Mnaotaka kufanya kazi na wanaojiita Nickshine Media Production kuweni makini sana

mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
10,809
2,000
Nachokiona kama point ni ufike shekilango toka ubungo mataa ila umezungukia ubungo>mwenge>bamaga>sinza>shekilango!

Umezunguka sana yani make your point clear...

Umelipa hujapewa picha? Picha zmepigwa vibaya? Baadhi ya vitu kama Tv Screens setups hazikuwepo ukumbini?
Hata mimi nimejaribu kumwelezea mlalamikaji ni kama anapiga porojo haelezi uhalisia wa tatizo ni kama anataka kumkomoa aliyempiga picha ,haelezei tatizo ni kama anazunguka tu mbuyu haileweki point yake nini?
 
mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
10,809
2,000
Pia tatizo ni kuwa wapigwaji picha wao wenyewe huwa na tatizo,nimeshuhudia vikao vingi vya harusi ,utakuta wanakamati wanakuwa na interest zao kwenye hizi sherehe za harusi na bahati mbaya mwenye harusi anazidiwa nguvu na wanakamati ,wanakamati wao ndio hufanya maamuzi mengi ikiwemo kuchagua watoa huduma lakini nyuma ya pazia hao wanakamati ndio wanakuwa na watu wao au ni wao ndio huchukua tenda za shughuli nzima za harusi,unaweza kuambiwa mpiga picha au mshereheshaji kalipwa milioni 2 kumbe si kweli na mwisho kujitangaza au ukubwa wa kampuni sio kwamba ndio kujua kazi,hizi studio kubwa mara hyingi nazo hukodi wapiga picha kwani utakuta kwa wiki wana harusi kama 3 kwa hiyo inabidi ''wawavalisha tisheti'' watu ambao ni wapiga picha wa kawaida sana,lakini pia wapigwaji picha tunapenda sana bure na bure ni aghali, ni muhimu kuwa na mikataba ambayo inaonyesha ni picha ngapi zitapigwa ni picha za aina gani ni wahusika wapi wapigwe picha , muda wa kazi , location ,pre wedding, n.k pia timeline ya kuedit kazi na kupewa, haki ya picha zako kwa mfano kuwekwa au kutowekwa mitandaoni bila idhaa yako, kupewa au kutopewa RAW files (mara nyingi mteja hupewa JPEG file tu, kwa kuwa mteja akipewa RAW file anaweza kupeleka kwingine kuedit na picha zikawa tofauti halafu akarudi mbio kukulaumu uliyempiga picha. bado tuna safari ndefu kwenye hii tasnia,hii tasnia imekuwa sawa na bodaboda.
 
ashera

JF-Expert Member
Aug 3, 2020
326
1,000
So namfahamu NICK, aliwahi kufanya Wedding ya Rafiki yangu mwaka huu hapo Dar es Salaam. ALIFANYA KAZI HIYO KWA UBORA NA UAMINIFU
Nilipoona hii post niliamua kumtafuta sikumpata, lakini rafiki yangu ambaye alifanya naye kazi alimpata na kumuuliza kuhusu Uzi huu ulioweka.

Ndugu, uzi wako una kasoro na viashiria kwamba UNATAKA TU KUMCHAFUA NICK KWA SABABU ZAKO. Kasoro hizo ni;

1. Huelezi Nick kakukosea nini haswa. Uko too general husemi ulichofanywa.

2. Umetanguliza kujihami kwingi kwamba huandiki kwa nia mbaya, ilinipa hofu kuona kwamba unaweza kuwa na nia mbaya. Umemaliza pia kwa kusema utaletewa povu, why uletewe povu kweny jambo hilo?

Nicki amejieleza na kuomba wanajamvi wapime mambo yafuatayo:

1. Yeye sio biashara ya mtandaoni ambayo mtu anaweza kupata tabu kuifahamu. YEYE NI KAMPUNI, INA OFISI ZAKE ZIKO SINZA. Hivyo kama kweli una malalamiko kwake, ni rahisi kabisa kumkamata na kufungua kesi. So fara Ofisni kwake hakuna malalamiko ya hivyo unavyosema kwamba eti unashindwa kumpeleka mahakamani.

2. Nicki anahusisaha suala hili na vita za kibiashara kwa sababu YEYE ANAJITANGAZA SANA NA KUTOA HUDUMA KWA BEI NAFUU jambo ambalo washindani wake kwenye biashara linawakera sana. Mnaungana kumpiga vita.

3. Nicki amehusisha hili na TUZO, mnajua wenyewe mambo yenu ya tuzo ambazo mwaka jana Nicki alishinda. Mwaka huu tena yuko Nominated, hivyo kuelekea tuzo hizo mmeanza kuwekeana fitna.

MSICHAFUANE, MWENYE MALALAMIKO YA KWELI TUAMBIE ULIFANYWA NINI, NICKI YUPO OFISNI KWAKE TUELEZE KWA NINI HUJAMKAMATA?

Uzi wako una dalili zote za chuki za kibiashara, umekosa mashiko na ukweli wa hoja. ACHA.
Nick tulia watu wawa expose maana mmezidi utapeli
 
ladyfurahia

JF-Expert Member
May 10, 2011
14,301
2,000
Nachokiona kama point ni ufike shekilango toka ubungo mataa ila umezungukia ubungo>mwenge>bamaga>sinza>shekilango!

Umezunguka sana yani make your point clear...

Umelipa hujapewa picha? Picha zmepigwa vibaya? Baadhi ya vitu kama Tv Screens setups hazikuwepo ukumbini?
unajua ukitapeliwa unakuwa tofauti sijui kwanini hawa watu wanawatapeli wenzao kiasi hiki

hapo ana uchungu sana alivyotapeliwa ila najua umeshamuelewa mm mwenyewe nimetapeliwa sina hamu kufanya biashara na mtu ambaye mtandaonizimu
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
45,018

Yeah akili inakuwa alert mda wote ukishatapeliwaga! Inataka uaminifu sana biashara ya mtandaoni hii!
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
50,341
2,000
Mshona suti ambaye anaustaarabu angalau kwa upande wnagu naona ni Jm na Mtani kwakweli, wanazingatia muda wa kumaliza kazi ya mtu na hata kama pana excuse wanakujulisha, sitaki kukumbuka nilimsindikiza ndg yangu na kwa suti bega kushona suti ya shughuli yake yaliyotukuta tulikoma ni ahadi za njoo kesho njoo keshokutwa ikisindikizwa na kubadilishiwa aina ya kitambaa alichochagua na uzuri alipiga picha wakati anachagua .
Mnafanyaje kazi na mafundi wenye majina hivyo?

Mdogo wangu wakati wa send off, alienda shona suti speshoz, siku 2 kabla ya tukio hata kitambaa hakijakatwa.

Alienda polisi, kazi zote zilisimama, nguo ikashonwa usiku kucha. Asubuhi akaja fanya fitting.

Toka siku hiyo siwatamani hawa jamaa wenye majina, kazi mbovu hela nyingi.

Mtaani kuna mafundi suti wazuri sana na bei zao ndogo.

Juzi nilishona suti nzuri tu kwa 120k tena in time ikakamilika.
 
Mi nilishona kwa 70k tu
 
Ndu wa kweru

Member
Nov 18, 2021
5
45
Maisha ni kuinuana,hizi kazi zinafanywa na vijana wenzetu.Tunapowapa kazi ni ili mpate riziki ya kazi zenu,sasa mnaharibu kesho kazi zikija kufanywa na watoka mbali mnalalamika,kuna waaminifu ila tasnia yenu imeingiliwa na watu wa hovyo sana ,mtu anajali kula na kunywa na kutongoza tu wanawake.Kuna mmoja nilimpa kazi ya birthday tu,kaja mbwembwe kibao,mara light hazifanyi kaz,video anarekodia simu ya mualikwa,wiki mbili kazi haijakimilika,ikaletwa video bado,ni mwaka sasa kimya,kakiniona na begi lake kanabadili njia.Uaminifu una uza vijana na unalipa,kazi ya picha nayo tuwape wakenya kama wenye mahotel walivyoajiri mameneja wakenya?Maisha ni kuinuana ila mnakatisha tamaa.
 
reymage

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
1,668

Acha kabisa wanakatisha tamaa sana hawa vijana
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
24,984
2,000
Mnafanyaje kazi na mafundi wenye majina hivyo?

Mdogo wangu wakati wa send off, alienda shona suti speshoz, siku 2 kabla ya tukio hata kitambaa hakijakatwa.

Alienda polisi, kazi zote zilisimama, nguo ikashonwa usiku kucha. Asubuhi akaja fanya fitting.

Toka siku hiyo siwatamani hawa jamaa wenye majina, kazi mbovu hela nyingi.

Mtaani kuna mafundi suti wazuri sana na bei zao ndogo.

Juzi nilishona suti nzuri tu kwa 120k tena in time ikakamilika.

tena mtaani mtu akisikia una ndoa anatetemeka asijekuvurugia mambo.

hawa wa laki 7 hawa,inaonekana hawababaiki na kima.
 
mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
30,588
2,000
mengi yana connection,kitu ungeambulia hapo ni kurudishiwa hela nusu tu,unadhani mtu anaamka tu na kuanza kufanya upuuzi kwa watu!!!!
Hela yangu ingerudi yote.
Ningemchukua ndugu yangu mmoja.
tungewapigisha push up za kutosha.alafu ningewaambia kesho nakuja kuchukua hela zangu.
USIPENDE KUWA MNYONGE.
tusingewapiga ila cha Moto wangekiona .
 
storyteller

JF-Expert Member
Nov 5, 2014
1,437
2,000
Kwa ss vijana wengi kimbilio ni upiga picha, kazi isiyolazimu sana uwekezaji, so makanjanja wapiga picha wamekua wengi na wanachojivunia ni kuretach na kutumia filters.... ss na wabongo wengi wanaingia kwenye huu mtego... na machalii wako active sana mitandaoni.... na wanapost zile picha konk tu....

Ila yote kwa yote riziki anatoa mungu.
 
Maya Angelou

JF-Expert Member
Oct 19, 2019
861
1,000
Mnafanyaje kazi na mafundi wenye majina hivyo?

Mdogo wangu wakati wa send off, alienda shona suti speshoz, siku 2 kabla ya tukio hata kitambaa hakijakatwa.

Alienda polisi, kazi zote zilisimama, nguo ikashonwa usiku kucha. Asubuhi akaja fanya fitting.

Toka siku hiyo siwatamani hawa jamaa wenye majina, kazi mbovu hela nyingi.

Mtaani kuna mafundi suti wazuri sana na bei zao ndogo.

Juzi nilishona suti nzuri tu kwa 120k tena in time ikakamilika.

Duh kumbe hata speshoz msumbufu ♀️
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom