Mnaotaka Katiba Mpya nawapa hoja

Hivi wale mnaopingana na mawazo ya mwanzisha uzi tuwaeleweje?
Kwani anapinga dai la katiba?
Si ametoa na kwanini katiba mpya ni hitaji.
Wazo lake ni nani na kwanini anaipambania. Amesema WANASIASA basi.
Nakushukuru sana ndugu Omulasil kwa kunielewa maana kuna watu humu wanahama key ni balaa tupu.
 
Nahuo ndo ukweli ,hawa wafata mkumbo bila kujua wamelivalia njuga kumbe wanatumiwa kutekeleza plan za watu.

Kuna kundi kubwa sana ambalo ni takribani 70%-75 halijui wala halina habari na hiki kinachoendelea na hakuna hata mmoja aliyejitokeza kulielimisha hili kundi kubwa, ipo siku nalo litaibuka kudai katiba inayowajali wao nasio hii inayotafutwa na wasaka tonge
 
Asante sana mkuu Goodguy tatizo wengi wanaojadili hili swala wanajadili kichama sana na ukilichukulia hili swala kichama ndipo linakuwa gumu zaidi
 
Katiba mpya ni dai linalotokana na utashi wa kisiasa kwa kiwango kikubwa lakini pia ni zao la mwamko mkubwa wa wananchi kuchoshwa na namna wanavyoongozwa.

Na mara nyingi kuchoshwa huku lazima kutokane na kukata tamaa ya maisha kwa walio wengi lakini pia kupata mwamko mkubwa wa elimu ya uraia.

Bahati mbaya ni kwamba wapigania katiba wa sasa wanataka katiba iwasaidie kwenye mapambano ya kisiasa, ndio maana hii ajenda ni ngumu sana.
Watanzania tunataka maji, umeme, barabara, elimu bora! Kiujumla huduma za jamii ziboreke, sio eti Raisi ana madaraka makubwa, ni nk
 
Katiba mpya ni dai linalotokana na utashi wa kisiasa kwa kiwango kikubwa lakini pia ni zao la mwamko mkubwa wa wananchi kuchoshwa na namna wanavyoongozwa.

Na mara nyingi kuchoshwa huku lazima kutokane na kukata tamaa ya maisha kwa walio wengi lakini pia kupata mwamko mkubwa wa elimu ya uraia.

Bahati mbaya ni kwamba wapigania katiba wa sasa wanataka katiba iwasaidie kwenye mapambano ya kisiasa, ndio maana hii ajenda ni ngumu sana.
CCM ni chama tawala na chama tawala ni zaidi ya mwingereza alipokuwa hapa, mwingereza aliondoka bila kuacha majeraha na mauaji. Kutokana na CCM kuwa watawala wao ndio wanufaika wakubwa kwenye haki ya kujumuika huku wengine wakinyimwa haki hiyo na watawala, Polepole aliposema CCM itatawala zaidi ya miaka 100 ijayo hakusema kwa bahati mbaya bali alijua mtawala atatumia mkono wa chuma kuendelea kutawala.
 
Katiba mpya ni dai linalotokana na utashi wa kisiasa kwa kiwango kikubwa lakini pia ni zao la mwamko mkubwa wa wananchi kuchoshwa na namna wanavyoongozwa.

Na mara nyingi kuchoshwa huku lazima kutokane na kukata tamaa ya maisha kwa walio wengi lakini pia kupata mwamko mkubwa wa elimu ya uraia.

Bahati mbaya ni kwamba wapigania katiba wa sasa wanataka katiba iwasaidie kwenye mapambano ya kisiasa, ndio maana hii ajenda ni ngumu sana.
Well said mkuu, na Tanzania mambo mengi yako vizuri hivyo wanasiasa wasitake kutumia wananchi kama daraja lao kubwa kutafuta madaraka.
 
Hakuna katika historia mahali popote duniani ambapo katiba mpya ilikuja kwa watu tu kusema tunataka katiba mpya!! Katiba mpya ni zao la msuguano mkali sana wa kijamii ambapo watu walio wengi Wanaona hakuna namna tukaenda mbele bila kubadili katiba ilitokea hivyo zanzibar,2010, kenya, 2013, nk na kiuhalisia tukiandika katiba mpya kwa sasa inaweza kuwa mbaya kuliko iliyopo!
 
Sijui una umri gani lkn nadhani ukoo wenu mna laana si bure yani we mbuzi huoni umuhimu wa katiba mpya kwa hali tuliyo nayo kwl!!!!? Unaelewa kbs watz ni wanyonge kama alivowaita Magufuli yani hawawezi kujijitea,, sasa wanatokea watu wa kuona mbali wanadai katiba ni mbovu we unakinzana nao,,,Ebu fikiria jamii za kusini na hata kanda ya ziwa(sukuma) wanajua nini juu ya Rais kuwa kila kitu hapa nchini( mungu mtu) hapana shaka jamii kama hizi lazima wawepo watu ambao watatenda kwa ajili yao hasa kuhusu mambo ambayo kwao wala hawajui chochote zaidi ya kula,kulala na kusubiri kufa.Na ccm ndio furaha yao kuwa na watu short sighted kama hao.
mkuu acha matusi jibu hija kistaarabu, mbona wapinzani especially CHADEMA hua adabu kwenu mtihani kiasi hiki?
 
Mwanaccm toka lini akapenda harakati za katiba mpya??

Mlikataa hakuna corona, mkakataa Chanjo leo yako wapi?? Na katiba Mpya mtakubali tu.

Huu moto hatupoi.

Iyo Corona Na chanjo inauhusiano kwenye Katiba sio? Unapochangia weka mihemko ya Kiutopolo pembeni aisee mana utadhihirisha upungufu fulani ubongoni mwako
 
Hakuna katika historia mahali popote duniani ambapo katiba mpya ilikuja kwa watu tu kusema tunataka katiba mpya!! Katiba mpya ni zao la msuguano mkali sana wa kijamii ambapo watu walio wengi Wanaona hakuna namna tukaenda mbele bila kubadili katiba ilitokea hivyo zanzibar,2010, kenya, 2013, nk na kiuhalisia tukiandika katiba mpya kwa sasa inaweza kuwa mbaya kuliko iliyopo!
Ccm et al katiba mpya wapi na wapi?
 
Wakati mwingine tutakapoamua kuandika katiba mpya tume ya katiba iundwe na wataalamu tu wa katiba na sheria wenye umri kuanzia miaka 45 kutoka ndani na nchi za mbali zilizo na demokrasia ya juu.

Watu aina ya Polepole na Bashite wasihusike kuandika katiba tunayotegemea itatupeleka miaka 100 mbele. Tutafute magenius wa katiba na sheria.
 
Katiba mpya ni dai linalotokana na utashi wa kisiasa kwa kiwango kikubwa lakini pia ni zao la mwamko mkubwa wa wananchi kuchoshwa na namna wanavyoongozwa.

Na mara nyingi kuchoshwa huku lazima kutokane na kukata tamaa ya maisha kwa walio wengi lakini pia kupata mwamko mkubwa wa elimu ya uraia.

Bahati mbaya ni kwamba wapigania katiba wa sasa wanataka katiba iwasaidie kwenye mapambano ya kisiasa, ndio maana hii ajenda ni ngumu sana.
MADAI YA KATIBA MPYA YANATOKANA NA UKWELI KWAMBA KATIBA ILIYOPO IMEKIUKWA NA WAKATI KWA SABABU INAZUNGUMZIA MUUNGANO, WAKATI MUUNGANO ULIVUNJIKA ZANZIBAR ILIPOAMUA JUWA NA SERIKALI YAKE NJE YA MUUNGANO. KATIBA MPYA NI LAZIMA ILI KUIPA TANGANYIKA SERIKALI YAKE PIA AU KUVUNJA SERIKALI YA ZANZIBAR ILI KUWA NA MUUNGANO HALISI WA SERIKALI MOJA.
 
kwa taarifa yako katiba ni muhimu sio tu kwa ajili ya shughuli za kisiasa kama unavyotaka watu waone ila pia katiba ndio inayoelekeza au kuonyesha namna ya mwelekeo wa kiuchumi na kijamii wa taifa husika mfano Tanzania wakati inatengenezwa katiba ya 1977 tulikua kwenye uchumi wa kijamaa ambapo vyanzo vyote vya kiuchumi vinakua chini ya serikali/umma lakini kwa sasa Tanzania tuna uchumi mchanganyiko(mixed economy) ambapo Kuna mchanganyiko wa umiliki wa vyanzo vya uchumi Kati ya mtu binafsi na serikali
 
Katiba mpya ni dai linalotokana na utashi wa kisiasa kwa kiwango kikubwa lakini pia ni zao la mwamko mkubwa wa wananchi kuchoshwa na namna wanavyoongozwa.

Na mara nyingi kuchoshwa huku lazima kutokane na kukata tamaa ya maisha kwa walio wengi lakini pia kupata mwamko mkubwa wa elimu ya uraia.

Bahati mbaya ni kwamba wapigania katiba wa sasa wanataka katiba iwasaidie kwenye mapambano ya kisiasa, ndio maana hii ajenda ni ngumu sana.
Maelezo au sababu ulizotoa kuwa ndio msingi wa "madai na mahitaji ya Katiba" SIYO YA KWELI, NI UONGO UNAOTOKANA NA UTASHI WAKO WA KISIASA TU!
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom