Mnapoibuka watu wa kumsafisha na kumtetea Ole Sabaya hamuoni aibu? Tuhuma za utapeli zimeanza leo?

Inawezekana ni Mr. Baya mwenyewe huyo ndani ya JF. Mijitu mingine bana Sijui Bob Jiwe anaiokotaga wapi. Nawaza hapa pengine ndio "Ndege Wafananao,....... "
Inawezekana! Halafu sasa jinsi Sabaya na lenyewe lilivyo kubwa jinga linajitetea kama mganga wa kienyeji, halina hata common sense.
 
Ndivyo alivyo ndugu yangu wala hujadanganywa hata kidogo. Sabaya kaanza starehe muda mrefu zana. Tukisema sisi tunaomfahmu tunaambiwa ni siasa, bora ninyi mnamsikia msema. Huyu DC sio wa kufanya kazi na JPM,hawaendani.
Hapa juzi kati situliletewa habari ya kupata ajali akiwa na mke wa afisa usalama tena wakitoka kununua gari Dar huyu mtu siyo mstaarabu kabisa hata sura yake inaonyesha haaminiki
 
Mi nawaza tu kwa sauti,kama mfanyabiashara mswahili amefanyiwa hivyo je wale wageni wenye mashamba ya maua na parachichi wanakamuliwa kiasi gani!?
 
Sabaya anakazi ngumu ya kupambana na wakwepa kodi ambao ni matajiri wakubwa mno ndani ya hai.Uzi wa kipuuzi kama huu haumrudishi nyuma ng'o.
AMEKUWA TRA? VIJANA WENGI WALIOWEKWA MADARAKANI NA JIWE NI WAHUNI NA WEZI NI WALA RUSHWA WAKUBWA NA WANATUMIA UKARIBU NA MALAIKA MKUU KUJIPATIA PESA ISIVYO HALALI, KUNA DC MMOJA PAMOJA NA KULIPWA POSHO YA NYUMBA ALIPANGA NYUMBA KULIPA IKAWA SHIDA MPAKA MWENYE NYUMBA ALIPOTISHIA KWENDA KWA MKUU WA MKOA. NADHANI IFIKE WAKATI MAMBO MAKUBWA YANAYOHARIBU TASWIRA YA MTANZANIA NA NCHI YAKE TUYAKEMEE.
 
Misukule ya mbowe mnajitoa ufahamu mkuu wa wilaya ndiye msimamizi na mwenyekiti wa kamati ya mapato na matumizi swine.
Awe mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya, hapo hapo awe mwenyekiti wa kamati ya mapato na matumizi ya wilaya? Kweli? Na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya anasimamia nini? Mwenyekiti wa halmashauri ndiye kiongozi wa baraza la madiwani ambao ndiyo inayosimamia mapato na matumizi wilaya.
Kwanza DC mwenyewe hanaga mafungu, hata hela ya mafuta ya gari anaendaga kumpigia magoti DED, afu hapohapo ni msimamizi wa matumizi ya wilaya? MAHANJU tutafutie hizi facts tafadhali, tusilishwe matango pori na hawa wahunihuni.
 
ni upumbavu mtupu. Sabaya si kuvumbia macho.
 
Misukule ya mbowe mnajitoa ufahamu mkuu wa wilaya ndiye msimamizi na mwenyekiti wa kamati ya mapato na matumizi swine.
Pumbavu kabisa.Akili za kizombie kabisa.Ok mkti ya ulinz na usalama kwa hyo yy ndo anaenda kùkamata wahalifu au polisi?Vijana wa Lumumba ni wanàfiki had shetan anawashangaà.Na makonda style ndo njia ya ķukušanya kodi?
 
Sabaya anakazi ngumu ya kupambana na wakwepa kodi ambao ni matajiri wakubwa mno ndani ya hai.Uzi wa kipuuzi kama huu haumrudishi nyuma ng'o.

DC kazi yake ni kufuatilia kodi au ni sehemu ya TRA? Au siku hizi ma-DC wanapewa access kwenye server ya TRA ili kujua ni nani kalipa au hajalipa kodi? Atajuaje kuwa A kalipa lakini B bado hajalipa?
 
Ninawashangaa sana watu mnaotokwa mapovu kumtetea huyu Sabaya ni kwa vile hamumjui tu. Endeleeni kuingiza siasa kwenye mambo ya msingi ili aendelee kula pesa za watu.

Kuna mambo mengine ya hovyo sana, hamwezi kujiuliza huyu mfanyabiashara kachoka kiasi gani mpaka kufikia kulalamika?
Kwani Sabaya akiondolewa mbafikiri DC mwingine atakayepelekwa Hai atatoka CHADEMA? Yaani kila kitu siasa tuu badala ya kuangalia content na mazingira na kisha kutazama historia ya Sabaya.
Hii Makonda style huyo mfanyabiashara kaijulia wapi? Kwanini serikali ambayo tunajaribu kujipambanua kwa rushwa tuchekelee hii hatari? Kabla ya Sabaya hakukua na DC?

Kwa bahati mbaya sana nimekua ndani ya kamati mbali mbali za CCM mkoa wa Arusha kabla sijaondoka na mzee wangu EL, Sababya sio mtu msafi tusitumie nguvu nyingi kutaka kumsafisha. Possibility yangu ni 100% kua amepiga hizo pesa. Sina ukaribu na Mbowe,hanijui na wala simjui tusiingize siasa kumhusidha yeye.

TAKUKURU watende haki kupitia yule mfanyabiashara watajua kila kita kitu, hata yule msanii aliyekua anasumbuliwa usiku kucha pia ni shahidi msiume maneno hamjui mambo.

Kwa taarifa yako anayetetea hapo siyo Sabaya bali mamlaka iliyomteua! Ikitokea leo mamlaka ikajitenga naye yanaweza hata kufanyika maandamano ya kuipongeza! Hivyo ndivyo tulivyoporomoka.
 
Back
Top Bottom