Mnapomwaga damu za ndugu zetu leo,ifikirieni kesho yenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnapomwaga damu za ndugu zetu leo,ifikirieni kesho yenu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Hunter, Aug 30, 2012.

 1. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Dhuluma na ubaya huzunguka, na mwisho hujikuta unawafikia hata wale wasiotarajiwa na hapo ndipo haki huonekana ni lazima
  Alipouliwa yule mtendaji wa kata kule Arusha serikali ilipiga kimya as if ni kamnyama flani hakana haki...
  Walipouwawa wafuasi wa CDM kule Igunga serikali hii hii ilipiga kimya na mpaka leo haijasema lolote..
  Alipojeruhiwa yule kada wa CDM kule Arusha akaokotwa siku ya pili akiwa hajitambui mtaroni still serikali haijasema cha uchunguzi wala nini...

  Leo tunavyoshuhudia vifo vya raia wenzetu, walipa kodi, wenye uchungu na nchi yao wakiuwawa na polisi ama weusi wenzetu inatia hamasa,....Lakini tukumbuke yenye mwanzo huwa na mwisho,.. kesho watauliwa watoto ama jamaa zao najua hapo ndipo watakapohisi uchungu kama tunaouhisi sisi... polisi hana mamlaka ya kumuua yeyote yule hata kama ni mwenye makosa kiasi gani, polisi si hakimu wala hajasomea sheria inayompa uhalali wa kuhukumu na kuua raia walio katika nchi yao.

  Leo sisi tunakubali kulia.. kesho nyie mtalia mara mbili yetu maana kama jamii kandamizwa tutazoea,tutachoka na tutaamua kulipa kisasi maana mnapoishi tunapajua, ndugu zenu na watoto wenu tunawajua na kupishana nao kila wakati

  Kuweni na moyo wa huruma kwa hawa mnaowaua leo kwa dhuluma..
   
 2. G

  Geru Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Well said!
   
 3. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  ndo maana mi nasema hili li serikali la ccm jamani hili!!!!!!!!!!!!!!!!!!aaaaaaaaarrrrrrrrrggggggggghhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!


  Tuendeleeni kuwaelimisha watanzania, waelimike ili waliondoe madarakani hili li serikali la ccm magamba/mafisadi/majambazi/wauaji.
   
 4. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  ndo maana mi nasema hili li serikali la ccm jamani hili!!!!!!!!!!!!!!!!!!aaaaaaaaarrrrrrrrrggggggggghhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!


  Tuendeleeni kuwaelimisha watanzania, waelimike ili tuliondoe madarakani hili li serikali la ccm magamba/mafisadi/majambazi/wauaji.
   
 5. S

  SASTONI Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  hayo ni mawazo yako na si mawazo ya watanzania zaidi ya milioni 40 na mawazo hayo hayana mashiko...wewe hujasomea upolisi hiyo ni kazi yao waacheeee.katika kazi za kudhibiti uhalifu lolote linaweza kutokea ikwa nipamoja na kifo si lengo la polisi na hawapendi vitu hivyo vitokee.walitumia reasonable force vinginevyo maafa makubwa yangetokea.Mmelishwa Chuki dhidi ya Polisi ili kuwarahisishia njia wenzenu ambao watawatelekeza jangwani.siku zote Polisi hawezi kupendwa na watu wote pia hawezi kuwafurahisha watu wote mpo mnao zuiwa kufanya uhalifu mnawachukia polisi hakuna namna ni lazima mshughulikiwe kwa mujibu wa sheria mlizo zitunga wenyewe.


  Leo tunavyoshuhudia vifo vya raia wenzetu, walipa kodi, wenye uchungu na nchi yao wakiuwawa na polisi ama weusi wenzetu inatia hamasa,....Lakini tukumbuke yenye mwanzo huwa na mwisho,.. kesho watauliwa watoto ama jamaa zao najua hapo ndipo watakapohisi uchungu kama tunaouhisi sisi... polisi hana mamlaka ya kumuua yeyote yule hata kama ni mwenye makosa kiasi gani, polisi si hakimu wala hajasomea sheria inayompa uhalali wa kuhukumu na kuua raia walio katika nchi yao.

  Leo sisi tunakubali kulia.. kesho nyie mtalia mara mbili yetu maana kama jamii kandamizwa tutazoea,tutachoka na tutaamua kulipa kisasi maana mnapoishi tunapajua, ndugu zenu na watoto wenu tunawajua na kupishana nao kila wakati

  Kuweni na moyo wa huruma kwa hawa mnaowaua leo kwa dhuluma..[/QUOTE]
   
 6. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [/QUOTE]

  Huyu kijana wa Morogoro alikuwa anajisomea magazeti. Ameuawa kama kuku bila kosa lolote lile. Wako watu wengi sana wenye story kama hizi. Kumbuka wale wafanyabiashara wa Ulanaga. Kumbuka Munishi wa Bomang'ombe. Kumbuka Dr. Ulimboka. Usimtetee shetani kwani ipo siku atakufikia hata wewe. Kilio cha watu hawa ni kikubwa. Kumbuka wazazi wao na ndugu zao. Acha ujinga hawa polisi wanageuka kuwa wauwaji na sii walinzi wa raia na mali zao. Ukweli ni kuwa watanzania wanamlilia Mungu na ipo siku kilio chao kitamfikia masikioni pake.
  Kuisingizia CDM ni kujisingizia wewe mwenyewe. Hata watoto wa Primary school walilalamika na kuandamana kudai haki zao. Hii ni serikali ya wapi ambayo hata mtoto anaiona haifai? Kama tungalikuwa na serikali ingalikemea haya madudu. Ni kwa nini inasema uwongo kana kwamba watu hawaoni kama inahusika?
  Kama hawa polisi wamesoma, wanatudhirishia kila siku kuwa hawakusomea maadili ya kazi yao. They have no idea what they are supporse to do in terms of ethics. They are the most corrupt people in the whole nation. Tunaamini CDM italifumua hili jeshi insideout na kuunda jeshi lenye polisi wachache wanaoheshimu utu wao na wa watu wengine. Tumechoka sana na umwagaji damu huu wa ndugu zetu wasio na hatia. Tumechoshwa pia sana na serikali hii iliyojaa usanii mtupu!!!!!
   
Loading...