Mnapoendelea na Siku Tatu za Maombi, Msisahau Kusoma Aya Hizi

Filipo Lubua

JF-Expert Member
Nov 18, 2011
339
578
Mnapoendelea na siku tatu za maombi, msisahau kusoma aya hizi:
"Kumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu. [kwa hiyo] kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote na hamkukubali karipio langu, mimi nami nitawacheka katika maafa yenu, nitawadhihaki wakati janga litawapata kama tufani, wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli.... Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu; watanitafuta lakini hawatanipata, watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa matunda ya hila zao. Kwa kuwa ukaidi wa wajinga utawaua, nako kuridhika kwa wajinga kutawaangamiza. Lakini yeyote anisikilizaye ataishi kwa usalama, atatulia, bila kuwa na hofu ya madhara.” (Mithali 1:7, 25, 26, 28, 31-33 NEN)
 
Serikali imetangaza ongezeko la wagonjwa wengine wapya 53 na sasa jumla ya walioambukizwa Tz ni 147. Hawa 53 wapya, wikiendi ilopita, mlikuwa nao huko makanisani, misikitini, vijiweni, baani, na kungineko? Kama walikuwa huko, waliambukizwa na nani? Nao wameshawaambukiza wangapi? Idadi halisi ya waliombukizwa sasa ni ipi?

Halafu mnataja maombi! Dharau iliyoje kwa Mungu!. Kuna wachungaji na viongozi wa dini wengi ninaowaheshimu sana kwa kazi kubwa ya kiroho wanayoifanya, na ninajua wanaombea nchi yetu sana. Ila mniambiapo hata watu kama Gwajima nao wataongoza sala kwa siku tatu hizi, napigwa na bumbuwazi. Majuzijuzi tu Gwajima aliitukana WHO kwa kuitahadharisha Tanzania na nchi ngingine za Kiafrika kuhusu COVID-19. Akizungumzia onyo la WHO kwa nchi za Kiafrika, Gwajima alisema "Nataka kukuambia hivi, Tanzania haimo! Aliyeitaja Tanzania amtaje baba yake mzazi! Aliyeitaja Tanzania amtaje mkewe! Aliyeitaja Tanzania ataje wanae!..." Mtu anayeitwa wa kiroho anatumia jina la Mungu kuporomosha matusi yote hayo. Hata hivyo, Korona haikumsikia, ikaingia tu na sasa wamekufa wenzetu 4, na wengine 147 wameshapata maambukizi.

Mnaponiambia taifa litakuwa katika maombi yakiongozwa na 'wachungaji' kama Gwajima, nashindwa kuelewa ni maombi gani tunapaswa kuyafanya! Hata hivyo niwaulize, kwani hapo kabla mlikuwa hamsali? Na tena, tushindwe kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima (jambo ambalo ni la kimwili na rahisi sana), tutaweza ya kiroho kama kufunga na kuomba kweli? Tusalini sana, ila tukumbuke kuwa tusipokwepa mikusanyiko isiyo ya lazima, Mungu atatuacha tuangamie katika ukaidi wetu. Juzi nilikuulizeni, 'vipi mbona mwamfanya huyo mungu wenu aonekane kama mganga fulani wa kienyeji toka Sumbawanga'? Oneni sasa majirani zetu watutukanavyo kwenye mitandao ya kijamii! Shame on us!
#Tuelimishane #COVID19
 
Hivi kuna sehemu tamko limetaja maombi lazima yafanyikie kwenye nyumba za Ibada? Au limesema tu kuomba?
 
Kila watu wasali majumbani kwao
 
Hapa tunatakiwa kuchukua tu hatua za kujikinga dhidi ya huu ugonjwa! Kwa sababu wahusika waliotuletea ni Wachina! Na sijui waliwaza nini wapumbavu wale.

Hivyo kutoa tamko la kufanya maombi eti kwa siku tatu! sidhani kama ni jambo sahihi sana. Mambo ya kisayansi ni vyema yakatatuliwa kwa njia za kisayansi badala ya kutumia njia a kiimani ambazo huwezi kuzithibitisha kisayansi.
 
Hata Yesu alidhihakiwa sana wakati wa Mateso baada ya kufufuka mahasimu walitoweka kama upepo.
Wekeni akiba ya maneno yenu.
 
Back
Top Bottom