Mnapotengana mnawapa mzigo mzito watoto sio tu wakiwa wadogo bali hata wakiwa watu wazima

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,864
Kwema Wakuu!

Huenda ukawa unajiuliza ni Kwa nini Taikon anapenda kujadili masuala ya familia, ndoa, na wanawake. Kwa kifupi tuu ni kuwa Msingi Mkuu wa Jamii ni Familia Bora, familia Bora ni matokeo ya ndoa iliyofuata misingi ya uadilifu. Familia Bora huleta jamii Bora, jamii Bora huzaa taifa Bora.

Sitochoka kugusia mambo haya ningalipo katika mgongo wa Dunia.

Umoja baina ya Baba na Mama huleta Umoja Kwa watoto. Kama Baba na Mama sio wamoja na kila mtu anafuata ubinafsi basi ni wazi hata familia hiyo watoto watakuwa hawana mbele wala nyuma.

Umoja ndani ya ndoa unaletwa zaidi na UPENDO WA dhati wenye msingi ya kimaadili. Upendo wa wanandoa usiofuata maadili huleta machafuko ndani ya Familia.

Taikon ninaamini zaidi katika Upendo. Ninaamini palipo na upendo wa kweli basi hapo usalama upo.

Wanaosema Ndoa haina umuhimu wengi wao ni kutokana na kukata tamaa na kuanguka katika kizazi Chao.

Watu wote wenye akili huchukulia familia Kama Jambo kubwa la maana.

Suala la Talaka haliwezi kupewa kipaombele mahali popote Kwa watu wenye Uelewa mkubwa na wenye malengo ya umilele.

Kutengana na kuachana huathiri watoto kivyovyote na Kwa miaka yote.

ATHARI KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 18


1. Watoto hukosa malezi ya Msingi kutoka Kwa wazazi wao wenyewe.

2. Watoto kuathirika kisaikolojia na kuwa na roho ya utengano tangu wakiwa wadogo.

3. Watoto kuathirika vibaya kiuchumi Kwa kukosa huduma zilizobora kutoka Kwa wazazi kutokana na Migogoro ya wazazi.

4. Watoto kuanza kujenga chuki ya ndani kabisa kutokana na kukosa malezi na Huduma kutoka Kwa wazazi.

5. Watoto kukosa roho ya kujali na kuwa Wabinafsi kulikochangiwa na ubinafsi wa wazazi wao. Sababu nyingi za utengano katika ndoa ni matokeo ya Ubinafsi uliopitiliza.

6. Watoto kukosa mwelekeo wa maisha na kukosa Sapoti ya wazazi kutokana na kutengana Kwa wazazi.

7. Watoto kukukosa Uhuru wa kimalezi Kwa kulelewa na Wazazi wa Kambo. Mtoto akilelewa na Mama au Baba WA kambo hata atendewe Mazuri yapi bado atakuwa hajiamini na hayupo huru.

ATHARI KWA WATOTO WENYE MIAKA 18-50


1. Watoto kushindwa kugawa bajeti kuwasaidia wazazi wake waliotengana
Amtumie pesa Baba, kisha amtumie pesa Mama. Hii inaathiri uchumi wa mtoto. Tofauti na wazazi wakiishi pamoja inakuwa rahisi kuwahudumia Kwa pamoja.

2. Mtoto kupata wakati Mgumu
Amelelewa na Baba wa Kambo mpaka Kakua na baada ya kujitegemea Baba mzazi anakuja naye anataka matumizi. Hii inawapa wakati mgumu Sana watoto, huyu ni Baba yake, Yule ni Baba mlezi. Wengi hapo hujikuta wanasaliti upande mmoja na mara nyingi upande huo unakuwa upande wa Baba Mlezi.

Vipato vya wengi ni duni hivyo uwezo wa kuhudumia Mababa wawili inakuwa ngumu.

3. Watoto kutokujali Wazazi wao
Mtoto akishakua hasa katika Mazingira ya kulelewa na Mzazi mmoja, nguvu ya wazazi Kwa mtoto inakuwa nusunusu tofauti na Aliyelelewa na wazazi mwanzo mwisho.

Ni rahisi kuwapuuza wazazi waliotengana kuliko wanaoishi pamoja. Rahisi Sana.

Na hiyo inatokana na Karma, ubinafsi uliowatenganisha ndio ubinafsi huohuo watoto wenu watautumia kuwatenga.

4. Watoto kutowaheshimu Wazazi wao
Mara nyingi watoto hawawaheshimu wazazi waliotengana Kwa ubinafsi, watoto lazima watajua kuwa Baba aliachana na Mama kisa mchepuko (Ubinafsi wa kutaka kutosheleza tamaa zake za kimwili), au mtoto atajua kuwa Mama alipata Hawara mwenye pesa ndio maana alimuacha Baba.

Mtoto hata kama hatasema Kwa mdomo wake lakini matendo yake yatajionyesha, unajua matendo ni matokeo ya Nafsi ya ndani kabisa.

Zingatia kuwa wazazi wanakuwa muhimu na kuonekana miungu kabla ya mtoto hajapata Mtoto, yaani mtoto wako Kabla hajazaa basi anakuchukulia Kama mungu mdogo lakini akishazaa mambo hugeuka kidogo. Hii ni kutokana na kuwa naye kawa mungu mdogo sasa huna utakalomuambua Kwa habari za Uzazi. Ila Kama ulimfundisha Maadili na ulifanya wajibu wako Kwa kiwango kikubwa pasipo kuonyesha ubinafsi kwake au Kwa Baba/Mama basi ataendelea kukuona wa Maana.

Heshima ya Wazazi IPO katika malezi sio katika Kuzaa. Kuzaa ni sifa ya Mnyama hivyo hata Panya anazaa lakini malezi ndio humtofautisha Mnyama na Binadamu.

Unapoendekeza ubinafsi katika maisha yako na kuathiri watoto wako basi lazima mambo yatakugeukia
Kumbuka watoto wako ni wewe (yaani toleo lako jipya) watoto wako ni kivuli chako kila unachokifanya nao watakufanyia.

Ni muhimu kuchagua Mwenza mnayefanana ili kuepusha utengano utakaoathiri watoto na kuja kuwarudia ninyi wenyewe.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Njia niliyoona ni vyema kwangu

Mfano mke aki cheat sitamuacha nitamfanya tu house girl alele tu wanangu na chumba namuhamisha sitalala nae tena sitamfukuza

Na sitaleta mwanamke ndani nisije vunjia wanangu heshima yao zidi ya mama yao
Nitakuwa napiga mechi nje

Hiyo kwangu naiita win win situation

Au mfasihi una wazo tofauti?
 
Njia niliyo ona ni vyema kwangu

Mfano mke aki cheat sitamuacha nitamfanya tu house girl alele tu wanangu na chumba namuhamisha sitalala nae tena sitamfukuza

Na sitaleta mwanamke ndani nisije vunjia wanangu heshima yao zidi ya mama yao
Nitakuwa napiga mechi nje


Hiyo kwangu naiita win win situation

Au mfasihi una wazo tofauti ?
Na yeye anakuwa anapiga mechi nje, utafanyaje?
 
Yes kuna Umri ukifika hiyo ndio mbinu muhimu ya busara lakini pia yenye faida Kwa familia hasa watoto.

Lakini kama bado haujafika mbali, na bado hamjachuma Mali na nguvu bado unazo hapo option ni kupiga chini tu.
 
Hili bandiko langu limefanya niwaze kuhusu ndoa.

Ubinafsi wa wazazi hufanya mtoto alelewe na mzazi mmoja.

Wacha nikupe nyingine hii.

Watoto wengi wanaolelewa na mzazi mmoja pia hua na kasumba ya kuona kila mtu anapaswa kumsaidia iwe upande wa baba au mama hivyo kupelekea wajomba, mashangazi, bibi, babu na ndgu wengine kushiriki katika ukuaji na masomo yake.

Akifanikiwa huyu huo mzigo anaokua nao unakua si wa kitoto, watoto wa waliomsaidia nao watataka asaidie wenzie.
 
Hili bandiko langu limefanya niwaze kuhusu ndoa.

Ubinafsi wa wazazi hufanya mtoto alelewe na mzazi mmoja.

Wacha nikupe nyingine hii.
Watoto wengi wanaolelewa na mzazi mmoja pia hua na kasumba ya kuona kila mtu anapaswa kumsaidia iwe upande wa baba au mama hivyo kupelekea wajomba, mashangazi, bibi, babu na ndgu wengine kushiriki katika ukuaji na masomo yake.

Akifanikiwa huyu huo mzigo anaokua nao unakua si wa kitoto, watoto wa waliomsaidia nao watataka asaidie wenzie.
Kweli kabisa. Anakuwa na msalaba.
 
Nikweli lakin ikitokea mmetangana ,uyo atakaye baki nawatoto anatakiwa aishi nao kiakili awalele in way hawatapa mizigo baadaye.

Mbona watu walelewa na mzaz mmoja hasa mama nawamekuwa sawa tu nahawana mizigo...kama mzaz mmoja kazingua mwache wew uliyebaki pambana uzeeni watakufaa
 
Njia niliyo ona ni vyema kwangu

Mfano mke aki cheat sitamuacha nitamfanya tu house girl alele tu wanangu na chumba namuhamisha sitalala nae tena sitamfukuza

Na sitaleta mwanamke ndani nisije vunjia wanangu heshima yao zidi ya mama yao
Nitakuwa napiga mechi nje


Hiyo kwangu naiita win win situation

Au mfasihi una wazo tofauti ?

unifanye house girl wa wanao wakati we unawaza hivyo mimi nitaondoka mwenyewe na watoto wangu ili nikupishe uishi vizuri
 
Nikweli lakin ikitokea mmetangana ,uyo atakaye baki nawatoto anatakiwa aishi nao kiakili awalele in way hawatapa mizigo baadaye.....
Mbona watu walelewa na mzaz mmoja hasa mama nawamekuwa sawa tu nahawana mizigo...kama mzaz mmoja kazingua mwache wew uliyebaki pambana uzeen watakufaa

Uliwahi kuishi na Wazee ukaona HAO watoto wanaowafaa wazazi wao?
 
Back
Top Bottom