Mnaponogewa kukusanya kodi na tozo kwenye gesi ya kupikia, kumbukeni pia kujiandaa kukabili athari za kimazingira

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
13,405
19,067
Kutokana na kupanda bei kwa gesi ya kupikia hivi sasa kuanzia alfajiri pilikapilika za bodaboda zilizobeba mafurushi ya mkaa mithili ya fuso zimeongezeka kwa spidi ya kimbunga. Hii inaashiria kwamba asilimia kubwa ya familia zilizokuwa zimeanza kutumia gesi zimerudi kwenye matumizi ya mkaa.

Wote mnajua vipato vya watu hasa watumishi vilivyoyumba miaka zaidi ya saba bila nyongeza za mishahara. Sasa bidhaa na mahitaji yote muhimu ikiwemo vifaa vya ujenzi, gesi ya kupikia, mafuta kama nishati ya kusafirisha bidhaa muhimu nk.

Vinapopanda huku vipato vya watu vikipungua au kubaki palepale miaka nenda rudi unasababisha mambo kama haya ya watu kurudi kwenye matumizi ya mkaa kama chanzo nafuu cha nishati.

Kwa hiyo mnapokopa mikopo fikirieni pia kukopa pesa za ku subsidize nishati ili kuepuka jangwa na athari za ukosefu wa mvua utakaosababisha janga la njaa.

Nawasilisha...​
 
Back
Top Bottom