Mnaonaje timu ta Taifa Ikiitwa "The Tanzanites" badala ya jina hili la sasa " TAIFA STARS"

Hiyo timu haiwezikulibeba jina la Tanzanites (Ni kubwa mno). Halahala msijeshusha thamani ya hayo madini!
 
Iitwe Gonjwa la Moyo au iitwe Mnyika....


Hili Litimu hakika Silipendi sababu huwa Sipendi Kukereka ndio Maana nashabikia Manchester United
 
Muungano unakaribia Kufa hiyo Tanza anzeni kuifuta modomoni mwenu.. Neno la Tanganyika liwekeni Mioyoni Mwenu....
 
Ikiitwa TANZANITE ndio itamfanya MRISHO NGASA awe kama MESSI?na ule uwanja wa KARUME uwe kama OLD TRAFFORD?.....TAIFA LENYE VIONGOZI DHAIFU UZALISHA WATU WENYE MAONO DHAIFU.
 
Kwanza naliona kama vile linagundu, za naidi ya hapo..haliwakilishi utaifa wetu..historia ya taifa latu inauhusiano gani na nyota?? nani alifikia uamuzi wa kuipa timu yetu jina la taifa stars...angalia majina ya timu za taifa za nchi nyingine...walau yanaleta maana..England " the three lions", Italia " The Azzuri" France " Les Blues" , Ivory Coast " The Elephants" ,Algeria " Atlas Lions" na kadhalika na kadhalika, nadhani umefika wakati muafaka wa kuwa na jina jipya la timu yetu ya taifa , jina ambalo kwa kiasi flani litawakilisha uhalisia wa taifa letu na historia yake..pamoj ana maliasili tulizo nazo mfano hili " The Tanzanites" naona litazidi kuitangaza nchi yetu kama sehemu pekee hapa Duniani ambapo madini haya hupatikana...Naomba kuwasilisha...

Jina zuri lakini umesahau kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekaribia mwisho. Timu yetu ya Tanganyika tayari ina jina - Kilimanjaro Stars
 
"Taifa Stars" bado ni jina zuri zaidi kuliko yaliyopendekezwa hapo juu...Mosi linatangaza lugha ya Kiswahili duniani kwani yeyote wa nje atauliza nini maana ya neno 'taifa'. Pili liliasissiwa na mmoja wa viongozi makini wa soka nchini Kanali Abdallah( km sikosei) huyo alikuwa kiongozi wa FAT miaka ya 70 ama 80 na alikuwa na timu ya taifa huko Nigeria na aliposhtukizwa kwa swali la kizushi kuwa timu yao ya taifa inaitwaje kwa jina la utani ndipo akajikuta akitamka 'taifa stars'.
 
Back
Top Bottom