kuanguka

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
43,087
2,000
Mwaka 2012 wakati najiunga JF moja ya post zangu za awali kabisa nikiwa Junior Member niliwafananisha CCM na wajenzi wa Mnara wa Babeli.

Leo hii miaka 3 ninayo furaha kuona Muumba anakamilisha ndoto zangu.

Watanzania wenzangu,yote hayo mnayoyashuhudia katika dakika za mwisho kuelekea kwenye uchaguzi mkuu hayatokei kwa bahati mbaya bali ni kwa makusudi ya mwenyezi Mungu.

Naamini pia ulikuwa ni mpango wa Mungu UKAWA watoke Bungeni ili wabaki wao peke yao na aibu yao.

Kwenye mbio za uraisi nako mambo ni yale yale tu.Sasa kwa hali hii ni kwani nisiamini huu ni mpango wa mwenyezi mungu?Wabunge hawa wanafanyaje maamuzi ya aina hii ikiwa ni miezi michache tu kuelekea kwenye uchaguzi mkuu kama sio kunyimwa maarifa au kutiwa upofu na mwenyezi mungu?

Wabunge wa chama chao hawaoni mbele,watia ni nao hawatazami mbele na viongozi wao wanenyimwa maono.

Nakumbuka niliandika mwenyezi Mungu kawanyima maarifa na kweli leo mambo wanayoyatenda yanadhihirisha wamekosa maarifa.

Leo hii hawako pamoja; hawana kauli moja; kilichobaki ni anguko kuu mithili ya mnara wa babeli kutimia.
 

Ngigana

JF-Expert Member
Apr 16, 2010
1,828
2,000
Salary Slip

Mkuu salary Slip, siyo kuanguka kwa mnara wa babeli tuu, bali tuko ndani ya kipindi cha Jubilee! After Jubilee lazima tupate mambo mapya, na mojawapo ya hayo ni kuwa na institutions mpya siyo zile zile za kiwenda wazimu na "ndiyooooo" kwa kila jambo. Mungu anaenda kutenda jambo jipya ktk nchi hii kwa kutikisa misingi yote ya taifa hili. Keep on watching, it will come to pass! majira mapya, mambo mapya, na utawala mpya pia! rushwa na mazindiko na ushirikina vitawatokea puani! Give them nights without vision of God, so that they dont remember their evil agenda and plans!
 
Last edited by a moderator:

sifongo

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,896
2,000
Hakuna kitu kipya chini ya hili jua, angukobla CCM ni lazima litokee kama ambavyo tawala zingine zilianguka baada ya kuacha njia iliyo haki na kukumbatia anasa na wizi, mateso kwa raia wake......unategemea nini kilio cha wamama wazazi wanapokuwa wanagaragara chini na matumbo yao,wazee wenye mikongojo wakilalamikia mafao yao mpk kulala barabarani watu wazima, tunasubiri laana ya aina gani tofauti na hiyo?
 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,544
2,000
Nakililia chama changu jamani. Hakika nilikipenda kwa moyo wote. Haswaa wakati ule nilipoamriwa kukariri ahadi za mwana ccm. Loh! Leo hii, sidhani hata kama huyo M/Kiti wa Taifa hili kiccm kama anaijua hata moja tu. Nasema sidhani, na kama unabisha, weye Nape, najua u karibu naye, mwulize ahadi ya kwanza ya mwana ccm ni... Akipatia tu ni PM nikutumie muda wa maongezi buku moja saa hii. Pia natangaza hata huyo Nape haijui labda akaangalie pale ukutani Chimwaga. Nilikuwa naangalia zile picha zinazoonesha ukumbi mpya wa chama chetu. Loh! Hakuna hata andiko moja la kuhamasisha uamsho wa wana ccm.
Anguko ni dhahiri sii unabii bali ni sasa. Muda uliobaki ni masaa wala sio siku tena.
 

izzo

JF-Expert Member
May 31, 2015
2,814
2,000
katika kila maombi yangu ya kila siku kwa mungu ni cku nishuhudie ccm inakuwa chama cha upinzani na huku mtaa wa lumumba kikiwa ni kijiwe cha kahawa badala ya office za chama kwani naamini viongozi wote wa ccm wayakuwa wakimbizi wa kisiasa ktk nchi mbalimbali duniani
 

mambomengi

JF-Expert Member
May 16, 2009
829
250
Bado sana. Wanasiasa wa bongo no uchuro mtupu na waganga njaa...na wachumia matumbo! Njoo Baada ya miaka kumi na kenda.
 

MTENDAHAKI

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
4,014
2,000
Salary Slip

Nadhani uliyatangulia maono ya nabii/askofu kakobe mwaka jana tu!Alisema hakuna namna CCM itanusurika mwaka huu mpaka watubu!
 
Last edited by a moderator:

Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
43,678
2,000
Pumzika kwa Amani CCM, unavuna ulichokipanda kwa mikono yako na ya watoto wako, Yuko wapi Mpwa wangu lusungo ? tafadhali pita pande hii
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom