Mnapotengana mnawapa mzigo mzito watoto sio tu wakiwa wadogo bali hata wakiwa watu wazima

Watu wote wenye akili huchukulia familia Kama Jambo kubwa la maana.
Mleta mada hivi wazungu na sisi watu weusi Nani mwenye akili? Huoni kwamba twahubiri na kukitukuza kitu (ndoa) ambacho hakiwezekani na tayari kmewashind hata wenye akili(wazungu)?

Sisi kinachotutesa ni unafiki. Ndoa zimetushinda lkn hatutaki kukubali kuwa zimetushinda. Tunaingia kwenye ndoa kwa kukifanya tunafuata taratibu za maadili (Mungu) wakati hakuna chochote.
 
Mleta mada hivi wazungu na sisi watu weusi Nani mwenye akili? Huoni kwamba twahubiri na kukitukuza kitu (ndoa) ambacho hakiwezekani na tayari kmewashind hata wenye akili(wazungu)?

Sisi kinachotutesa ni unafiki. Ndoa zimetushinda lkn hatutaki kukubali kuwa zimetushinda. Tunaingia kwenye ndoa kwa kukifanya tunafuata taratibu za maadili (Mungu) wakati hakuna chochote.

Wazungu wenye akili walishakufa, hawa waliobaki ni masalia wanaoishia ishia.
Subiri uone kinachoenda kutokea.

Wazungu wanajijua uwezo wao ni duni ndio maana wanapigana kufa kupona kukandamiza jamii zingine.

Ila Kwa tulipofikia Anguko lao washalikaribia, wewe jionee mwenyewe.

Akili ni kuilewa Nature inataka nini na sio kwenda Against Nature.

Wazungu wanaelewa Nature inataka nini katika mambo mengi lakini wanajifafanya hawaielewi linapokuja suala la Ndoa na mambo ya demokrasia.

Endelea kutazama nini kitatokea, ni ANGUKO tuu
 
Isingefaa watu watengane wanaoumia ni watoto hata kama ni wakubwa Wana miji yao. Muunganiko wa familia unayo baraka na kuna nguvu fulani ya kiroho toka juu, mkitengana mnatengana pia na ile nguvu toka juu. Ingekuwa ni vyema watu waishi pamoja hata kifo sema tu ndo hivyo mitihani isiyovumilika na wengi hawana elimu kuhusu Roho. Roho ndio uongoza KILA kitu ukiitibu roho suala la talaka ni ndoto.
 
Talaka ni laana. Talaka ni roho ukitataliki umefungulia roho ya kutalikiana kwenye uzao wako ni lazima nao wataachana labda uwe na maarifa jinsi ya kukata connection na hio roho.
 
Mzazi yeyote mtoto wake sio wake yeye ni mlezi wa ndoa wa mtoto wake. Mtoto wako ni mme au mke wa mtu kile anachokiona kwako au unachokijaza kwenye makuzi yake ndio anakwenda kukipractice kwenye ndoa yake, so mzazi ndie anajenga au bomoa ndoa ya mtoto wake.

Kama mzazi ni mtaliki atashindwa vipi kumwambia mwanae achanae nae huyo si una Kazi yako mbona wapo wengi asikubabishe. Wakati mwingine sio sahihi Sana kuingia kwenye ndoa na mtu ambae wazazi au kwao kuna roho ya talaka waliotalikiana ile ni roho inafatilia labda tu mtu awe matured, yaani anaendeshwa na akili na sio roho means anaejitambua.

Mtoto umleavyo ndivyo atakavyokuwa labda tu apate Neema ya kuwa na elimu ya utambuzi kuhusu nini maana ya maisha ambayo wengi awapendi kutafuta maarifa bali uongozwa na matukio au upepo mfano kucopy toka kwenye tamthilia au marafiki wapotoshi, maana lengo kuu la tamthilia zote duniani bila kujali lugha iwe za kichina, kiswahili, english, korea, nk agenda kuu nyuma yake ni kubomoa familia iwe director anajua au ajui siri behind, shida wanawake wengi hawana uwezo wa kutofautisha kitu halisi na kisicho halisi wao ucopy na kupractice kwenye ndoa zao, then ndoa inavunjika kwa mikono yao wenyewe then wanaenda tena kumlilia Mwamposa awarejeshe ndoa zao kupitia upako.
 
Ni kanuni ya asili vitu upata moto wakati mwingine Ingekuwa ni busara watu wapeane distance yaani kukaa mbalimbali kwa mda maalumu inaitwa kipindi cha matengenezo au ujitafakari hadi joto litakapoa then mnaungana tena japo hii ni hatari pia maana kipindi hicho ni rahisi kupata faraja kivuli ukatekwa jumla.

Faraja kivuli ni kitendo cha kusahau shida zako kwa mda yaani unapata faraja ya mda toka kwa mtu anaejua yanayokusibu kwenye mahusiano yako na anatumia kipindi hicho kukuvuna kipesa au kingono kutimza haja zake za kipesa au kingono then nae akishapata hitaji lake ukumwaga.

Hii wanatumia Sana michekupo hasa makahaba kuwanasa wanaume za watu wenye pesa kwa kuwapa au kuwahadaa faraja au riziko au penzi bandia Ili kuteka akili ya mwanaume hapa ndipo mme uona kapata mtu sahihi anaemliwaza atatekwa ndio unasikia mtu katekwa na kahaba katelekeza familia kaloea huko huko baada ya kukimbia kelele za mke wake.

Pia hata wanawake nao upata mikasa ya faraja kivuli, wapo wanaume Kazi yao kutongoza wanawake wenye migogoro kwenye ndoa zao Ili wapate cheap ngono kwao kuwapa wanawake faraja bandia ambayo wameikosa kwenye ndoa uwatumia kingono wakisharidhika uwatupa wanawake hao.
 
Ukijiona una tatizo lolote shugulika na roho, Roho ndio inaongozwa mwili Roho ikiwa chafu ndo chanzo cha vurugu zote nje ya mwili. Wapo wataalamu wanadili na kusafisha Roho na ukapata balance nzuri ya maisha ukaweza jisimamia mwenyewe pasipo kutegemea ukamilisho toka nje yako.
 
Wanawake wengi ubomoa ndoa zao kwa midomo yao.
Wao ndio chanzo cha uasherati yaani mume kuchepuka, upungufu wa nguvu za kiume yaani mume akiwa ndani nguvu hamna akienda nje zipo yote chanzo ni mdomo, kauli chafu, maneno machafu yote haya wanaiga kwenye tathmilia na lengo kuu la tamthilia ni kubomoa ndoa ajenda ya siri.
 
Back
Top Bottom