Mnaotumia/mliowahi kutumia sola za zola naombeni ushauri

UMUNYU

JF-Expert Member
Jan 28, 2017
685
484
Mimi ni mtumiaji mgeni wa Zola, kwa muda wa wiki sasa huduma yao inanisumbua,betri haijai.Taa yao wanayoita ya ulinzi inawaka masaa 24 ambayo waliniahidi kuwa itakuwa inajiwasha jioni na kujizima asubuhi.

Ajabu hata waliponielekeza pa kuzimia haizimi.Waliniahidi kumtuma FUNDI wao aje anirekebishie lakini imekua si kweli.

Kwa nyie mnaowafahamu hawa watu huduma zao zikoje?Mbona wameanza kunilaza gizani pamoja na kuwalipa hela ndefu?
 
Mm pia ni mtumiaji na nilimalizana nao ila kwa Sasa umeme umeshafika

Kiukweli wako vizuri,huduma kwa wateja pia wako vizuri ila kwenye betri linaweza kutokea tatizo lakini ukiwasiliana nao na kuwajulisha wanakubadilishia lingine ambalo litakuwa vzuri kabisa

Mm katika jamaa wa umeme wa jua hawa nawakubali Mia mia.

Ingawa kukuhaidi fundi atakuja na asifike huenda ni mattzo ya kibinadamu tu maana mafundi wao unakuta wamewatrain ma agent wa humohumo ambao hawatoki mbali ili wawahudumie kwa wepesi,Sasa fundi akiwa na dharura hawez kufika kwa wakati...usijisikie vibaya endelea kuwajulisha watakusaidia

Mm nilichukua ule mtambo wa tv,redio,taa 5 mkataba wao miaka 3 nilimalizana nao vzr na kila kwenye tatzo walinisaidia vizuri ingawa changamoto ndogondogo zipo.

Ila kiukweli jamaa wako vizuri kwenye Mambo ya solar na pazur zaidi ukiwapigia wanna ushirikiano mzuri.

Mpaka Sasa natumia mtambo wao Kama back up umeme wa tanesko ukizingua na sijawahi kuona ubaya wao mkuu.
 
Hiyo taa ya ya ulinzi ni ile kubwa ambayo ikifika jioni inajiwasha yenyewe,ila kwa inavyoonekana wewe battery yako iko na matatizo wakubadilishie maana betri mara nyingi ndio huwa zinazingua endelea kuwapigia ama wafuate ofisini kwao mkuu mm Nina mwaka wa tano Bado natumia vitu vyao viko gud sana nisiposema ukweli wa huduma niliyotumia nitakuwa na roho mbaya.ila battery hata mm ilibidi nibadilishiwe maana ilifika wakat haijai mpaka 100 na inazima haraka baada ya kuripoti nilibadilishiwa chapu.
 
As

Asante sana kwa ushauri,nitaufanyia kazi
 
habarini naomba mwenye contact za ZOLA OFFGRID TANZANIA anisaidie nina jambo nao lakini cjawezakuona contact zao kwa website yao kama namba za simu
 
Back
Top Bottom