Mnaonaje timu ta Taifa Ikiitwa "The Tanzanites" badala ya jina hili la sasa " TAIFA STARS" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnaonaje timu ta Taifa Ikiitwa "The Tanzanites" badala ya jina hili la sasa " TAIFA STARS"

Discussion in 'Sports' started by stroke, Jun 19, 2012.

 1. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,407
  Likes Received: 6,597
  Trophy Points: 280
  Kwanza naliona kama vile linagundu, za naidi ya hapo..haliwakilishi utaifa wetu..historia ya taifa latu inauhusiano gani na nyota?? nani alifikia uamuzi wa kuipa timu yetu jina la taifa stars...angalia majina ya timu za taifa za nchi nyingine...walau yanaleta maana..England " the three lions", Italia " The Azzuri" France " Les Blues" , Ivory Coast " The Elephants" ,Algeria " Atlas Lions" na kadhalika na kadhalika, nadhani umefika wakati muafaka wa kuwa na jina jipya la timu yetu ya taifa , jina ambalo kwa kiasi flani litawakilisha uhalisia wa taifa letu na historia yake..pamoj ana maliasili tulizo nazo mfano hili " The Tanzanites" naona litazidi kuitangaza nchi yetu kama sehemu pekee hapa Duniani ambapo madini haya hupatikana...Naomba kuwasilisha...
   
 2. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hilo jina ni zuri, ila kiukweli kutokana na sisi wenyewe kutokuwa makini bado hilo jina litatatiza walimwengu. Nasema hivyo kwasababu, ingawa Tanzanite inapatikana hapa tanzania tu, ila cha kushangaza kwenye takwimu za mauzo katika masoko, inaonekana kuwa inatoka South Africa, na angalau hata Kenya pia. Kutokana na uzembe huu, walimwengu wanaweza fikiri hiyo timu ni ya South Afrika, ama wakijichanganya sana Kenya. Nashauri turudishe uzalendo kwanza, then tujipange kwenye mambo mengine vizuri zaidi.
   
 3. s

  siyabonga Senior Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani uko sahihi. Pamoja na vigezo ulivyovitaja, tuweke pia dhana ya ushindani katika jina. Mfano wenzetu wanatumia majina na taswira zenye uwakilishi wa nguvu na ushindani,kama vile tai, simba, tembo, cranes, harambee,nk. Tubadilishe majina haya yasiyo na maana yoyote wala ushindani. Maybe, nyota? Tunawaangazia wengine watufunge na kuiba rasilimali zetu!

  Equally, ni muhimu pia kufikiria hata maeneo mengine muda muafaka utakapofika. Mfano bendera ya taifa, imepooooza mno! Inakosa rangi ya muhimu mno, nyekundu. Mashujaa wetu kina mkwawa, waliopigana vita vya majimaji na vingine, wote hawa walikuwa wanapigania uhuru na minyororo ya kutawaliwa! Ni kupotosha historia kusema hatukumwaga damu! hizi ni dhana za kubweteka na upotoshaji na kuwafanya watu hawaelew:embarrassed:i kinachoendelea. Tume ya Jaji Warioba tuzingatie hili.
   
 4. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,859
  Likes Received: 4,544
  Trophy Points: 280
  Tanzanites zingekuwa na faida kwa taifa,basi ningekuunga mkono.
   
 5. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,407
  Likes Received: 6,597
  Trophy Points: 280
  Huoni kuwa ndio itakuwa njia sahihi ya kuujulisha ulimwengu kuwa tanzanites hazitoki huko wanapojua wao bali tanzania pekee..
   
 6. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,407
  Likes Received: 6,597
  Trophy Points: 280
  Wazo lako la kuwa na majina ya kiushindani ni zuri sana, ila nimependekeza jina hili kama kianzio cha kupata mbadala wa hili la sasa ambalo naona halina tija, mvuto wala uhalisia wa historia..Nyota??? nyota zimefanya nini??
   
 7. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,025
  Likes Received: 744
  Trophy Points: 280
  Itakuwa sawa na kikombe kipya chai ile ile.
   
 8. k

  kiparah JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,176
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Tanzanites kwa kiingereza inawakilisha mwanamke!
   
 9. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mkaliwakitaa, jana nilitaka kubandika poll tupendekeze majina mapya kwa ajili ya Taifa Stars, jina la Tanzanites lilinijia na linafaa sana maana ni special and unique.
  Nakuunga mkono, Taifa Stars iitwe The Tanzanites.
   
 10. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,407
  Likes Received: 6,597
  Trophy Points: 280
  Linaweza kuwa hilo au jingine lolote , ila si ajabu kwa jina kuwa na maana zaidi ya moja..ila jambo la msingi ni kuwa tunalitumia tukimaanisha nini..tutaeleweka tu
   
 11. o

  obseva JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 80
  Mimi naona kama tunapoteza tu, ndiyo jina ni muhimu sana, lakini si kwa hapa tulipo. Mbona hata hayo majina yaliyotwa hapo juu na momoja wa wachangiaji watu hawangaiki nao, watu wanaziita timu kufuatana na taifa lake. mfamo utakuta watu wanasema Ufaransa inacheza na Uingereza, wala hakuna " the three lions" Or " Les Blues". Mimi naona mjadala huu ni mzuri lakini wakati bado. Kwa sasa tungejikita kufundisha vijana wacheze soko la kufa mtu muone kama Tanzania haitagitangaza na kupewa heshima inayostahili, watu wanataka "substance" Sio majina, mtu yeyote au kitu chochote hakifahamiki jina au hakipewi heshima kwa jina isipokuwa kwa kinachotoa au kuonyesha.

  Mnafikiri jina ndo litakuza kiwango cha mpira? au litavutia wawekezaji kuja kujenge viwanja? au ndo watu wataamka na kutengeneza program bora za kufundishia michezo? au TBL,NMB na etc watachangia zaidi kwenye kapu la mpira. Sidhani kama kweli tukibadilisha jina ndio mwarobaini wa kutibu matatizo yetu ya kisoka. Nafikiri hata Afrika ya kusini waliingia kwenye mjadala kama huu, sijui kama kuna ushahidi umewasaidia kujitangaza zaidi.

  Kwanza watu wafahumu, jina zuri ni lile linaloleta [FONT=&quot]furaha na fahari kwa watu wake [/FONT]na sio kwa wageni,ni kama Amali fulani na likitajwa linaleta hisi za haraka na kumbukumbu kwa wahusika mfano "three lions" kwa Waingeleza lina maana kwao ambayo sio muhimu Tanzania mkaifurahia pia " Les Blues" kwa wafaransa. Hivi Tanzanite imetusaidia nini? imeleta ufahari gani? zaidi ya kusema yetu,yetu,yetu na wenzenu wana kula na kushiba, mara Afrika ya kusini hee Kenya nyie kufia kwenye mashimo mbuguni, na watu wamebaki na masononeko mioyoni lakini eti inapatikana Tanzania tu. Pia mfano Tanzanite ikaisha leo hilo jina linakuwa na sura na umuhimu gani baada ya miaka 20??

  Kwangu mimi taifa Stars bado ni jina bora kwetu sisi kwani linaonyesha [FONT=&quot]Umiliki wetu na Umoja wetu[/FONT] na [FONT=&quot]utaifa wetu[/FONT], lakini kwa baadaye baada ya timu yetu kufika viwango vizuri laweza kubadilishwa kwa kuzingatia mantiki na hoja nilizo ziweka.

  Natoa hajo.
   
 12. s

  sawabho JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja ya kubadilisha jina ila lisiwe Tanzanite kwa sababu watu wa nje watafahamu kuwa hiyo ni Timu ya Kenya au Afrika Kusini. Aidha, kwa kuwa kwa muda mrefu timu ya Taifa imekuwa haifanikiwi kimichezo, ni afadhali itumike kutangaza utalii kuliko kwenda nje inafungwa na kurudi bila faida, sasa faida itakuwa kutangaza utalii. Nashauri ipewe jina ambalo mtu akilisikia tu asiulize kuwa hicho kitu kiko wapi ? Maana Tanzanite ingawa ianatoka Tanzania lakini wazalishaji wakubwa ni Kenya na South Africa. Iiite timu hiyo "Simba wa Manyara" ikimaanisha wale simba wenye uwezo wa kukwea miti.
   
 13. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,407
  Likes Received: 6,597
  Trophy Points: 280
  Simba wa manyara linaleta maana na faida
   
 14. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,407
  Likes Received: 6,597
  Trophy Points: 280
  Yote uliyozungumza yana nafasi yake, ila jina pia hatuwezi acha kuona umuhimu na mchango wake..kwani linakuwa kielelezo cha tamadumi, na historia ya wahusika..ukijaribu kufuatia hata histori aya majina ya hizo timu nilizozitaja utaona pia yalitolewa katika lengo la kuhamasisha wachezaji na wananchi pia ...jina pekee linaweza kuwa msingi wa uhamasishaji katika msingi...ushindi si katika mambo makubwa tu kama uliyoyasema wewe hata katika mambo madogo kama hayo..
   
 15. s

  sawabho JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Linatangaza utalii wa nchi yetu. Kumbuka nimesema timu imekuwa ikifanya vibaya katika mchezo, sasa itumike kutangaza utalii. Aidha, elewa kwamba hata wewe ukibadilisha jina na kitwa.. Bill Gates.....huwezi kuwa tajiri kama Bill Gates kama huna bidii. Kumbe kinachotakiwa sio kutafuta jina zuri kwa ajili ya hii timu, bali kuijenga ili ifanye vizuri. Kama timu itafanya vizuri hata Taifa Stars halina shida, watu wa nje wata-google wenyewe kuifahamu zadi hiyo timu na nchi yake. Kwani ukimwita Marehemu jina la Hayati anakuwa tofauti ?
   
 16. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #16
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,025
  Likes Received: 744
  Trophy Points: 280
  Iiitwe kichwa cha mwendawazimu.
   
 17. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,407
  Likes Received: 6,597
  Trophy Points: 280
  Kama chako..watu tupo serious hapa, this is JF to remind you.
   
 18. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #18
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,356
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Tanzaniate ni nzuri, lakini tutafute jina ambalo litakuwa linatangaza kivutio mojawapo ambalo linalodumu na halitaweza kupotea milele, Tunaweza tukaliita "Udzungwa stars" kwa maana kuna mlima wenye water fall yenye urefu wa mita mia mbili, na kila siku waterfall ipo pale na mlima upo pale haufutiki! Jina Udzungwa ni tamu au mnasemaje wakuu?
   
 19. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #19
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,025
  Likes Received: 744
  Trophy Points: 280
  You don't know what you are doing.
   
 20. POLITIBURO

  POLITIBURO Member

  #20
  Jun 20, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 41
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana JF, mjadala wa jina la timu ya soka ya Tanzania umekuja wakati muafaka. Ebu tukumbuke enzi hizo Kombe la Taifa likiwa na mashamushamu ya kila aina ambapo wkeli soka lilichezwa. Tujikumbushe majina ya timu zetu za mikoa naamini kila mmoja anayamaizi. Kumbuka timu ya DSM ikiitwa Mzizima Utd, Kagera ikiwa Rweru Eagles, Arusha Meru Warriors, Shinyanga wakiwa na Igembe Nsabo, Mbeya Mapinduzi, nk. Haya majina yanamaanisha kitu na yanabeba uhalisia wa kitu ama uwe mkoa au uwakilishi wa eneo husika n.k. Sasa, wakati umefika, kwa timu ya taifa hatuna haja ya kuigiza kwa wengine mfano eti nyota au wanyama. Tunacho kitu cha pekee nacho ni mlima KILIMANJARO. Mi kwa maoni yangu timu yetuiitewe Kilimanjaro. Tunajua Kilimanjaro ni mlima wetu, ni mlima mrefu wa Volcano Afrika, kuna mbuga pale, ni kivutio siyo kwa watalii tu bali kwa yeyote apataye fursa ya kuutazama au kuona picha yake. Mlima unapendeza Lakini kuupanda ni shughuli pevu, Too tough to climb! lakini zaidi ya yote twatujua "Kilimanjaro is the tallest free standing mountain in the world". Hii ndo fahari yetu. Hivyo, wapinzani wetu watajua, kucheza au kuishinda Tanzania ni kazi kubwa sawa na kuupanda mlima. Tukumbuke wengi upenda kuupanda, na wengine ujaribu kuupanda mlima huu akini wanaofanikiwa kufika kileleni ni wachache, na hao wachache wanaofika kileleni wanakuw hoi. Vivyo hivyo, kucheza na Tanzania tu peke yake kwa jina liwe tishio na kuishinda iwe kazi ngumu sawa na kuupanda Kilimanjaro. Pia, jezi zetu ziwe na nembo ya mlima Kilimanjaro hii iwe alama ya kilicho chetu. Naamini wachezaji na mashabiki wataiona dhamana walioyo nayo kwa kuilinda na kuiteteza Tanzania popote pale. Hivyo, ni maoni yangu kuwa timu yetu iitwe KILIMANJARO.
  Naomna kutoa hoja
   
Loading...