Mnaotarajia kuoa au kuolewa chukueni tahadhari mapema usijejuta

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Ewe mwanaume ukioa mwanamke:

  • Mrefu, jua kwamba utaoa mwanamke mpenda maendeleo, mchapa kazi na mkarimu ila hawajui mapenzi na ni wavivu kujiweka safi kimazingira.

  • Mfupi kiasi, jua ya kwamba utaoa mwanamke mchangamfu na mpenda elimu sana ila tu wanapenda mnongono na hawaridhiki.

  • Mfupi kabisa.Jua ya kwamba utaoa mwanamke msikivu na mcha Mungu ila ni waroho kwa kula na wabishi sana.
Ewe mwanamke ukiolewa na mwanaume:

  • Mrefu, jua ya kwamba utaolewa na mwanaume mwenye upendo, utu na ubinadamu ila ni wabahili mno na hawapendi kupendeza.

  • Mfupi kiasi, jua ya kwamba utaolewa na mwanaume mwenye fikra na akili timamu za maendeleo, mbunifu, mcheshi na fundi wa mahaba ila ni wapenda ushirikina sana, wana wivu na wambea sana na mara nyingi hupenda kupiga chabo kwa watu wanaofanya mapenzi.

  • Mfupi kabisa, jua ya kwamba utaolewa na mwanaume mwaminifu, msikivu, mnyenyekevu ila huwa wepesi wa kujiua, kukata tamaa upesi, wanawivu sana na hawapendi kuoga.
Nawatakieni kila la kheri wale wenye wapenzi na ambao mnajiandaa kuoa au kuoelewa ila zingatia sana tabia hizo hapo juu za huyo unayetegemea kufunga nae pingu za maisha ili usije kutusumbua baadae. Chukueni tahadhari!
 
Chanzo cha utafiti wako tafadhali, na sio kukurupuka kwa kufanya majumuisho ya wale wachache unaowajua. Mke / Mume bora, safi, mwema, mtiifu, msikilizaji, Mcha Mungu, kumpata ni kuanza kwa kusugua goti kwa kumuomba Mungu, na siyo Illusions kama zako hizo.

Ahsante!
 
Subir na mm ntakuja nautafiti wangu maana naona ishakuwa shida na hzi tafiti sasa
 
Ungetaja vipimo halisi ili tujue na tuwapime kwa futi kabisa maana hujaeleza urefu na ufupi kiasi gani.
 
Tafiti nyingine jamani ni mtihani mtupu.usikute hao ni wake/waume wa ndugu zake wenye tabia hizo basi tafitu yake ikaishia hapo maskini weee.
 
Back
Top Bottom