Mnaonaje kama watumishi wa serikali na taasisi kubwa binafsi wakianza kulipwa mishahara yao kila baada ya wiki mbili na sio wiki nne (mwezi mmoja)?

Mishahara yenyewe hata ukiikusanya ya miezi 6 pesa yenyewe haijai hata kikombe cha Lita moja , je tukilipana kwa wiki?
 
Achana na wiki 2, wafanyakazi wanatakiwa walipwe per hour.

Unforgetable

Manners Maketh Man

Hiyo ndo nzuri, payment per production ndo mpango mzima ambao haumnyonyi mfanyakazi wala mwajiri.

Unalipwa kulingana na ulichozalisha, ukazalisha kidogo na malipo yako yanakuwa madogo. Ukizalisha kwa wingi posho yako nayo inakuwa kubwa.

Hii itaondoa wavivu wote na bla bla mingi kazini!
 
Mnaonaje kama watumishi wote wa serikali pamoja na wale wa taasisi kubwa binafsi wakianza kulipwa mishahara yao kila baada ya wiki mbili na sio wiki nne (mwezi mmoja) kama ilivyozoeleka sasa?

Wenzako hakukaliki kwenye viti kampeni imepamba moto huko sidhani kama watakuelewa
 
Hiyo itawapunguzia wafanyakazi milima wanayokumbana nayo kabla yakuzifikia wiki 4
Ndio hivyo mkuu. Wafanyakazi wanapitiaga wakati mgumu sana ifikapo tarehe 15.

Kama mtu kwa mwezi take-home ni 700,000/=, basi apewe 350,000/= tarehe 14 kisha nusu iliyobaki tarehe 28
 
Back
Top Bottom