Mnaotaka mikataba iende bungeni mnaonyeshwa kinachojadiliwa bungeni leo?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Wapo watu wanataman mikataba ipelekwe bungeni huku wakijua wazi kuwa Bunge letu halipo live kwa wananchi na hakuna anayejua wanajadili nini ila tunachojua ni kile tu wanachoona kinafaa ndicho kinaletwa kwetu.

Lakini pia huko Bungeni Kuna wabunge wakusoma mikataba au Kuna wabunge wakuunga mkono hoja? Kama miswada ya kawaida tu haipati mijadala mizito je mikataba ambayo inamisukumo ya wawekezaji bungeni ndo tutapata michango chanya?

Naamini hata mikataba ipelekwe bungeni bila kuwa na Bunge huru na lenye wawakilishi huru Bora ibakie kuwa Siri ya ikulu na ofisi ya AG
 
Back
Top Bottom