Mnaosumbuliwa na UTI pita hapa

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,525
Eti Dawa ya UTI unauwita ni ugonjwa katika karne kama hii ukiwa kwenye bara la watu weusi hususani Tanzania, wapo watu wanavituko kwelikweli wanakwambia wanaumwa UTI kila mara, UTI sio ugonjwa shida hapa watu hawajui ni kuwa makampuni ya madawa yanategeneza dawa za UTI ikiwa wao wenyewe hawajui Chanzo cha UTI hivyo asilimia ya wengi wanaomeza madawa ya UTI wengi hawaponi na zaidi wanakunywa dawa hizo kisha tatizo linabaki palepale leo hii utakaposambaza na kupenda ukrasa huu utakuwa Wa kwanza kuto ugua wala kunywa tena madawa ya UTI mwiko.

UTI haitokani na vimelea wala wadudu , bali UTI inatokana na mazoea au mtindo wa watu kubanwa mkojo kwa mdaa mrefu kisha wao wakaubana kwa kipindi wanaubana acid inayopatikana kwenye mkojo ni 638.92gml ambapo acid hii inategemea kiwango cha maji ulichotumia ndani ya masaa 48, hivyo Acid hii huenda kuchoma kwenye njia ya mkojo na kupelekea kuta za povu kujitunga hapo ndipo UTI uanzia,Ndio maana ukiwa na UTI utaona vitu vizito mfano wa usa unatoka hayo ndio mapovu yaliokwisha jiegemeza kwenye kuta na ili upone UTI ni kwa kusafisha kuta hizo na sio kusema unywe dawa uwe wadudu wa UTI.

Pili UTI unaweza kuipata kama utafanya Sex na mtu ana uchafu (hajisafishi vyema) hasa jasho au ameshiriki tendo na watu wawili bila kujifanyia usafi sahihi hivyo wakati wa tendo la ndoa ume au uke unaposukuma ndani au kwenda nje kuna nguvu Fulani ya force husukuma majimaji ya mwanamke yale machafu kumwingia mwanamme kwenye njia ya mkojo na kwa mwanamke ule uchafu mweusi unaingia kwenye njia ya kizazi hadi kwenye njia ya mkojo hivyo chafu hizi zinapofika huko hutuga bacteria na kuta la vimelea wabaya sasa hii ndio UTI ambayo wengi huchanganya na ile ya kwanza .

Ukibahatika kuwa Tanzania, kuka mahali zipo choo chafu za kulipia zinanuka ukienda kwenye sehemu ya kukojolea wanaume tazama kwa makini zile kuta utaona zimekuwa mfano wa rangi ya maziwa ukiugusa utandao huo utaona ukauwa kama mapovu au maziwa hayo ndio mfano wa masalia yanayobaki kwenye njia ya mkojo na kusababisha UTI na wala sio wadudu wala bacteria.

Ili uweze kuitibu UTI unahitaji uzingatie baya
1-Usikae na mkojo kwa mdaa mrefu.
2-Ndani ya masaa 24 hakikisha umetumia Lita 6(mwanamke) na 8-10 kwa siku.

Jinsi ya kutibu UTI
Ukichanganya tangawizi + limao na maji utatibu UTI ambayo inatoa mkojo umchafu na mwekundu .

Ukichanganya magadi + limao na majibutatibu UTI ambayo imepanda kwenye figo.

Ukichanganya kitungu swaumu + chumvi na maji utaweza kutibu UTI Kali kwa mtu mvuvi wa kunywa maji mengi.

Ukichanganya mwarobaini + mchaichai na maji utaweza kutibu UTI sugu ya mdaa mrefu zaidi.

Ukichanganya majani ya mzambarau + magome ya mti wa embe na maji utaweza kutibu UTI iliyodumu kwa siku 7 mfululizo.

Ukichanganya majani ya molinga + majani ya mabua utaweza kutibu UTI iliyopanda kwenye figo juu.

*Ulichokuwa hujui?
Dawa za Hospital hazitibu UTI 100% ila watakacho kwandikia ni kunywa 2*3 ambapo kwa kila kidoge huwekewa compound ya SLD ambayo itakufanya/ kuchochea kunywa maji kati ya glass 3-5 kwa siku hivyo kinachotibu UTI kwa asilimia zote ni matumizi ya maji mengi na uyatoe kwa wakati kupitia haja ndogo.

Na Dr.Willium Mtanzania wa USA Marekani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya mambo yanachanganya sana sasa huyu mbona anasema hivi

1663489204471.png
 
Bwana Eisteen hayo uliyaandika halo juu naweza kuuita uongo uliopitiliza. Hi fan I ya uganga wa mwili wa binadamu waachie waliosomea fani hiyo. UTI kirefu chake ni Urinary track infection. Inaletwa na bacteria waitwao E. coli au Klebsilla spps na wengine wachache. Shida iliyopo ni kuwa UTI ni mpaka ufanye culture ya mkoja wa asubuhi na kuweza kuwaona hawa bakteria na kufanya sensitivity testing ili kuweza kujua Dawa ya kutibu. Majority ya hospitali zetu humpa mgonjwa diagnosis ya UTI kwa kupima mkojo wowote kwenye darubini au kutokana na dalili tuu. Hi hawezekani na jinai. Hivyo fuse waangalifu sana unapoambiwa una UTI. Mwisho, udanganyifu upo pia kwenye Typhoid.
 
Apo kwenye michanganyiko ya dawa mfano mwarobaini na mchaichai maji yawe ya Moto au balidi doctor 🙏🙏🙏
 
Eti Dawa ya UTI unauwita ni ugonjwa katika karne kama hii ukiwa kwenye bara la watu weusi hususani Tanzania, wapo watu wanavituko kwelikweli wanakwambia wanaumwa UTI kila mara, UTI sio ugonjwa shida hapa watu hawajui ni kuwa makampuni ya madawa yanategeneza dawa za UTI ikiwa wao wenyewe hawajui Chanzo cha UTI hivyo asilimia ya wengi wanaomeza madawa ya UTI wengi hawaponi na zaidi wanakunywa dawa hizo kisha tatizo linabaki palepale leo hii utakaposambaza na kupenda ukrasa huu utakuwa Wa kwanza kuto ugua wala kunywa tena madawa ya UTI mwiko.

UTI haitokani na vimelea wala wadudu , bali UTI inatokana na mazoea au mtindo wa watu kubanwa mkojo kwa mdaa mrefu kisha wao wakaubana kwa kipindi wanaubana acid inayopatikana kwenye mkojo ni 638.92gml ambapo acid hii inategemea kiwango cha maji ulichotumia ndani ya masaa 48, hivyo Acid hii huenda kuchoma kwenye njia ya mkojo na kupelekea kuta za povu kujitunga hapo ndipo UTI uanzia,Ndio maana ukiwa na UTI utaona vitu vizito mfano wa usa unatoka hayo ndio mapovu yaliokwisha jiegemeza kwenye kuta na ili upone UTI ni kwa kusafisha kuta hizo na sio kusema unywe dawa uwe wadudu wa UTI.

Pili UTI unaweza kuipata kama utafanya Sex na mtu ana uchafu (hajisafishi vyema) hasa jasho au ameshiriki tendo na watu wawili bila kujifanyia usafi sahihi hivyo wakati wa tendo la ndoa ume au uke unaposukuma ndani au kwenda nje kuna nguvu Fulani ya force husukuma majimaji ya mwanamke yale machafu kumwingia mwanamme kwenye njia ya mkojo na kwa mwanamke ule uchafu mweusi unaingia kwenye njia ya kizazi hadi kwenye njia ya mkojo hivyo chafu hizi zinapofika huko hutuga bacteria na kuta la vimelea wabaya sasa hii ndio UTI ambayo wengi huchanganya na ile ya kwanza .

Ukibahatika kuwa Tanzania, kuka mahali zipo choo chafu za kulipia zinanuka ukienda kwenye sehemu ya kukojolea wanaume tazama kwa makini zile kuta utaona zimekuwa mfano wa rangi ya maziwa ukiugusa utandao huo utaona ukauwa kama mapovu au maziwa hayo ndio mfano wa masalia yanayobaki kwenye njia ya mkojo na kusababisha UTI na wala sio wadudu wala bacteria.

Ili uweze kuitibu UTI unahitaji uzingatie baya
1-Usikae na mkojo kwa mdaa mrefu.
2-Ndani ya masaa 24 hakikisha umetumia Lita 6(mwanamke) na 8-10 kwa siku.

Jinsi ya kutibu UTI
Ukichanganya tangawizi + limao na maji utatibu UTI ambayo inatoa mkojo umchafu na mwekundu .

Ukichanganya magadi + limao na majibutatibu UTI ambayo imepanda kwenye figo.

Ukichanganya kitungu swaumu + chumvi na maji utaweza kutibu UTI Kali kwa mtu mvuvi wa kunywa maji mengi.

Ukichanganya mwarobaini + mchaichai na maji utaweza kutibu UTI sugu ya mdaa mrefu zaidi.

Ukichanganya majani ya mzambarau + magome ya mti wa embe na maji utaweza kutibu UTI iliyodumu kwa siku 7 mfululizo.

Ukichanganya majani ya molinga + majani ya mabua utaweza kutibu UTI iliyopanda kwenye figo juu.

*Ulichokuwa hujui?
Dawa za Hospital hazitibu UTI 100% ila watakacho kwandikia ni kunywa 2*3 ambapo kwa kila kidoge huwekewa compound ya SLD ambayo itakufanya/ kuchochea kunywa maji kati ya glass 3-5 kwa siku hivyo kinachotibu UTI kwa asilimia zote ni matumizi ya maji mengi na uyatoe kwa wakati kupitia haja ndogo.

Na Dr.Willium Mtanzania wa USA Marekani

Sent using Jamii Forums mobile app

Ieleweke tiba ya ugonjwa wowote huusisha:
1: Historia(anachojisikia mgonjwa kwamba si sawa kwake).

2: Vitals(mwili kuonyesha utendaji wake).

3: Examination(kinachoonyeshwa na mwili kwa mkaguzi kupitia ukaguzi).

4: Differentials(wazo la matatizo ya mhusika baada ya kupitia 1-3).

5: Investigation(hutaji la mhusika kivipimo kwa kuzingatia 4 hapi juu, kukanusha au kuthibitisha).

6: Final diagnosis( muunganiko wa 1-5, kuthibitisha tatizo/matatizo).

7: Education(matumizi ya dawa, mabadiliko kwenye maisha kuendana na aina ya ugonjwa).

UTI
1: Inaweza kuwa na dalili
2: Inaweza isiwe na dalili

Hii hutegemea na eneo lililoathiriwa. Mfumo wa mkojo huanzia kwenye figo, ureta, kibofu na urethra. Hivyo, dalili hutofautiana.

MAAMBUKIZI
Kulingana na tafiti zilizofanyika. Wadudu maambukizi mengi ya UTI yanatokana na wadudu wanaoishi njia ya haja kubwa (E. Coli). Hivyo, watu wengi wamekuwa wakijiambukiza wenyewe.

Unaweza kupata UTI
1: Kujiambukiza/toka njia ya haja kubwa.
2: Matumizi ya uzazi wa mpango kama kiwambo na dawa za kuua mbegu za kiume
3: Kujamiiana
4: Kutokuwa na mfumo wa mkojo ulio vyema. Mfano: kuwa na kijiwe kwenye njia ya mkojo.

Visababishi
1: Wanawake (ukaribu wa tundu la mkojo na njua ya haja kubwa na urethra fupi)
2: Kutokunywa maji ya kutosha (kupunguza kiasi cha mkojo na idadi ya kujisaidia, hapo hutoa nafasi ya wadudu kuzaliana).
3: Wanawake kukoma hedhi
Hubadili vichoche na ulinzi wa mfumo wa mkojo.
4: Ugonjwa kama kisukari.
Hupunguza mfumo wa kinga na kuweka sukari ambayo bakteria hujistawisha nayo.
5: Kuzaliwa na matatizo ya kimaumbile ya njia ya mkojo.
6: Kutumia dawa au vimikinika vyenye muwasho sehemu za kike kama tampuu, deodorant nk.
7: Ngono isiyo salama
8:

VIPIMO
1: Urinalysis(urine routine)/matumizi ya machine maalumu kutambua uwepo wa seli nyeupe za damu.
Hii hutumia uwepo wa kiasi kikubwa cha chembechembe nyeupe za damu kwenye mkojo isivyo kawaida(kiwango kinachotakiwa). Uwepo wa seli hizi kwa kiasi kikubwa huthibitisha shambulio la wadudu wageni ndani ya mfumo wa mkojo. Pia uwepo wa Nitrate kwenye mkojo ni kiashiria kingine cha uwepo wa maambukizi ukiunganisha na hali ya mgonjwa.
Kuna mambo mengine mengi yawezatambuliwa toka mwilini kwa kipimo hiki pia.

2: Microscope/darubini
Ni kipimo kunachohitaji utaalamu wa kuangalia seli nyeupe za damu kwenye mkojo. Huitaji kuwa mtaalamu mzuri wa utambuzi na kuhesabu pia kitendea kazi kizuri. Kuna mambo mengine mengi yanaweza kutizamwa kwenye mkojo pia kupitia kipimo hiki.

3: Urine culture and sensitivity/uoteshaji mkojo
Lengo hapa huwa ni kutambua aina ya mdudu na aina ya dawa ambayo inaweza kutumika kutibu tatizo husika, hasa kwa wadudu waliojenga usugu.

Kulingana na wadudu wanaosababisha UTI, kuna dawa ambazo zinaeleweka kwa wataalamu wa afya kufanya vyema/sensitive. Yaani huweza kuwaua wadudu husika, hivyo ni haki na ni salama kuanzisha dawa kwa kuzingatia hilo.

Mambo huwa tofauti pale wadudu husika wanapokuwa wamejenga usugu na aina hizi za dawa.

Hivyo, kupata dawa bila kufanya culture si tatizo. Ila utibiaji utatofautiana:
1: Kama ni mara ya kwanza kukutwa na UTI(pata tiba au fanya culture)
2: Kama ulishapata tiba na bado UTI ipo(fanya culture).

Ufanyaji culture unaweza kufanyika kulingana na:
1: Upatikanaji wa kipimo(kuna maenei huduma haipatikani, hivyo maamzi hutegeme).

2: Uwezo wa kumudu gharama( je mgonjwa anamudu gharama husika).

3: Hali ya mgonjwa(kuna wagonjwa wataanzishiwa dawa na kufanya culture au kusubiri majibu ya culture ili kuanza dawa).

KUJIKINGA
1: Zingatia kutatua changamoto kwenye visababishi.
2: Tuamia dawa kwa usahihi unapogundulika kuwa na tatizo husika.
3: Usitumie dawa pasipo kuthibitisha tatizo husika.
4: Pata tiba mapema na kwa usahihi mara unapopata dalili na hatimaye kuthibitisha tatizo.
 
Back
Top Bottom