mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,760
- 35,205
Wamachinga ni wananchi kama wengine na wana haki ya kuishi mijini kama watanzania wengine. Mkitaka kuwahamisha hakikisheni mmeandaa mazingira ambayo hayataathiri biashara zao, maana hii ndio kazi inayowafanya wazilee familia zao na kusomesha watoto.
Hawa watu hawakupenda kuwa wamachinga kwahiyo wasionewe. Ma RC, DC, DED msitumie police vibaya kuwafukuza hawa, wala msiwapeleke ambako hawawezi kufanya biashara. Mkiona hamuwezi acheni kazi; nyie mmeteuliwa ila Mimi, Samia, Wabunge na Madiwani ndio tulizunguka kuomba kura na ndio tunajua shida za wananchi.
Serikali ndio ilitengeneza hawa wamachinga kwa kuwa na mifumo mibaya. Na hawa wamachinga wameonewa zaidi ya miaka 50 huku wanaoona wao ni wa class ya juu wakipendelewa. Sisi tunawasaidia hawa maskini.
Wamachinga na nyie mfuate taratibu. Msijenge mabanda kila mahali fanyeni biashara zenu bila kuathiri miji yetu - JPM.
Mnaosema JPM ndio aliwaambia wamachinga wajenge mabanda kila mahali sikilizeni maagizo yake halafu waulizeni hao viongozi wanaoshindwa kusimamia wananchi kwanini hawafuati maelekezo ya serikali.
Endelea kupumzika salama shujaa JPM
Rais wetu mama SSH kazi iendelee
Mungu ibariki Tanzania